Swali fikirishi...kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, angekuwepo leo, je naye angekaa kimya kama Mwinyi, Mkapa na Kikwete?

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,682
2,000
Baada ya kustaafu/kung'atuka...
 • Mwalimu hakukaa kimya Azimio la Arusha lilipochinjwa na kuzikwa huko Zanzibar na kupitishwa kwa azimio jipya lililojulikana kama Azimio la Zanzibar chini ya Rais Mwinyi.
 • Baba wa Taifa hakukaa kimya CCM ilipoamua kupiga vita upepo wa mageuzi ya kisiasa uliotishia mfumo wa chama kimoja na kuruhusu mfumo wa vyama vingi.
 • Mwalimu hakukaa kimya mapendekezo ya kumuongezea Rais Mwinyi awamu ya tatu yalipotolewa na baadhi ya viongozi wa CCM kwa kuogopa ujio wa vyama vingi.
 • Mwalimu hakukaa kimya wabunge wa CCM walipopitisha mswada wa serikali tatu wakiungwa mkono na Waziri Mkuu J. Malecela akidai hiyo si sera ya CCM.
 • Mwalimu hakukaa kimya alipoona serikali ya awamu ya pili ikianza kuwakumbatia wafanya biashara kiasi cha nchi kushindwa kukusanya kodi na serikali kukosa mapato.
 • Mwalimu hakukaa kimya alipoona Kamati Kuu ya CCM ikipendekeza majina ya watu wawili alioamini hawakuwa na sifa za kugombea Urais mwaka 1995...Lowassa na Kikwete.
 • Mwalimu hakukaa kimya Mkapa baada ya kuchaguliwa kuwa Rais katika awamu ya tatu kuamua kuuza hovyo mashirika ya UMMA ikiwa ni pamoja na Benki ya taifa na alitumia majukwaa kukemea maamuzi hayo.
Hata hivyo mwaka 1998, sauti ya Mwalimu ilipozimika wengine wetu tumekuta tukijiuliza maswali kadhaa...
Je Mwalimu kweli angekaa kimya kwa yanayotokea leo kama walivyo kimya Marais waliomfuata kwa mambo kama haya?
 • Katiba kusiginwa
 • Kuuzwa kwa nyumba za serikali
 • Bunge kutokuwa na meno
 • Mahakama kuingiliwa
 • Kuteka, kuteswa na kuuawa kwa raia
 • Demokrasia kutiwa kufuli
 • Matumizi ya hoja za nguvu
 • Ubaguzi na uhasama wa kisiasa
 • MaDC na MaRC kuwasweka ndani wawakilishi wa wananchi
 • Sheria ya manunuzi kutofuatwa
 • Ufisadi uliotamalaki.
Je ukimya wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete unasababishwa na nini? Karibuni jukwaani tujadili...
 
Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,290
2,000
Ifikie hatua watu muwe waelewa....kila kitu na zama zake..kwa kpindi kile mwalimu alikuwa kiongozi bora kwa wakat wake..kwa wakat huu sidhan kama angefit hata mawazo yake sidhan kama angekuwa na ushawishi sana... kwenye zama hzi za teknolojia na elimu ya juu huwezi kuwa na ushawishi wa kibabe...hoja ya mwalimu iliathiriwa na mfumo wa ujamaa....bado ushawishi wake na mawazo yake yalikuwa na kiujamaa tu na ndo mana kwa sasa asingeweza lolote..mwacheni apumzike huyo mzee....istoshe Tanzania hatuna mfumo wa kuwapa nguvu maraisi wastaafu dhidi ya maamuz ya Raisi...yan hao ni kama raia tu sa hv hata maisha yao yanategemea mbeleko za Raisi..Still Kwa mfumo wa Tz Raisi ni final say
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,682
2,000
istoshe Tanzania hatuna mfumo wa kuwapa nguvu maraisi wastaafu dhidi ya maamuz ya Raisi.
Hawazuiwi kutoa ushauri wala kukosoa, hizo ni haki za msingi za raia wa nchi hii.
yan hao ni kama raia tu sa hv hata maisha yao yanategemea mbeleko za Raisi..Still Kwa mfumo wa Tz Raisi ni final say
Sikujua kama maisha yao yanategemea mbeleko za Raisi, nilidhani ni matakwa ya Katiba. Ama unataka kuniambia kuna mtu yuko juu ya Katiba? Of course Rais ndiye ana final say lakini Katiba haitukatazi kumkosoa au kumshauri na si lazima afuate ushauri huo ila lazima atende kulingana na Katiba.
 
Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,290
2,000
Hawazuiwi kutoa ushauri wala kukosoa, hizo ni haki za msingi za raia wa nchi hii.
Sikujua kama maisha yao yanategemea mbeleko za Raisi, nilidhani ni matakwa ya Katiba. Ama unataka kuniambia kuna mtu yuko juu ya Katiba? Of course Rais ndiye ana final say lakini Katiba haitukatazi kumkosoa au kumshauri na si lazima afuate ushauri huo ila lazima atende kulingana na Katiba.
Ni kweli katiba ndo kila kitu...hata hivo katiba imepwaya sana kusimamia mamlaka yake..Kwa Africa na Tanzania Raisi ana nguvu kuliko katiba...na maamuzi yake huathiri mstakabali wa Taifa na wala sio katiba...ili katiba isimame vyema inategemezwa na mihimili miwili ambayo ni Mahakama na Bunge...shida inakuja Mahakama na Bunge viongozi wake wakuu ni wateule wa Raisi...kwa vyovyote vile Watatekeleza anayosema Raisi na sio Katiba inasemaje......na kwa hiyo Raisi hayupo juu ya katiba ila ana nguvu kuliko katiba
 
MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,535
2,000
IMG-20170117-WA0003.jpg
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
2,414
2,000
Baada ya kustaafu/kung'atuka...
 • Mwalimu hakukaa kimya Azimio la Arusha lilipochinjwa na kuzikwa huko Zanzibar na kupitishwa kwa azimio jipya lililojulikana kama Azimio la Zanzibar chini ya Rais Mwinyi.
 • Baba wa Taifa hakukaa kimya CCM ilipoamua kupiga vita upepo wa mageuzi ya kisiasa uliotishia mfumo wa chama kimoja na kuruhusu mfumo wa vyama vingi.
 • Mwalimu hakukaa kimya mapendekezo ya kumuongezea Rais Mwinyi awamu ya tatu yalipotolewa na baadhi ya viongozi wa CCM kwa kuogopa ujio wa vyama vingi.
 • Mwalimu hakukaa kimya wabunge wa CCM walipopitisha mswada wa serikali tatu wakiungwa mkono na Waziri Mkuu J. Malecela akidai hiyo si sera ya CCM.
 • Mwalimu hakukaa kimya alipoona serikali ya awamu ya pili ikianza kuwakumbatia wafanya biashara kiasi cha nchi kushindwa kukusanya kodi na serikali kukosa mapato.
 • Mwalimu hakukaa kimya alipoona Kamati Kuu ya CCM ikipendekeza majina ya watu wawili alioamini hawakuwa na sifa za kugombea Urais mwaka 1995...Lowassa na Kikwete.
 • Mwalimu hakukaa kimya Mkapa baada ya kuchaguliwa kuwa Rais katika awamu ya tatu kuamua kuuza hovyo mashirika ya UMMA ikiwa ni pamoja na Benki ya taifa na alitumia majukwaa kukemea maamuzi hayo.
Hata hivyo mwaka 1998, sauti ya Mwalimu ilipozimika wengine wetu tumekuta tukijiuliza maswali kadhaa...
Je Mwalimu kweli angekaa kimya kwa yanayotokea leo kama walivyo kimya Marais waliomfuata kwa mambo kama haya?
 • Katiba kusiginwa
 • Kuuzwa kwa nyumba za serikali
 • Bunge kutokuwa na meno
 • Mahakama kuingiliwa
 • Kuteka, kuteswa na kuuawa kwa raia
 • Demokrasia kutiwa kufuli
 • Matumizi ya hoja za nguvu
 • Ubaguzi na uhasama wa kisiasa
 • MaDC na MaRC kuwasweka ndani wawakilishi wa wananchi
 • Sheria ya manunuzi kutofuatwa
 • Ufisadi uliotamalaki.
Je ukimya wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete unasababishwa na nini? Karibuni jukwaani tujadili...
Sikuwahi kumuona Nyerere akiongoza Taifa lakini kadri ninavyo msoma namuona Nyerere aliyekuwa so Hash zaidi ya Magufuli..! Huyo Nyerere na Magufuli sipaoni pa kuwatofautisha.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,698

Mada nzuri sana hii. Tuelewa kuwa mtu yeyote mwenye ada ya uongozi huwa ana silka ya kutoa dira ya jamii. Anaweza kutoa dira hiyo akiwa na mamlaka au bila kuwa na mamlaka. Mtu anayeamaini kuwa kuwa akiwa kiongozi atafanya mambo yaliyoko akilini mwake kabla ya kueleza dira yara yake ya jamii ikoje, mara zote akishaindoka madarakani hukaa kimya kwa sababu hakuwa na dira ya kijamii, uongozi wake ulitegemea zaidi mamlaka. Nyerere alikuwa na dira, lakini hao wote liowataja hawakuwa na dira, bali walikuwa na ndoto za kuongoza nchi tu.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
106,934
2,000
Mkuu Mag3 Baba wa Taifa hakuwa mnafiki kama hawa wastaafu wengine na hakuwa fisadi wala mwizi kama haya majizi hivyo angemsemea hovyo tu huyu dhalimu na dikteta aliyevuruga kila kitu ikiwemo amani na mshikamano wetu ambavyo Mwalimu alivijenga kwa miaka chungu nzima. Msikilize hapa utadhani aliona maovu ya huyu kichaa.

