Swali fikirishi kidogo: Hivi kwanini baada ya TANU na ASP kuungana waliamua kujiita Chama Cha Mapinduzi ?

Mbali na mapinduzi ya zanzibar Tanu imeshiriki sana kwenye ukombozi wa nchi nyingi kusin mwa jangwa la sahara japo sio kwa mapinduzi lakin kuna mageuz mengi ya kimifumo waliyaleta nchi mbali mbali.nadhan hawakutaka dhana hii ipotee hivyo wakaibeba kifikra kwenye muundo wa chama kipya.

Pia si unajua ccm niwazee wa kupindua meza kwenye chaguzi.Asbuh wapinzani wanaongoza kwa kura jioni wamesha achwa mbali sana..ahahah..just a joke
 
Shule ya msingi kulikuwa na swali, mapinduzi ni nini?, jibu lilikuwa ni mabadiliko ya hali ya binadamu kutoka hali duni kwenda bora. kama vile industrial revolution. Walifanya bidii sana kutuaminisha hili. japo naona walikuwa wanacheza na maneno kuficha maana halisi, Pengine alikuwa anataka kuanzisha cultural revolution kama ya wachina iliyotoka kuisha punde(1976)!? Ni swali muhimu umeuliza?
 
Chama Cha Mapinduzi kilipozaliwa sherehe ziliendelea kwa siku saba. Vijana wa Chipukizi, ngonjera, kwaya na maigizo wakila wali na pofu mchana.

Mabanda yaliwekwa vivutio, kulikua mpaka na simba waliketwa na Idara ya Wanyama Pori, bidhaa mbali mbali ziliuzwa uwanjani kuanzia vitenge na khanga za Urafiki
 
Back
Top Bottom