Swali Fyatu: Walitaka Rais afanye nini hasa baada ya ripoti ile?

Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,917
2,000
Tundu Lissu aliandika jinsi Evo Morales rais wa Bolivia alivyoitoa katika mikataba mibovu nchi yake.

Alianza kuitoa Bolivia katika international conventions zinazolazimisha nchi kufanya arbitration London na vifungu kama hivyo.

Ukianzia hapo, rais kama sovereign wa nchi, anakuwa kavuka kiungi cha kuwa na kesi itakayoamuliwa London ambako tutashindwa tu.

Kisha baada ya hapo ndipo unavunja hii mikataba.

Wakipeleka kesi London baada ya sisi kujitoa kwenye conventions, Tanzania inakuwa hailazimiki kwenda kwenye hiyo kesi kwa sababu inakuwa si signatory wa international conventions zinazoitaka iende huko.

Sasa Magufuli kakurupuka.

Anavunja mikataba kabla ya kujitoa katika conventions.

Kesi itapelekwa London. Tanzania itashindwa. Tutawalipa tena kama IPTL hata kama hawachimbi madini.

Magufuli katulisha hasara mara mbili.

Mwanzo alivyokaa kimya kama waziri wa cabinet iliyopitisha hii mikataba. Yuko responsible.

Tena sasa alipovunja mikataba kiholela

Kwa mara nyingine nasema, tatizo la Magufuli ni kwamba, hata anapofanya jambo zuri, huwa analifanya vibaya.
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,917
2,000
Ninachosikitika ni kuwa tumelijua hili mapewa wakati wameshabeba madini ya kutosha... Sasa yamebaki mashimo ndio haya mapywa yanaibuka. Its so sad...
Kinachotokea hapa kama una imani ndogo unaweza kusema Magufuli kala njama na hao wawekezaji!

Kwa nini?

Ni kama vile Magufuli kahusika kupitisha mikataba mibovu alivyokuwa waziri katika cabinet iliyopitisha mikataba hii.

Magufuli amekuwa rais mwaka mmoja na nusu sasa. Hakuwagusa kabla. Kwa nini sasa?

Wawekezaji wamechota madini na mchanga wote mpaka sasa wanaona hakuna kilichobaki.

Wamekula njama na serikali iwavunjie mikataba kiholela.

Serikali inawavunjia mikataba kiholela na kuonekana inajali maslahi ya nchi. Wananchi wanashangilia Magufuli kidume.

Wawekezaji wanapeleka kesi London.

Serikali inashindwa na kutakiwa ilipe faini kubwa.

Wawekezaji ambao washamaliza kuchimba madini, badala ya kufanya biashara ya madini, watapata hela bila kuchimba madini kwa kulipwa faini na serikali ya Tanzania kutokana na serikali kuvunja mkataba.
 
SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
540
250
Nayaona machungu yako dhidi ya ACCACIA lakini pia mapendekezo yako nayaona yanapungukiwa utaalamu na umakini. Kutaka kampuni ya ACCACIA eti Rais angetangaza kuifuta siku hiyo hiyo, naona yangekuwa maamzi ya kukurupuka na yenye jazba zisizo na tija, nijazba ambazo zinafaa kutolewa kwenye mitandao ya kijamii kama ulivyofanya hapa jf. Kuifuta kampuni yeyote kunashitaji maamzi ya kisheria na kiuchumi ili kuona kuwa kwa kufanya hivyo kuna gharama zipi na nani atazigharamia na je uwezo wa kuzilipa tunazo? Pia kuna shida gani kiuchumi baada ya kuzilipa, watu ambao wameajiriwa humo nini hatma ya maisha yao? Nini matokeo ya kidiplomasia baada ya kuwafukuza ACCACIA? uamzi kama huu hauwezi kufanywa kwa kufurahisha nafsi za watu wachache kama mleta post hii. Baada ya uchunguzi wa kina huenda Rais na Taasisi yake watafikia hatua ambayo Taifa halitaingia kwenye msukosuko wowote. Amina.