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
8,105
2,000
lakini kadri ninavyo msoma namuona Nyerere aliyekuwa so Hash zaidi ya Magufuli..! Huyo Nyerere na Magufuli sipaoni pa kuwatofautisha.
Sijui unamsoma wapi mkuu!. Tupatie 'reference' nasi tuyasome hayo uliyoyasoma ili tuyaone na kuyapima.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
8,105
2,000
Mada nzuri sana hii. Tuelewa kuwa mtu yeyote mwenye ada ya uongozi huwa ana silka ya kutoa dira ya jamii. Anaweza kutoa dira hiyo akiwa na mamlaka au bila kuwa na mamlaka. Mtu anayeamaini kuwa kuwa akiwa kiongozi atafanya mambo yaliyoko akilini mwake kabla ya kueleza dira yara yake ya jamii ikoje, mara zote akishaindoka madarakani hukaa kimya kwa sababu hakuwa na dira ya kijamii, uongozi wake ulitegemea zaidi mamlaka. Nyerere alikuwa na dira, lakini hao wote liowataja hawakuwa na dira, bali walikuwa na ndoto za kuongoza nchi tu.

Hii ndio tofauti kubwa sana wengi wetu tusiyoweza kuibainisha katika viongozi wetu.

Tuchukulie kwa mfano, 'Ujenzi wa Vijiji vya Ujamaa'. Na huu utakuwa ni mfano mmoja tu katika mingi.

Bila ya kutilia maanani matokeo yake yalivyokuwat, na matatizo kadhaa yaliyojitokeza sehemu mbalimbali katika utekelezaji wake; jambo hilo lilikuwa na lengo, na mijadala na maandalizi yalifanyika kulitekeleza. Sababu za kufanya hivyo zilelezwa kwa wananchi kwa upana wake na utekelezaji ukafanyika.
Kabla ya utekelezaji huo maandalizi yalifanyika nchi nzima.

Leo hii kampeni kama hiyo ingetangazwa, sijui utekelezaji wake ungekuwa vipi. Huenda hata kampeni ya ununuzi wa korosho ingekuwa ni bora zaidi!

Uzito wa mawazo uliyoyaweka hapo juu, mkuu 'Kichuguu,' ni nadra sana kuyaona siku hizi.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
8,105
2,000
Je ukimya wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete unasababishwa na nini?
Nikijaribu kukumbuka vyema, CCM ya "Huyu ni Mwenzetu" ilianza wakati wa Mwinyi.
Hawa wote uliowataja hapo juu ni kundi la "wenzetu". Mtu kama ni mwenzako, unamsitiri, hata na siri zenu mnazisitiri.
Unapoona akina Lowassa wanarudi nyumbani, ujue hiyo ni ishara mhimu sana.

Kwa hiyo, katika hao uliowataja hapo juu, hakuna anayeweza kusema kama alivyosema Mwalimu.
Hofu yangu tu ni kwamba, kama angekuwepo wakati huu, asingenyamaza, angesema, na kusema huko huenda kungemwingiza matatani hata usiyoweza kuyafikiria. Hili tuliachie hapo.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,995
2,000
Waache wakae Kimya mana nchi ni ya kwao na aliyepo ni wa kwao na chama ni cha kwao.
Mfumo wa kijamaa kina kundi la wateule wachache waliochukua nafasi ya Wakoloni. Wanatumia sheria na namba ile ile ya mkoloni kutawala kwa hiyo hakuna sababu ya kukosoana. Watawala wote Afrika wameingia kwenye siasa kwa sababu ya kutamani maisha ya kifahari kama wakoloni.
Ndio maana hawataki kuhisi kuwa wanadharauliwa. Wanapenda ukubwa na heshima.
Nyerere alitokea kwenye uana harakati mpaka urais tofauti na hao wengine waliotokea kwenye kuungana mkono ,kushangilia kila kinachofanywa na serikali na kutukuza kila kinachofanywa na serikali ili wapate vyeo na madaraka na maslahi manoni.
Nyerere alikua mkosiaji na mpingaji wa serikali ya kikoloni iliyokua inatawala kibabe.
Aliingia madarakani akiwa hivyo na alitawala akiwa hivyo na akastaafu akiwa hivyo.

