Swali Fyatu la Jumamosi: Hili Soko la Bilioni 32 litakuwa na Vitu Gani Ndani?

Kuendesha Serikali ya Kijamaa ni mzigo kwa wananchi....

Unadumbukiza bilion 32 kujenga soko k.koo utafikiri kuna huduma zimesimaa kwa kuungua soko hilo...

Serikali imekua ikijenga majengo makubwa yasiyo na tijaa...

Kodi za wananchi hazinufaishi wananchi....

Hatujawahi pata Rais mwenye dhamira ya kuondoa umasikini na kuwapa wananchi dira ya kuondokana na umasikini....
100%
 
Najiuliza pia hivi hili soko likijengwa pembezoni mwa mji hawa watu ambao tunasema ni overpopulated na wapo katikati ya mji watakuwa saved na soko gani?

Au ndio nao wataanza kutoka mjini saa kumi alfajiri kuelekea pembezoni ili waweze kuwahi kununua mahitaji yao na kurudi?

Hivi hakuna uwezekano wa kujenga barabara za juu kupunguza msongamano katikati ya mji na ikawezekana kufika kariakoo kwa muda mchache?

Je kwa jinsi mji wa Dar ulivyokaa ni sehemu ipi ya pembezoni inaweza fikika kirahisi bila foleni kwa mfumo wa barabara tulizonazo?

Je hizo nchi zingine ambazo miji ni over populated wanajenga masoko nje ya mji (pembezoni) au yapo katikati ya miji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na unafiki wako wa kutetea kila kitu hata cha kijinga kwa Magufuli na kuja kuanza kukosoa sasa ..
Naunga mkono ni wazo la kipumbavu..

Binafsi ningependa nione wanajenga masoko mengine pembeni ya mji..
Kama gongo la mboto
Mbezi mwisho
Tegeta
Mbagala n.k...

Soko la kariakoo libaki kama soko la historia...
Tupunguze watu kukusanyana mjini...

Kwangu ishu sio hela ..ishu Mpango mbovu
Upo sahihi soko la kariakoo lijengwe tena kubwa tu lakini pia pawe na masoko ya ku serve maeneo mengine kama Tegeta, Gongo la mboto etc.

Soko la k.koo kwa size ya sasa ni dogo sana na linasababisha msongamano mkubwa sana wa wanunuzi. Kama kinachotembea kwenye media ni kweli kuwa ndio soko jipya la k.koo basi nakubaliana nao kabisa wameona mbali.

Hatuwezi kubaki na k.koo tuliyonayo leo ambayo ilijengwa miaka sijui ya 60 au 70 huko tunahitaji soko kama hili ili kuweza ku serve population ya mjini iliyo ongezeko.

Muundo wa majengo mengi ya k.koo na mji wa Dar kwa ujumla kwa sasa hivi ni wa ghotofa tatu kwenda juu.

Wakati K.koo inajengwa maeneo mengi ya Dar nyumba zilikuwa za bungalow sasa hili ongezeko kubwa la watu linahitaji soko kubwa sana katikati ya mji na wala sio pembezoni ya mji.

Wale wa pembezoni wajengewe masoko ili wasilazimike kuja mjini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu hakiko sawa kwenye maelezo ya waziri wa tamisemi. Amesikika akisema kuwa jengo litakuwa na basement ya ghorofa mbili,...achilia mbali ground level floor na ghorofa nne kwenda juu.

Maelezo haya ya kitalaamu tena ya ubunifu yangepaswa kutolewa na wabunifu wa majengo kwani wao ndio wanaojua changamoto zinazojitokeza kwenye ujenzi wa jengo alilolinadi waziri Ummy Mwalimu pamoja na gharama zake.

Hizi kauli za kisiasa kwenye mambo ya kitaaluma kwa lengo la kuwafurahisha wapiga kura mara zote huongeza gharama maradufu.
 
Ccm inatutesa dola million 14 nisawa na billion 32 zakitanzania hapa watanzania Mana yake kwenye thamani yafedha yetu wanaelewa kweli
 
Stand ya mabasi mbezi pamoja na fidia tumetumia bil. 50 soko la magomeni tumetumia bil.3

Kwa hizi bil 32 za mama tungejenga Kariakoo moja Dar nyingine Mbeya, Arusha, Mwanza na Ruvuma Songea.

Muda si mrefu utasikia mfereji wa milioni 700, karavati ya bil 1 na darasa la milioni 400
 
Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
Mkiambiwa katiba mpya inahitajikika hakuna anaejali ,mnaamini kwenye mtu binafsi baadala ya kuamini kwenye taasisi.Nchi ingekuwa na muongozo wa kila raisi atafuata misingi na mipango aliyoikuta na uajibishwaji kwa kila mmoja atakae fisadi aku kufanya jambo lolote.
 
Nadhani badala ya serikali kutoa fedha hii moja kwa moja watumie mfumo PPP...

Mamlaka za serikali za mitaa nyingi [wilaya, miji, manispaa na majiji] zinatumia mfumo wa PPP kwa ujenzi wa masoko...

Mfano kwa Jiji la DSM, wafanyabiashara wenyewe wanaweza kujenga soko hilo na serikali kazi yake ikawa ni kuandaa designs, mobilization ya resources, kutoa ardhi na mengine ya namna hiyo...

å CHA KWANZA, kinachotakiwa kufanyika ni kupata orodha ya wafanyabiashara wote wanaotaka kuwa wapangaji kwenye jengo litakalojengwa...

å CHA PILI, waandalie mkataba wa upangaji wa aidha miaka 2, 5, au 10...

å CHA TATU, wakokotolee gharama za upangaji na kila mmoja alipe in advance na fedha hiyo itumike kwenye ujenzi soko...

Mathalani kama mkataba ni wa miaka 10, ina maana kila mfanyabiashara atalipa kodi ya miaka hiyo kulingana na thamani ya nyumba/chumba/kizimba anachotaka kuchukua. Kutakuwa na GRADE YA VYUMBA/NYUMBA/VIZIMBA kulingana na aina ya biashara ya mtu MF. banks au financial institutions, hotel, maduka nk nk...

Kwa miaka yote hiyo, yeye ndiye atakuwa mpangaji mmiliki halali wa eneo na kama ataamua kuacha biashara ama amefilisika, atatoa taarifa kwa mbia mwenzake [i.e serikali/jiji la DSM] ili aweze kumpangisha mtu mwingine hadi contract expired time yake na fedha itakuwa yake...

Baada ya mkataba kwisha, 100% serikali kupitia Jiji inakuwa mmiliki wa majengo/jengo na kila mpangaji ataanza kulipa tens kodi ya pango...

Sasa tuashumu serikali inapokea maombi ya wafanyabiashara 20,000 na kila mmoja akaweza kutoa fedha kiasi cha wastani wa TZS 50,000,000 maana yake zitapatikana jumla ya TZS 1,000,000,000,000 [TILIONI MOJA]..!!

Hii maana yake kwa fedha hii wananchi wenyewe wanaweza kujijengea soko la kisasa la aina yake duniani bila serikali kutumia hata senti moja kutoka kwenye fedha za kutoa huduma zingine kwa umma!

å MWISHO, kupitia biashara zitakazokuwa zinaendelea na kufanyika kwenye soko hili, serikali itajipatia kodi za aina mbalimbali kwa kiwango cha kutosha na kutisha sana...

Na kwa kuwa soko litakuwa la kimataifa na kila mfanyabiashara anapenda KARIAKOO, mimi nauhakika kutakuwa na msururu wa malaki ya wafanyabiashara watataka kuwa wabia wa soko hili...!!

Mawazo yangu haya kwa kukukwoti wewe..
Duh! Una akili kama mchwa braza! Sema ukileta akiki zako hizi kwa wale jamaa utakuwa unaleta hujuma kali kwa matumbo yao!
 
Soko la Kariakoo litajengwa upya; inakadiriwa na kudaiwa kuwa serikali itatenga bilioni 32 kulijenga upya. Hili si jambo baya. Ila naomba kuuliza kwa hizo bilioni 32 Watanzania watarajie nini kwenye soko hilo kubwa na maarufu zaidi nchini...

Japo hii bilioni 32 kwenye hela yetu inaweza kuwa ni nyingi lakini kwa dola ni kama dola milioni 14 hivi... lakini je purchasing power ya hiyo bilioni 32 ni sawa na ile ya dola milioni 14? au tunalinganisha mchicha na mapapai?

Ili tutakapokaa chini na kusema "value for money" wote tuchekeane.. vinginevyo naona ugomvi mwingine wa CAG unatengenezwa... Ila angalau liwe na vitu vifuatavyo...

a. Uwanja wa ndege... kupita wa Chato...
b.
Litakuwa na zile bidhaa zote zilizoungua
 
Leo asunuhi nimeijiwa na wazo la ajabu wakati najiandaa kwenda ibadani, hivi tukitangaza kuuza kipande kimoja wapo cha sehemu ya ardhi yetu mfano Kigamboni mzima tukatangaza kuwa inauzwa; mfano dola bilioni 100 tu, na atakayenunua awalipe wenye ardhi pale.

Hivi si ndo utakuwa mwisho wa umaskini na kulipa madeni yote tunayodaiwa?

Sjui niliwaza vizuri!! Yaani kuliko kuendelea na umasikini huu wa kifala bora tuuze viwilaya kama viwili vitatu kwa anayetaka,kisha hela ile tumalize changamoto zote watu tuishi maisha mazuri kuliko maisha haya ya kuvaa barakoa kinafiki ili tupewe katilioni kamoja nukta tatu kakutudhalilisha.
 
Soko la Kariakoo litajengwa upya; inakadiriwa na kudaiwa kuwa serikali itatenga bilioni 32 kulijenga upya. Hili si jambo baya. Ila naomba kuuliza kwa hizo bilioni 32 Watanzania watarajie nini kwenye soko hilo kubwa na maarufu zaidi nchini...

Japo hii bilioni 32 kwenye hela yetu inaweza kuwa ni nyingi lakini kwa dola ni kama dola milioni 14 hivi... lakini je purchasing power ya hiyo bilioni 32 ni sawa na ile ya dola milioni 14? au tunalinganisha mchicha na mapapai?

Ili tutakapokaa chini na kusema "value for money" wote tuchekeane.. vinginevyo naona ugomvi mwingine wa CAG unatengenezwa... Ila angalau liwe na vitu vifuatavyo...

a. Uwanja wa ndege... kupita wa Chato...
b.
Ungehoji Kwanza na ule uwanja wa ndege chato wa billion 40 una faida gani kwenu wasukuma
 
Nani ame undermine Kariakoo?
Yaani wewe unaona sawa kabisa kila siku watu watoke nje ya viunga vya jiji la Dar ili kuja kuuza na kununua hapo Kariakoo?

Toka miaka ya 1970 (zaidi ya miaka 50) watu wamekuja kuuza au kununua Kariakoo (hivyo Kariakoo ni soko la kihistoria hapa Tz) lakini sio eneo la kutoshea au kulazimisha liwe pekee kufanyia biashara hapa Dar kwa sasa, jiji limekuwa na kupanuka, kwanini huduma za kijamii kama soko zisizogezwe huko huko alipo?
Ndugu Zanzibar-ASP:

Kwani kuna mtu amesema ikijengwa Kariakoo kunazuiwa kujengwa masoko mengine pembezoni mwa miji kulingana na uhitaji wa watu..?

Mimi nadhani tunaongelea soko la Kariakoo kama soko mama na kubwa la yote na kama soko la kimataifa
 
Nadhani badala ya serikali kutoa fedha hii moja kwa moja watumie mfumo PPP...

Mamlaka za serikali za mitaa nyingi [wilaya, miji, manispaa na majiji] zinatumia mfumo wa PPP kwa ujenzi wa masoko...

Mfano kwa Jiji la DSM, wafanyabiashara wenyewe wanaweza kujenga soko hilo na serikali kazi yake ikawa ni kuandaa designs, mobilization ya resources, kutoa ardhi na mengine ya namna hiyo...

å CHA KWANZA, kinachotakiwa kufanyika ni kupata orodha ya wafanyabiashara wote wanaotaka kuwa wapangaji kwenye jengo litakalojengwa...

å CHA PILI, waandalie mkataba wa upangaji wa aidha miaka 2, 5, au 10...

å CHA TATU, wakokotolee gharama za upangaji na kila mmoja alipe in advance na fedha hiyo itumike kwenye ujenzi soko...

Mathalani kama mkataba ni wa miaka 10, ina maana kila mfanyabiashara atalipa kodi ya miaka hiyo kulingana na thamani ya nyumba/chumba/kizimba anachotaka kuchukua. Kutakuwa na GRADE YA VYUMBA/NYUMBA/VIZIMBA kulingana na aina ya biashara ya mtu MF. banks au financial institutions, hotel, maduka nk nk...

Kwa miaka yote hiyo, yeye ndiye atakuwa mpangaji mmiliki halali wa eneo na kama ataamua kuacha biashara ama amefilisika, atatoa taarifa kwa mbia mwenzake [i.e serikali/jiji la DSM] ili aweze kumpangisha mtu mwingine hadi contract expired time yake na fedha itakuwa yake...

Baada ya mkataba kwisha, 100% serikali kupitia Jiji inakuwa mmiliki wa majengo/jengo na kila mpangaji ataanza kulipa tens kodi ya pango...

Sasa tuashumu serikali inapokea maombi ya wafanyabiashara 20,000 na kila mmoja akaweza kutoa fedha kiasi cha wastani wa TZS 50,000,000 maana yake zitapatikana jumla ya TZS 1,000,000,000,000 [TILIONI MOJA]..!!

Hii maana yake kwa fedha hii wananchi wenyewe wanaweza kujijengea soko la kisasa la aina yake duniani bila serikali kutumia hata senti moja kutoka kwenye fedha za kutoa huduma zingine kwa umma!

å MWISHO, kupitia biashara zitakazokuwa zinaendelea na kufanyika kwenye soko hili, serikali itajipatia kodi za aina mbalimbali kwa kiwango cha kutosha na kutisha sana...

Na kwa kuwa soko litakuwa la kimataifa na kila mfanyabiashara anapenda KARIAKOO, mimi nauhakika kutakuwa na msururu wa malaki ya wafanyabiashara watataka kuwa wabia wa soko hili...!!

Mawazo yangu haya kwa kukukwoti wewe..
Una akili nyingi sana
 
Back
Top Bottom