Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Baada ya kustaafu/kung'atuka...
Je Mwalimu kweli angekaa kimya kwa yanayotokea leo kama walivyo kimya Marais waliomfuata kwa mambo kama haya?
- Mwalimu hakukaa kimya Azimio la Arusha lilipochinjwa na kuzikwa huko Zanzibar na kupitishwa kwa azimio jipya lililojulikana kama Azimio la Zanzibar chini ya Rais Mwinyi.
- Baba wa Taifa hakukaa kimya CCM ilipoamua kupiga vita upepo wa mageuzi ya kisiasa uliotishia mfumo wa chama kimoja na kuruhusu mfumo wa vyama vingi.
- Mwalimu hakukaa kimya mapendekezo ya kumuongezea Rais Mwinyi awamu ya tatu yalipotolewa na baadhi ya viongozi wa CCM kwa kuogopa ujio wa vyama vingi.
- Mwalimu hakukaa kimya wabunge wa CCM walipopitisha mswada wa serikali tatu wakiungwa mkono na Waziri Mkuu J. Malecela akidai hiyo si sera ya CCM.
- Mwalimu hakukaa kimya alipoona serikali ya awamu ya pili ikianza kuwakumbatia wafanya biashara kiasi cha nchi kushindwa kukusanya kodi na serikali kukosa mapato.
- Mwalimu hakukaa kimya alipoona Kamati Kuu ya CCM ikipendekeza majina ya watu wawili alioamini hawakuwa na sifa za kugombea Urais mwaka 1995...Lowassa na Kikwete.
- Mwalimu hakukaa kimya Mkapa baada ya kuchaguliwa kuwa Rais katika awamu ya tatu kuamua kuuza hovyo mashirika ya UMMA ikiwa ni pamoja na Benki ya taifa na alitumia majukwaa kukemea maamuzi hayo.
Je Mwalimu kweli angekaa kimya kwa yanayotokea leo kama walivyo kimya Marais waliomfuata kwa mambo kama haya?
- Katiba kusiginwa
- Kuuzwa kwa nyumba za serikali
- Bunge kutokuwa na meno
- Mahakama kuingiliwa
- Kuteka, kuteswa na kuuawa kwa raia
- Demokrasia kutiwa kufuli
- Matumizi ya hoja za nguvu
- Ubaguzi na uhasama wa kisiasa
- MaDC na MaRC kuwasweka ndani wawakilishi wa wananchi
- Sheria ya manunuzi kutofuatwa
- Ufisadi uliotamalaki.