Swali Fyatu: Utendaji wa Shughuli za Mahakama Unatungwa na Nani na Kwanini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Ni swali ambalo limetokana na yanayoendelea katika sakata la Mbowe. Wabunge wanarushwa mubashara. Tunasikia mawazo yao, malumbano yao, na hata ufyatu wao. Tunasikia wakishangilia na wakizodoa; tunawasikia wakicheka na kuchekana au kuchekeana. Vyombo vya habari vya taifa na vya binafsi vinapewa nafasi ya kuwahabarisha wananchi habari za yanayotokea Bungeni. Wanasema ni "haki ya kuwapa wananchi kupata habari".

Lakini pia tunaona mara kadhaa shughuli zikifanyika Ikulu au mahali ambapo Rais ni mgeni rasmi. Tunahabarishwa nini kinaendelea kwa sababu kuna imani kuwa ni kwa maslahi ya taifa. Hivyo, vyombo vya habari siyo tu vinaruhusiwa lakini Ikulu yenyewe ina "channel" yake ya kuwahabarisha wananchi na unapata video na clips za video huko Youtube kama ukitaka kurejea chochote kilichosemwa au kufanywa. Ni namna nyingine ya ukusanyaji na utunzaji wa rekodi mbalimbali.

Ndio maana swali langu linauliza vipi kuhusu Mahakama. Kama tunaamini katika mfumo wa Mihimili mitatu ni kwanini hadi leo hatujahabarishwa uwepo wa channel ya habari ya mahakama? Je, ni kwanini Mahakama nayo isiweke utaratibu wa shughuli za kesi kurushwa "live" badala ya kushindana na vyombo vya habari. Nina uhakika kwenye kesi ya Mbowe kwa mfano, watu wengine wala wasingejishughulisha kwenda mahakamani kama wangejua wanaweza kukaa waliko na kufuatilia kinachoendelea kupitia matangazo mubashara. Sasa ni nani anayewatungia Mahakama Utaratibu (regulations) za utendaji kazi wao wa kila siku. Ni nani anaweza kuamua kuhusu kutumia video na kamera kurusha matangazo; haiwezekani iwe kesi kwa kesi tu na maamuzi tu ya jaji mmoja mmoja.

Kama tunapata nafasi ya kuwaona viongozi wachovu wa hoja kwenye Bunge na sehemu nyingine nina uhakika tunahaki ya kuwaona pia watu wanaolipwa mishahara kutoka kodi za wananchi kuwa wapelelezi, wachunguzi, waendesha mashtaka - na wengine wakiwa wamesomeshwa na serikali wanajengaje hoja huko Mahakamani na kama hoja zao zina hoja au ni za vihoja.

Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma na uongozi wake wa mhimili wa Mahakama wanahitaji kukaa chini na kuamua mara moja ni nini sera ya matumizi ya kamera mahakamani - hilo moja na pili waamue ni lini na wao wataanzisha channel yao ya kuwapasha habari Watanzania ili Watanzania nao waweze kufuatilia kinachofanywa na mahakama zetu mbalimbali. Vinginevyo, tuache ufyatu wa kuaminishana kuwa mihimili hii mitatu iko sawa.
 
kitabu cha Supremacy of Law
Kitabu cha Jaji mstaafu B. Samata kimeelezea mapungufu mengi ya law reports and reporting

15 Apr 2021

kitabu cha Supremacy of Law

Prof. Chris Maina Peter, Mhariri wa kitabu cha Supremacy of Law akikichambua kitabu cha Supremacy of Law, cha Judge Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta, akikielezea nini kilichopo ndani ya kitabu hicho

  • Kesi ya rais awajibike kwa matendo yake
  • Lumumba to Mlimani journey
  • Army mutiny
  • Kesi ambazo Judge Samatta aliziamua toka akiwa acting judge mpaka jaji kamili
  • Vitu anavyokumbuka jaji Samatta
  • "A judge who is not independent, he or she is not a judge"
  • Mapungufu makubwa katika Law Reporting nchini Tanzania, Tanzania inaweza kuchukua miaka 16 kabla ya kutiwa ktk Law Report wakati nchi zingine wanachapisha chapuchapu
  • Advocates maarufu Eric Ng'maryo na Jenerali Ulimwengu hawakubali Jaji Samatta astaafu na kupotea, waapa watamfuatilia ili aendelea kuelimisha umma
  • Kwa kirefu kuna sehemu kubwa 8 ndani ya buku hili kubwa muhimu kusomwa
Source : Ngowi TV

Rejea zaidi za mhimili wa mahakama :

Nini kifanyike mkuu ili mahakama ziwe huru mkuu?
Kama Katiba mpya imeshindikana basi Rais asiteue majaji directly, majaji wapendekezwe na TLS, Rais apelekewe listi ya majina kuteua na uteuzi wao uthibitishwe na bunge.

Mtu akishakuwa jai asiteuliewe kushika nafasi nyingine yoyote.

Makosa yote yawe na dhamana.

Bunge ndio liwe mpangaji wa mwisho wa bajeti ya nchi.
 
Ni swali ambalo limetokana na yanayoendelea katika sakata la Mbowe. Wabunge wanarushwa mubashara. Tunasikia mawazo yao, malumbano yao, na hata ufyatu wao. Tunasikia wakishangilia na wakizodoa; tunawasikia wakicheka na kuchekana au kuchekeana. Vyombo vya habari vya taifa na vya binafsi vinapewa nafasi ya kuwahabarisha wananchi habari za yanayotokea Bungeni. Wanasema ni "haki ya kuwapa wananchi kupata habari".

Lakini pia tunaona mara kadhaa shughuli zikifanyika Ikulu au mahali ambapo Rais ni mgeni rasmi. Tunahabarishwa nini kinaendelea kwa sababu kuna imani kuwa ni kwa maslahi ya taifa. Hivyo, vyombo vya habari siyo tu vinaruhusiwa lakini Ikulu yenyewe ina "channel" yake ya kuwahabarisha wananchi na unapata video na clips za video huko Youtube kama ukitaka kurejea chochote kilichosemwa au kufanywa. Ni namna nyingine ya ukusanyaji na utunzaji wa rekodi mbalimbali.

Ndio maana swali langu linauliza vipi kuhusu Mahakama. Kama tunaamini katika mfumo wa Mihimili mitatu ni kwanini hadi leo hatujahabarishwa uwepo wa channel ya habari ya mahakama? Je, ni kwanini Mahakama nayo isiweke utaratibu wa shughuli za kesi kurushwa "live" badala ya kushindana na vyombo vya habari. Nina uhakika kwenye kesi ya Mbowe kwa mfano, watu wengine wala wasingejishughulisha kwenda mahakamani kama wangejua wanaweza kukaa waliko na kufuatilia kinachoendelea kupitia matangazo mubashara. Sasa ni nani anayewatungia Mahakama Utaratibu (regulations) za utendaji kazi wao wa kila siku. Ni nani anaweza kuamua kuhusu kutumia video na kamera kurusha matangazo; haiwezekani iwe kesi kwa kesi tu na maamuzi tu ya jaji mmoja mmoja.

Kama tunapata nafasi ya kuwaona viongozi wachovu wa hoja kwenye Bunge na sehemu nyingine nina uhakika tunahaki ya kuwaona pia watu wanaolipwa mishahara kutoka kodi za wananchi kuwa wapelelezi, wachunguzi, waendesha mashtaka - na wengine wakiwa wamesomeshwa na serikali wanajengaje hoja huko Mahakamani na kama hoja zao zina hoja au ni za vihoja.

Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma na uongozi wake wa mhimili wa Mahakama wanahitaji kukaa chini na kuamua mara moja ni nini sera ya matumizi ya kamera mahakamani - hilo moja na pili waamue ni lini na wao wataanzisha channel yao ya kuwapasha habari Watanzania ili Watanzania nao waweze kufuatilia kinachofanywa na mahakama zetu mbalimbali. Vinginevyo, tuache ufyatu wa kuaminishana kuwa mihimili hii mitatu iko sawa.
Mahakama Tanzania iko mfukoni mwa serikali! Ikifanya fyoko itanyimwa fedha za kujiendesha.

Pili kwa kuwa serikali inaendeshwa kichawi kamwe haiwezi kukubali mambo yake yawekwe hadharani! Giza na mchawi ni sawa na inzi na kinyesi!
 
Back
Top Bottom