Makusudically, Kwa kweli hakuna utaalamu wowote unaohitaji kujua kwamba unaibiwa. Nitaafiki na wewe kuwa unahitaji "umakini" kuelewa hivyo
Makusudically, Gharama ambayo mtanzania ameeingia ni kubwa zaidi ya hilo la kupelekana mahakamani na waha wezi. Tuulizane; Wafanyakazi wa Accacia waliopo Tanzania(migodini) ni wangapi wamenufaika na ajira hizo? Je kama wanavyodai uajiri wao ni manufaa wa wakina nani?, basi watuonyeshe (wafanyakazi tu, wa migodni) wamechangia kiasi gani kwenye mfuko wa taifa:-Ushuru walio lipa. Je maisha yao ni bora zaidi? Afya zao? Where is you phsyc? Naona mengi yanaweza kujibiwa na Kamati ya pili...kama utaafiki.
Kwa maoni yangu Jazba ndio zinazotupeleka kufanya maamuzi mengi hata pale tunapo kataa kuwa ni jazba iliyotufanya hivyo. Wananchi wa Tanzania, Waafrika kwa ujumla bado tunayo jazba kwa mambo ambayo tumefanyiwa na Ukoloni, na jazba ambazo wameweza kutupatia ni hofu, huzuni na hasira tu na tunabakiwa na mshangao mkubwa ati ni kwanini wanutufanyia haya mambo(hapa ni wizi wa rasilimali zetu) kwani sii sote sio wanadamu? kwani na sisi hatutaki manufaa?
Makusidically Je accacia walifikiria hayo? "Matokeo ya kidiplomasia"
Kwa kweli jazba ambayo hatujaweza kupata kutokana na wizi wao ni furaha, sasa kama kiongozi wa nchi anaweza kutupatia hilo, hata kama ni kwa mda sioni kwanini umekurupuka.
Sioni sababu unasisitiza tuwe na woga sioni sababu yako wewe kutishia Raisi wa nchi na taasisi yake kwani misukosuko huwa ni moja ya vitu ambavyo vinatokea sehemu yeyote ya kazi ikiwa na Ofisi ya Raisi wa nchi. We na Tundulisu et al. ndio wachache. Mjifikirie, kwani, hiyo "misukosuko" tuko tayari kupambana nayo. Na nina Uhakika Raisi wangu John Pombe Maghufuli atashinda.
 
THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,778
2,000
Hii nchi ina watu wa ajabu sana.Wale waliokuwa vinara wa kupinga ufisadi na nchi kuibiwa leo ndio wamekuwa vinara wa kutetea wezi wa kila namna.
Yani tuko tayari tuibiwe kuliko wezi wakamatwe na mtu tunayetofautiana vyama.
 
akazuba

JF-Expert Member
May 16, 2014
533
500
Ebu Nipe faida za kuendelea kuwa na mwekezaji kama Acacia?
Nayaona machungu yako dhidi ya ACCACIA lakini pia mapendekezo yako nayaona yanapungukiwa utaalamu na umakini. Kutaka kampuni ya ACCACIA eti Rais angetangaza kuifuta siku hiyo hiyo, naona yangekuwa maamzi ya kukurupuka na yenye jazba zisizo na tija, nijazba ambazo zinafaa kutolewa kwenye mitandao ya kijamii kama ulivyofanya hapa jf. Kuifuta kampuni yeyote kunashitaji maamzi ya kisheria na kiuchumi ili kuona kuwa kwa kufanya hivyo kuna gharama zipi na nani atazigharamia na je uwezo wa kuzilipa tunazo? Pia kuna shida gani kiuchumi baada ya kuzilipa, watu ambao wameajiriwa humo nini hatma ya maisha yao? Nini matokeo ya kidiplomasia baada ya kuwafukuza ACCACIA? uamzi kama huu hauwezi kufanywa kwa kufurahisha nafsi za watu wachache kama mleta post hii. Baada ya uchunguzi wa kina huenda Rais na Taasisi yake watafikia hatua ambayo Taifa halitaingia kwenye msukosuko wowote. Amina.
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,821
2,000
Kwako vile vile, nimefurahi kukuona upo. Tatizo hata tukianza huko sijaona nani mwingine ambaye anaweza hata kutuonesha njia! Angalau chini ya JPM njia tunaitafuta na ikibidi tunatengeneza njia nyingine! Labda waje watu wengine kabisa na sijui watatoka wapi
Good intentions don't always lead to good outcomes.