Hao wengine walipewa madaraka kwa ajili ya kulindana hivyo hawana chembe ya uanaharakati zaidi ya kulinda maslahi ya Chama na madaraka yao. Hao kama watahisi kuwa kugeuza ardhi ya eneo Fulani juuchini na kutumia watu wote ardhini kuwa itawezesha chama chao kibaki madarakani na madaraka yao yabaki hakika hawatasita kufanya hivyo.

Kwa sasa ni Tundu Lisu peke yake anayeweza kuingia madarakani na kuishi kama Nyerere hata atakapo staafu na akakosoa panapostahili kukosolewa.

Wengine wote ni vigumu sana kutumikia mali na Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000
Baada ya kustaafu/kung'atuka...
Hata hivyo mwaka 1998, sauti ya Mwalimu ilipozimika wengine wetu tumekuta tukijiuliza maswali kadhaa...
Je Mwalimu kweli angekaa kimya kwa yanayotokea leo kama walivyo kimya Marais waliomfuata kwa mambo kama haya?
Je ukimya wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete unasababishwa na nini? Karibuni jukwaani tujadili...
Mkuu Mag3, kila zama na zama zake, hata Mwalimu angekuwepo kwa zama hizi, angekaa kimya!

Kuna watu wa aina mbili, Wakimya na Waongeaji, Mwalimu alikuwa ni muongeaji, Mwinyi ni mkimya, naomba usimuingize humu.
Na kwenye ukimya pia kuna ukimya wa aina mbili, 1. Unaona na kuamua kunyamazi. 2. Ukimya unakua huoni hivyo huna cha kuongea.
Lets asume Mkapa na JK, kwa haya yanayotokea, wako kimya kwa sababu hawaoni, kufuatia zama hizi tulizomo. Siku wakiona na wao wataibuka kama Nyerere alivyokuwa anaibuka.

NB. I was privileged kuwepo ni person pale Msasani kwenye "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania", na kuwepo pale Kilimajaro Hotel kwenye hotuba ya "Nyufa"

P.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
8,105
2,000
Ifikie hatua watu muwe waelewa....kila kitu na zama zake..kwa kpindi kile mwalimu alikuwa kiongozi bora kwa wakat wake..kwa wakat huu sidhan kama angefit hata mawazo yake sidhan kama angekuwa na ushawishi sana... kwenye zama hzi za teknolojia na elimu ya juu huwezi kuwa na ushawishi wa kibabe...hoja ya mwalimu iliathiriwa na mfumo wa ujamaa....bado ushawishi wake na mawazo yake yalikuwa na kiujamaa tu na ndo mana kwa sasa asingeweza lolote..mwacheni apumzike huyo mzee....istoshe Tanzania hatuna mfumo wa kuwapa nguvu maraisi wastaafu dhidi ya maamuz ya Raisi...yan hao ni kama raia tu sa hv hata maisha yao yanategemea mbeleko za Raisi..Still Kwa mfumo wa Tz Raisi ni final say
Umejipigia pigia tu mradi liende; maanake hakuna hata moja ulilolieleza kuonyesha unalo uelewa nalo!

Mara 'teknologia na elimu ya juu'; mara 'ujamaa' na ukiambiwa ueleze kuhusu jinsi ujamaa ulivyoathiri, sidhani kuwa unao uwezo huo, pamoja na kujigamba na 'teknologia' na 'elimu ya juu'!
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
8,105
2,000
Mkuu Mag3, kila zama na zama zake, hata Mwalimu angekuwepo kwa zama hizi, angekaa kimya!

Well, have to respond to this, can't resist the urge.

?? Ninaweza kusema kwa asili mia 100 kuwa HAPANA asingekaa kimya!!

Angewekwa ndan au zaidii? Inawezekana; lakini asingekaa kimya!

A principled person cannot keep quiet when he encounters what he does not believe in. Mwalimu stood for principles.
 
charles mususa

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
287
250
Ifikie hatua watu muwe waelewa....kila kitu na zama zake..kwa kpindi kile mwalimu alikuwa kiongozi bora kwa wakat wake..kwa wakat huu sidhan kama angefit hata mawazo yake sidhan kama angekuwa na ushawishi sana... kwenye zama hzi za teknolojia na elimu ya juu huwezi kuwa na ushawishi wa kibabe...hoja ya mwalimu iliathiriwa na mfumo wa ujamaa....bado ushawishi wake na mawazo yake yalikuwa na kiujamaa tu na ndo mana kwa sasa asingeweza lolote..mwacheni apumzike huyo mzee....istoshe Tanzania hatuna mfumo wa kuwapa nguvu maraisi wastaafu dhidi ya maamuz ya Raisi...yan hao ni kama raia tu sa hv hata maisha yao yanategemea mbeleko za Raisi..Still Kwa mfumo wa Tz Raisi ni final say
Ukapimwe akili Kwanza technologia na ideologia wapi na wapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom