Swali Fikirishi: Nini mwelekeo wa waliohama vyama kwa misingi ya kuunga mkono juhudi?

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Wakati Chama cha Mapinduzi kikiendelea na michakato ya kupanga safu za uongozi kufuatia kuondoka kwa Mwenyekiti Hayati John Pombe Magufuli, nini hatima ya wanachacshama waliohamia chama hicho kwa misingi ya kuunga juhudi za rais?

Najaribu kuwaza kwa sauti:

1. Ukizingatia kwamba juhudi zilizokuwa zinavutia ni za mtu binafsi na sasa hayupo, kuna kila uwezekano wa chama kushikailiwa ama moja kwa moja ama kwa mlango wa uani na waasisi ama vinara wa mfumo fisadi ambao kama ndivyo maumivu ya Taifa hasa wanyonge hayatakuwa na kipimo wala mfariji. Kwa mantiki hii je hawa wanachama waliokwenda kuunga mkono wataendelea kubaki ndani ya chama cha CCM?

2. Rais watu wa awamu ya tano A. alipitia wakati mgumu wa kutumbua tumbua na kuwaamini Watanzania waliohamia toka vyama pinzani na ambao hawajamuangusha. Na kwa usahihi wamekuwa wakifanya kazi katika kasi na taswira halisi ya Rais wetu. Hii ni dhahiri kwamba ndani ya chama kulikuwa na ukakasi na uhaba wa watu sahihi wenye nia na uwezo wa kutembea katika maono ya Rais wetu. Ikiwa sasa aliyekuwa anafagia fagia kaondoka, ni dhahiri kwamba CCM inarudi kwenye uhalisia wake. Chini ya viongozi halisia wa CCM Fisadi, hao waliokwenda kuunga mkono juhudi, wataaminika na hatimaye kukubalika hata kupewa nyadhifa sahihi ambazo ki uhalisia wameonyesha kuzimudu na kuzitendea haki?

3. Kwa kuzingatia haya juu, wataamua kubaki wakisubiri siku ya kwenda kwa Mungu ama watafight kubadilisha hicho chama ambacho kinawaita wageni? Lakini nini mtazamo wa vyama pinzani kama wakiamua kurejea ili waunganishe nguvu na kuimarisha vyamacha? Kama vyama vyao vya mwazo vitawaktaa kwa kutokuwa na imani nao, wakiamua kuanzisha chama chaoma cha siasa, waweza kusababisha mabadiliko katika taifa waliyayalilia katika hali ya kutokuaminika na chama tawala na vyama vya upinzani?

4. Hapa tunajifunza nini?
Naomba tujadili ama kuwapa ushauri mfupi nini wafanye.
 
Tunajifunza tusifuate mtu bali itikadi na mfumo wa taasisi.

Chakuwashauri watulie wakipata viinua mgongo vyao wakaanze ujasiriamali maana hawataaminika ccm au vyama m adala.

1. Ninaona pia kuna somo la kupima gharama na faida za muda mfupi na muda mrefu kabla ya kufanya maamuzi.
Wale waliokuwa na malengo ya muda mfupi, yawezekana wameyafikia na hawatakuwa na majuto.

2. Lakini pia kuna methali inasema usitukane wakunga na uzazi bado ungalipo. Hii inamaana watu wajifunze kutumia uhuru wa kubadilisha mahusiano bila vurugu zisizo sababu kwa kuwa katika maisha watu hukutana ama kuhitajiana kwa nyakati na namna mbalimbali.
 
Wengi wao walikua CCM apo awali,wamefanya"kurudi nyumbani kumenoga"
Na bado kuna ambao watarudi nyumbani siku za usoni.
Walijibaini wapinga ufisadi. Baada ya Mheshimiwa Hayati kuonyesha kwamba ana itikadi ya kupinga ufisadi wa aina zote kama wao wakaamua kwenda kuunganisha nguvu. Sasa mpinga ufisadi kaondoka, watabaki kule wakiunga mkono? Na wazawa, watawakubali?
 