Binafsi, I don't question his intentions, nina shida na process. Ameingia kwenye mchakato na closed mind tena na lengo moja tu, kukomesha wizi huu!

Lakini hakuna anayenyanyuka kutuambia mwizi ni nani? Na kama yupo mbona hajachukuliwa hatua mpaka hivi sasa? Tutofautishe kati ya unfair na illegal; kama umepata unfair deal, huo ni UPUMBAVU wako, tafuta namna ya kutoka legally. Halafu fanya uchambuzi ujue, tumefikaje hapo, rekebisha makosa na yasijirudie tena. Tusilete ubabe kama tuko majumbani kwetu, let's fight but fight smart. There's a price to pay na hizi shenanigans, hata kama sio explicit cost zitakuwa implicit cost.

Mungu akitupa uhai by 2030 huko, tutalia kilio hiki hiki na mafuta na gesi
 
Kifyatu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,384
2,000
Hivi tuseme watu wanataka rais afanye nini na hiili la michanga? Aiachilie?
Nina uhakika hili swali lako ni rhetorical.

Kule Kusini hiki kinacholalamikiwa sasa kuhusu huu mchanga wanakiita "Ntima nyongo" au roho mbaya.

Magufuli anajaribu kutekeleza/kurekebisha vile vyote vilivyolalamikiwa na upinzani hapo awali. Kwa hiyo zile hoja zote za upinzani ambazo zingewapeleka Magogoni (kama isingekua ule uamuzi wao wa 2015) sasa zinatekelezwa na Magufuli. Hiki kitu kimewapoteza maboya kabisa.

Kwa hiyo swali lako linawasuta upinzani na kuwaambia watafute mikakati mipya ya kukuza upinzani na sio kumsakama Magufuli anaetekeleza sera zao.

Mkuu, tunahitaji upinzani mahiri wa kuisimamia serikali. Sio kila raisi atakuwa kama Magufuli. Kinachoendelea kutoka kambi ya upinzani lately leaves a lot to be desired.
 
service

JF-Expert Member
May 22, 2014
3,087
2,000
Tundu Lissu aliandika jinsi Evo Morales rais wa Bolivia alivyoitoa katika mikataba mibovu nchi yake.

Alianza kuitoa Bolivia katika international conventions zinazolazimisha nchi kufanya arbitration London na vifungu kama hivyo.

Ukianzia hapo, rais kama sovereign wa nchi, anakuwa kavuka kiungi cha kuwa na kesi itakayoamuliwa London ambako tutashindwa tu.

Kisha baada ya hapo ndipo unavunja hii mikataba.

Wakipeleka kesi London baada ya sisi kujitoa kwenye conventions, Tanzania inakuwa hailazimiki kwenda kwenye hiyo kesi kwa sababu inakuwa si signatory wa international conventions zinazoitaka iende huko.

Sasa Magufuli kakurupuka.

Anavunja mikataba kabla ya kujitoa katika conventions.

Kesi itapelekwa London. Tanzania itashindwa. Tutawalipa tena kama IPTL hata kama hawachimbi madini.

Magufuli katulisha hasara mara mbili.

Mwanzo alivyokaa kimya kama waziri wa cabinet iliyopitisha hii mikataba. Yuko responsible.

Tena sasa alipovunja mikataba kiholela

Kwa mara nyingine nasema, tatizo la Magufuli ni kwamba, hata anapofanya jambo zuri, huwa analifanya vibaya.
Mkuu kwani,kuna maamuzi yamefanyika kuwahusu hawa accasia, mbona kama mnatangulia mbele.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,291
2,000
Tundu Lissu aliandika jinsi Evo Morales rais wa Bolivia alivyoitoa katika mikataba mibovu nchi yake.

