Swali fikirishi: Je, dini zimezidiwa kasi na maarifa mbele ya utandawazi na teknolojia?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,987
49,651
Habari wadau

Ukiangalia kwa makini kiwango cha maovu na vitendo vya uvunjifu wa maadili vinazidi kuongezeka licha ya uwepo wa dini na madhehebu kila kona.

Ushoga, kusagana, sijui biriani, wanaume kama mabinti na ubinafsi ni baadhi tu huku dini nazo zikichanja mbuga majengo makubwa ya makanisa na misikiti inapamba miji, manabii, wasoma dua na kisomo n.k. wametapakaa kila kona lakini hatuoni impacts yao kupunguza uovu nchini. Je, watu wa dini wabadili mbinu za medani ili kukabiliana na utandawazi wenye nguvu ya teknolojia?

Karibu kwa maoni ya nini kifanyike ili kujenga jamii bora yenye hofu ya Mungu
 
Imeandikwa, Dunia ya sasa na Ulimwengu huu Imewekwa akiba kwa moto, hutakuja kuona tena Mungu akiiangamiza dunia kwa kuzidi maovu.
 
Imewekwa akiba kwa moto hapo hapo unasema hutakuja kuona tena Mungu akiiangamiza dunia mbona unaji contradict?
 
Lakini vipi mahubiri na mihadhara ya dini zenyewe ina tija au? Bila kujalisha zimejengwa wapi
Mahubiri gani?

Katika kila hubiri zuri unaloweza kulipata katika dini, naweza kukuonesha mstari mwingine au tafsiri nyingine inayoweza kuchochea baya.

Kwenye Biblia hapa utaambiwa jicho kwa jicho na jino kwa jino, pale utaambiwa atakayekupiga shavu moja, mpe akupige na la pili.

Kwenye Quran hapa utaambiwa dini halilazimishwi, pale utaambiwa atakayekataa kusilimu mfukuze bila neema.

Dini haina mahubiri yaliyo consistent.

Na haina mahubiri consistent kwa sababu imetungwa na watu tu waliojaribu kukabili mazingira yao ya wakati huo.

Sasa mazingira yanavyobadilika, na mahubiri yanabadilika.
 
Mahubiri gani?

Katika kila hubiri zuri unaloweza kulipata katika dini, naweza kukuonesha mstari mwingine au tafsiri nyingine inayoweza kuchochea baya.

Kwenye Biblia hapa utaambiwa jicho kwa jicho na jino kwa jino, pale utaambiwa atakayekupiga shavu moja, mpe akupige na la pili.

Kwenye Quran hapa utaambiwa dini halilazimishwi, pale utaambiwa atakayekataa kusilimu mfukuze bila neema.

Dini haina mahubiri yaliyo consistent.

Na haina mahubiri consistent kwa sababu inetungwa na watu tu waliojaribu kukabili mazingira yao ya wakati huo.

Sasa mazingira yanavyobadilika, na mahubiri yanabadilika.
Sasa si ndio inatakiwa kubadilika kukabiliana na mabadiliko ya utandawazi?
 
Mimi nadhani nyakati zimebadilika, ila dini imejifunga katika kifungo cha mapokeo.
ukweli ni kwamba nyakati zote ni za Mungu, jana leo na kesho ni ya Mungu. Na Mungu anasema kama "LEO" Mtaisikia sauti yangu msiifanye migumu mioyo yenu.

anaposema leo ana maanisha leo na sio jana. Na kesho ikifika itakua leo.

ila dini zimebaki jana, sijui ibrahimu alifanya hivi na sisi tufanye. Mara musa mitume manabii wakale nk.
kumbe wale walifanya kwa mazingira yao ambapo kwao ilikua ni leo kwa kwa kipindi hicho.

dini zetu leo zina ihubiri jana katika leo, na ndio maana leo inaikosoa jana ya kuwa imepitwa na wakati yaani tecnogia.
na ndipo wakina Kiranga wanapata hoja.
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Habari wadau
Ukiangalia kwa makini kiwango cha maovu na vitendo vya uvunjifu wa maadili vinazidi kuongezeka licha ya uwepo wa dini na madhehebu kila kona
Ushoga,kusagana,sijui biriani,wanaume kama mabinti na ubinafsi ni baadhi tu huku dini nazo zikichanja mbuga majengo makubwa ya makanisa na misikiti inapamba miji,manabii,wasoma dua na kisomo nk wametapakaa kila kona lakini hatuoni impacts yao kupunguza uovu nchini.Je watu wa dini wabadili mbinu za medani ili kukabiliana na utandawazi wenye nguvu ya teknolojia?
Karibu kwa maoni ya nini kifanyike ili kujenga jamii bora yenye hofu ya Mungu

Hapana.

Dini zilijengwa kwenye misingi ya uwongo na vitisho visivyo na mashiko ambayo inaelekea kupoteza maana tena.

Kwenye dini kuna uwongo ambao kwa karne hizi watu hawawezi kuamini tena.

Ni suala la muda tu dini hizi zilizolenga kutupumbaza huku wakoloni wakinyakua rasilimali zetu zitakufa.
 
Dini zimezidiwa kwa sasa watu hawaogopi tena dhambi.
Habari wadau

Ukiangalia kwa makini kiwango cha maovu na vitendo vya uvunjifu wa maadili vinazidi kuongezeka licha ya uwepo wa dini na madhehebu kila kona.

Ushoga, kusagana, sijui biriani, wanaume kama mabinti na ubinafsi ni baadhi tu huku dini nazo zikichanja mbuga majengo makubwa ya makanisa na misikiti inapamba miji, manabii, wasoma dua na kisomo n.k. wametapakaa kila kona lakini hatuoni impacts yao kupunguza uovu nchini. Je, watu wa dini wabadili mbinu za medani ili kukabiliana na utandawazi wenye nguvu ya teknolojia?

Karibu kwa maoni ya nini kifanyike ili kujenga jamii bora yenye hofu ya Mungu
 
ukweli ni kinyume cha uwongo, sasa ulivyosema dini imejengwa juu ya uwongo ndio nikauliza sayansi imejengwa katika ukweli?
Sayansi imejengwa katika ukweli kwamba

1. Haina majibu ya kila kitu.
2. Inagunduliwa na watu tu.
3. Inabidi iende ikijiongeza kutafuta majibu yaliyo ya ukweli zaidi.

Ndiyo maana Newton alikuwa sahihi, lakini Einstein akamuongezea usahihi kwenye Relativity kwa kuonesha kwamba, kwenye gravity kubwa au velocity kubwa, equations za Newton hazifanyi kazi, utahitaji equations za Relativity ya Einstein.

Ukitumia internet hapa, unatumia satellite system, ukitumia satellite system, unatumia sayansi ya Einstein ya Relativity. Hutakiwi kusema sayansi hii imejengwa katika uongouongo wakati unaitumia.

Katika sayansi unaruhusiwa kusema hapa nyuma tulikosea, au tulipatia lakini hatukujua mengine.

Siyo tu unaruhusiwa, unatiwa moyo utafute makosa. Ukigundua makosa katika Relativity ya Einstein, ukachapisha paper, mwakani una uwezekano mkubwa sana kupewa nishani ya Nobel.

Dini ukiikosoa unaambiwa umekufuru. Ukiwa Saudi Arabia unaweza kuchinjwa.

Dini inaanza kwa kusema hili ni neno la Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, neno lisilo na kosa.

Na hapo ndipo unapoanza uongo.

Kwa sababu huyo Mungu hayupo
 
Interesting ni kwamba huyo mwenye upendo mkuu alishindwa kuumba dunia isiyokuwa na natural phenomena zinazoangamiza maelf ya watu bila makosa yao...eg vibunga, tetemeko...sunami nk....

Huu upendo lazima ni wa kipekee sana.
Sayansi imejengwa katika ukweli kwamba haina majibu ya kila kitu, inagunduliwa na watu tu, na inabidi iende ikijiongeza kutafuta majibu yaliyo ya ukweli zaidi.

Back
Top Bottom