Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Ni swali ambalo limetokana na yanayoendelea katika sakata la Mbowe. Wabunge wanarushwa mubashara. Tunasikia mawazo yao, malumbano yao, na hata ufyatu wao. Tunasikia wakishangilia na wakizodoa; tunawasikia wakicheka na kuchekana au kuchekeana. Vyombo vya habari vya taifa na vya binafsi vinapewa nafasi ya kuwahabarisha wananchi habari za yanayotokea Bungeni. Wanasema ni "haki ya kuwapa wananchi kupata habari".
Lakini pia tunaona mara kadhaa shughuli zikifanyika Ikulu au mahali ambapo Rais ni mgeni rasmi. Tunahabarishwa nini kinaendelea kwa sababu kuna imani kuwa ni kwa maslahi ya taifa. Hivyo, vyombo vya habari siyo tu vinaruhusiwa lakini Ikulu yenyewe ina "channel" yake ya kuwahabarisha wananchi na unapata video na clips za video huko Youtube kama ukitaka kurejea chochote kilichosemwa au kufanywa. Ni namna nyingine ya ukusanyaji na utunzaji wa rekodi mbalimbali.
Ndio maana swali langu linauliza vipi kuhusu Mahakama. Kama tunaamini katika mfumo wa Mihimili mitatu ni kwanini hadi leo hatujahabarishwa uwepo wa channel ya habari ya mahakama? Je, ni kwanini Mahakama nayo isiweke utaratibu wa shughuli za kesi kurushwa "live" badala ya kushindana na vyombo vya habari. Nina uhakika kwenye kesi ya Mbowe kwa mfano, watu wengine wala wasingejishughulisha kwenda mahakamani kama wangejua wanaweza kukaa waliko na kufuatilia kinachoendelea kupitia matangazo mubashara. Sasa ni nani anayewatungia Mahakama Utaratibu (regulations) za utendaji kazi wao wa kila siku. Ni nani anaweza kuamua kuhusu kutumia video na kamera kurusha matangazo; haiwezekani iwe kesi kwa kesi tu na maamuzi tu ya jaji mmoja mmoja.
Kama tunapata nafasi ya kuwaona viongozi wachovu wa hoja kwenye Bunge na sehemu nyingine nina uhakika tunahaki ya kuwaona pia watu wanaolipwa mishahara kutoka kodi za wananchi kuwa wapelelezi, wachunguzi, waendesha mashtaka - na wengine wakiwa wamesomeshwa na serikali wanajengaje hoja huko Mahakamani na kama hoja zao zina hoja au ni za vihoja.
Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma na uongozi wake wa mhimili wa Mahakama wanahitaji kukaa chini na kuamua mara moja ni nini sera ya matumizi ya kamera mahakamani - hilo moja na pili waamue ni lini na wao wataanzisha channel yao ya kuwapasha habari Watanzania ili Watanzania nao waweze kufuatilia kinachofanywa na mahakama zetu mbalimbali. Vinginevyo, tuache ufyatu wa kuaminishana kuwa mihimili hii mitatu iko sawa.