Alianza kuitoa Bolivia katika international conventions zinazolazimisha nchi kufanya arbitration London na vifungu kama hivyo.

Ukianzia hapo, rais kama sovereign wa nchi, anakuwa kavuka kiungi cha kuwa na kesi itakayoamuliwa London ambako tutashindwa tu.

Kisha baada ya hapo ndipo unavunja hii mikataba.

Wakipeleka kesi London baada ya sisi kujitoa kwenye conventions, Tanzania inakuwa hailazimiki kwenda kwenye hiyo kesi kwa sababu inakuwa si signatory wa international conventions zinazoitaka iende huko.

Sasa Magufuli kakurupuka.

Anavunja mikataba kabla ya kujitoa katika conventions.

Kesi itapelekwa London. Tanzania itashindwa. Tutawalipa tena kama IPTL hata kama hawachimbi madini.

Magufuli katulisha hasara mara mbili.

Mwanzo alivyokaa kimya kama waziri wa cabinet iliyopitisha hii mikataba. Yuko responsible.

Tena sasa alipovunja mikataba kiholela

Kwa mara nyingine nasema, tatizo la Magufuli ni kwamba, hata anapofanya jambo zuri, huwa analifanya vibaya.

Kwa hiyo ushauri wa Lissu ni kuwa Rais aitoe nchi kwenye hii mikataba ya kimataifa kwanza?
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,917
2,000
Kwa hiyo ushauri wa Lissu ni kuwa Rais aitoe nchi kwenye hii mikataba ya kimataifa kwanza?
Sijui Lissu amesema nini katika ukamilifu wa maneno yake.

Na sijui kama kuitoa nchi katika mikataba ya kimataifa (underlying multilateral conventions) ni ushauri mzuri, kwa sababu hilo linaweza kusababisha kile kinachoitwa "unintended consequences" ya kuwa na investment flight, wawekezaji kuona kama nchi inataka kutaifisha viwanda na biashara zote za wageni.

We have been there before (almost the same thing) with Azimio la Arusha. It did not work too well.

Unaweza kuwa mtego wa panya utakaonasa waliotakiwa na wasiotakiwa na kutuletea matatizo makubwa zaidi.

Kwa hiyo haya mambo si ya kuyasema kirahisi rahisi tu.

Ila ukweli ni kwamba Rais Magufuli amekurupuka na angeweza kufanya haya mambo kwa weledi zaidi, bila kujionyesha yeye ana nguvu zaidi.

Kwa sababu kashikwa pabaya. Mikataba waliyosaini ni mibaya na kesi ikipelekwa mahakama za usuluhishi London chances are most likely tutashindwa. Kwa sababu

1. Hatuna wanasheria wazuri wa kesi hizi. Kuna kipindi nchi ilikuwa inasaini mikataba hii wakati mwanasheria aliyekuwa ana qualifications za kimataifa kwenye mikataba hii alikuwa mmoja tu nchi nzima. Philip Marmo.

2. Hata kama tuna wanasheria wazuri, mahakama za usuluhishi za London ziko biased ku side na investors kwenye kesi kama hizi. Hiki ni kitu kinachojulikana, na ndiyo maana wanazipenda. Usuluhishi kutakiwa kuwa London tu ni ushindi wa aina fulani kwa wawekezaji.

Mzee wangu amefuatilia kesi hizi za usuluhishi London kwa niaba ya taifa miaka kumi in the nineties na walishinda kwa sababu ya strategic planning tangu mwanzo na hawakukurupuka kama Magufuli wala kuwa na mikataba mibovu to begin with. Ndipo nilipoanza kujifunza haya.

3. Rais Magufulikwa ubabe wake na kufanya mambo kwa pupa ameifanya kesi kuzidikuwa rahisi kwa investors na amefanya wao kuonyesha wanaingiliwa na serikalikuwa ni kitu rahisi zaidi.

Kuna mambo mengine yanataka kutumiaakilizaidi ya nguvu.Magufuli hajui hili.

Kuna mambo mengine mazuri lakini utekelezaji wake ukiwa mbaya yanageukakuwa mazuri.Magufuli haelewi hili.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom