Swali:English ni official language Tanzania?

mawemeusi

Member
Oct 13, 2012
28
13
Miaka hii ya karibuni nimeona baadhi watu wakitetea Kiswahili kitumike kwenye mikutano au kwenye dhiara za viongozi wanapotoka nje ya nchi au wanapopata wageni kutoka nje.
1)HV official language ya Tz in hipi?
2)Kuna haja gani Tz kuweka somo la English kuanzia primary na masomo yote kufundishwa kwa English kuanzia Sec?
NAOMBA MSAADA MNIFAFANULIE KWANINI TUCHAGUE KISWAHILI NA SIO ENGLISH.HILIHALI ENGLISH HUFUNDISHWA KWA MSISITIZO MKUBWA.
 
jibu ni ndio, english ni official language in tanzania cha ajabu mtukufu haielewi vizuri, huyu anaweza kuwa kiongozi wa kwanza duniani kutojua kiufasaha lugha ya nchi yake, mwenzie kama kagame anaongea english, french na kiswahili kiufasaha!
Nyerere aliwahi kusema fikra sahihi huja kwa lugha sahihi.
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Kwenye majukwaa mengi ya kimataifa Tanzania inajulikana kuwa ina Official Language 2, Kiingereza na Kiswahili. Hii ni kwa sababu tunakitumia katika mitaala ya Elimu.
 
Tanzania Lugha ya Taifa ni kiswahili na Lugha rasmi ni kiswahili. Ninaposema lugha rasmi ninamaanisha official language. Kufundishwa aina fulani ya lugha tangu primary hakuipi lugha hadhi ya kuws rasmi bali matumizi ndiyo yanaifanya lugha irasimishwe. Ni kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa kiswahili ndiyo maana ilirasimishwa. Ndio maana ofisi zote za serikali lugha ya mawasiliano inayotumika ni kiswahili. Bunge linaendesha mikutano kws kiswahili. Wimbo wa taifa tunaimba kwa kiswahili. Nembo ya taifa ina maneno ya kiswahili. vyote hivi havijafanyika kwa bahati mbaya. Ndiyo lugha tuliyoirasimisha.
 
Kiswahili ndio lugha rasmi kwa shughuli zote za serikali. ukitaka kujua angalia barua nyingi zinazoandikwa na Wizara ya Utumishi ndio utafahamu kuwa Kiswahili ndio lugha rasmi. Hata hivyo English pia inaruhusiwa kutumika maofisini.
 
Ni kweli kuna haja gani ya kusisitiza English kama Kiswahili kinatosha?Kuna haja gani yakijifunza kitu ambacho hukutumii na unafundishwa miaka mingi na bado hatukielewi vizuri!!!
 
Back
Top Bottom