Hawa jamaa kama wana macho ya kuona mbali, ni bora kuanzia sasa wakaanzisha mchakato wa kusajili chama chao kipya cha kisiasa ambacho hakita fungamana na ccm au chadema, au wakatafuta chama chochote kile ambacho hakina jina, wakakijenga ili waendelee na siasa!

Wasipofanya hivyo, basi wayatumie vizuri mafao yao na mishahara yao kuanzia sasa. Kiufupi tu ni kwamba, aliyewapa jeuri ya kupumua na kuvuta hewa safi kule Lumumba, hayupo tena! Na itakapofika 2025, chama kitakuwa tayari mikononi mwa wenyewe! Hivyo hawana budi kujiongeza mapema.

Hii ni mpaka kwa akina Julius Mtatiro and Co. Ltd.
 
Wakati Chama cha Mapinduzi kikiendelea na michakato ya kupanga safu za uongozi kufuatia kuondoka kwa Mwenyekiti Hayati John Pombe Magufuli, nini hatima ya wanachacshama waliohamia chama hicho kwa misingi ya kuunga juhudi za rais?

Najaribu kuwaza kwa sauti:
1. Ukizingatia kwamba juhudi zilizokuwa zinavutia ni za mtu binafsi na sasa hayupo, kuna kila uwezekano wa chama kushikailiwa ama moja kwa moja ama kwa mlango wa uani na waasisi ama vinara wa mfumo fisadi ambao kama ndivyo maumivu ya Taifa hasa wanyonge hayatakuwa na kipimo wala mfariji. Kwa mantiki hii je hawa wanachama waliokwenda kuunga mkono wataendelea kubaki ndani ya chama cha CCM?

2. Rais watu wa awamu ya tano A. alipitia wakati mgumu wa kutumbua tumbua na kuwaamini Watanzania waliohamia toka vyama pinzani na ambao hawajamuangusha. Na kwa usahihi wamekuwa wakifanya kazi katika kasi na taswira halisi ya Rais wetu. Hii ni dhahiri kwamba ndani ya chama kulikuwa na ukakasi na uhaba wa watu sahihi wenye nia na uwezo wa kutembea katika maono ya Rais wetu. Ikiwa sasa aliyekuwa anafagia fagia kaondoka, ni dhahiri kwamba CCM inarudi kwenye uhalisia wake. Chini ya viongozi halisia wa CCM Fisadi, hao waliokwenda kuunga mkono juhudi, wataaminika na hatimaye kukubalika hata kupewa nyadhifa sahihi ambazo ki uhalisia wameonyesha kuzimudu na kuzitendea haki?

3. Kwa kuzingatia haya juu, wataamua kubaki wakisubiri siku ya kwenda kwa Mungu ama watafight kubadilisha hicho chama ambacho kinawaita wageni? Lakini nini mtazamo wa vyama pinzani kama wakiamua kurejea ili waunganishe nguvu na kuimarisha vyamacha? Kama vyama vyao vya mwazo vitawaktaa kwa kutokuwa na imani nao, wakiamua kuanzisha chama chaoma cha siasa, waweza kusababisha mabadiliko katika taifa waliyayalilia katika hali ya kutokuaminika na chama tawala na vyama vya upinzani?

4. Hapa tunajifunza nini?
Naomba tujadili ama kuwapa ushauri mfupi nini wafanye.
kosa kubwa sana alifanya hapa aliungana na adui bila kujua.
Wamemmaliza kirahisi sana.

Alikumbatia adui akatupa waumini wake kirahisi sababu ya udwanzi akiamini yuko sahihi.
 
Hebu fafanua kidogo ili tupate picha ya wazi ya hao adui.
 
Daaa!!! Mkuu umepewa au umekaribishwa chakula km mgeni unataka ukakombe mpaka sufuria??

Mwalimu anaonyeshaga njia tu!! Mengine ni kazi ya denti...ajiongeze!!!

Mkuu Umesomea wapi kwani!!! Na lini..
 
Back
Top Bottom