Swali Butu: Mambo haya 4 Magufuli anayafanya tofauti na Marais 3 waliomtangulia! Nani anabisha?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Na. M. M. Mwanakijiji

Yote tisa, kumi tuseme ukweli. Kuna mambo ambayo mtu anaweza kuamua kuyachukia dhidi ya Rais Magufuli. Mtu anaweza kuamka na kuapa kwa jina la miungu na mababu zake ya kwanini hataki kulisikia jina la Rais Magufuli. Tena mtu anaweza akaamka hata usiku wa manane kama mtu aliyepatwa na jinamizi akiwa na hofu ya Magufuli. Siwezi kuwasemea wale ambao wakisikia jina la Rais Magufuli wanaweza kujihisi pumzi zinawaisha na kujisikia unyonge. Umpende au umchukie Rais Magufuli bado anaonekana kugawa hisia za watu mbalimbali tena kwa ukali sana; ama unamkubali au unamkataa; hakuna upande wa katikati.

Na wapo pia ambao wanaposikia jina la Magufuli kwao wanajisikia matumaini, faraja, na wengine wanakuwa kama yule mwanamuziki aliyeimba wimbo wa “Magufuli Raha Tu”. Hawa wanaposikia jina la Rais Magufuli ni kama wanapata Amani ya huko mbeleni, wanajua nchi iko salama na kuwa wao na watoto wao wanashuhudia mambo ambayo labda hayakudhaniwa kuwa yanaweza kutokea katika nchi hii hii ya Waafrika tena miongoni mwa zile nchi zilizokubali jina la “Maskini Zaidi” duniani. Kwa hawa ukitaja jina la Magufuli hata ukiwaamsha usingizini wengine wanaweza kuhisi ni kama unawakatisha zile ndoto tamu tamu zinazoweza kumfanya mtu ajikute anatafuna mto akidhania ni keki!

Vyovyote vile ilivyo kuna mambo manne ambayo naweza kuyasema kwa ufupi tu ambayo Rais Magufuli anayafanya tofauti sana na viongozi wengine. Bila ya shaka kuna mengine anayafanya ambayo yanafanana na watangulizi wake na kubwa katika hayo ni ile hali ya kutukuza chama chake na kukifanyia kila namna ya msaada na mbinu ya kutaka kiendelee kubakia madarakani kwa miongo mingi ijayo. Sidhani kama kuna kiongozi atakayekuja kutoka CCM ambaye atafikiria au kujaribu kufanya kinyume cha hilo. Hata hivyo, binafsi ningependa kudokeza yale mambo ya kiutendaji (executive) ambayo Rais Magufuli anayanya – kwa maoni yangu – kwa namna tofauti na viongozi watatu waliomtangulia.

1. Dhana ya Kujitegemea Ameipa Magurudumu
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati anaikaripia serikali ya Rais Mkapa kufuatia ile sera ya “ubinafsishaji wa mashirika ya umma” na ile hali ya kujaribu kuendekeza sana “wawekezaji wa nje” aliwahi kusema hivi (naapa nimenyambulisha kidogo) “Mnaweza kuamua kuachana na siasa ya ujamaa, lakini hamuwezi kuachana na sera ya kujitegemea”.

1574092280084.png

Rais na viongozi wengine wakiangalia modeli ya bwawa la kufulia umeme la Nyerere, Rufiji.

Nadharia hii ya “Kujitegemea” ni miongoni mwa dhana ambazo bila kueleweka zinaweza kumfanya mtu awe duni mbele ya wengine. Mtu ambaye ni “tegemezi” au Nyerere aliita “ombaomba” kwa kiasi fulani anajidunisha mbele yaw engine. Kwa muda mrefu nchi zetu hizi za Kiafrika zilifika mahali za kuomba hadi misaada ya kujenga vyoo! Na bado hata leo kuna watu ambao wanasubiria serikali iwafanyie vitu ambavyo hata vilivyopo ndani ya uwezo wao. Kurudi kwenye “kujitegemea” ni kurudi kwenye kuuheshimu na kuulinda utu wetu kama binadamu. Hivi ni kweli, tunahitaji msaada wa kigeni kupanda bustani ya maua shuleni, au kwenye ofisi? Je, ni kweli tunahitaji msaada kutoka SIDA, USAID, EU, JICA, DANIDA, NORAD ili kuweza kufanyia ukarabati shule zetu kongwe, kujenga shule mpya, kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za watoto wetu, au kujenga viwanja vya kuchezea watoto na maktaba? Magufuli anaposema “tunaweza” anataka kutuambia kuwa “tumechelewa kujitegemea!”

Magufuli tangu kuingia kwake madarakani ameamua kulishikilia hili kama kwa mapembe. Analazimisha Taifa liwe na fikra za kujitegemea. Na hapa ni katika kutumia raslimali zake, uwezo wake, watu wake na mipango yake katika kujiletea maendeleo. Hakuna jambo linalotishia uhuru na utu wetu kama taifa kama kutegemea watu wa nje kwa mafanikio yetu. Jambo hili la kulazimisha taifa kujitegemea linaweza kuwa ni mafanikio makubwa zaidi ya Rais Magufuli kuliko mambo mengine.

Binafsi sitoshangaa kwa mwaka unaokuja Magufuli akiagiza wizara na idara zote kuandaa bajeti zao za 2020/2021 bila kuweka ndani au kusubiria misaada ya kigeni. Sitoshangaa kabisa akaamua kutukatisha kunyonya (weaning) kutoka kwa mashangazi zetu wa Ulaya na kulazimisha taifa kupanga bajeti yake kwa kutumia mapato na vyanzo vyake vya ndani. Misaada ya kigeni ikawa siyo tena ya moja kwa moja kwenye bajeti (Non-direct budgetary support). Akiamua kufanya jambo hili nawahakikishia dunia nzima itashtuka na hawatoamini na siyo hivyo tu wapo wenzetu humu humu (wapingaji) ambao watatuambia kwanini hatuwezi kujitegemea kwenye bajeti!

2. Amekataa Kuheshimu Sura
Kwa muda mrefu watu walikuwa wakishika madaraka walikuwa wanajiona wamefika. Watu walipoapishwa kushika ofisi yeyote walijisikia wako salama na wengine walifanya sherehe na kujisahau wakidhania sasa hatimaye na wao wamekuwa kwa waliokuwemo. Magufuli amewafanya sasa hivi watu kutokuwa salama kwenye vyeo vyao. Mtu anaweza kudhania hili ni jambo baya; lakini kiutawala hakuna jambo muhimu kama watu kurudi na kutambua dhana ya “cheo ni dhamana”. Hakuna aliye salama kwenye kiti chake na kuwa wakati huko nyuma watu walitegemea “Rais kuwalinda” sasa hivi hakuna anayeweza kuishi na kujihisi kuwa analindwa. Unaweza hata kuwaonea watu huruma.

Lakini kinyume na hisia ya wengi Rais Magufuli haoni aibu au kufikiria mara mbili kumuondoa hata mchezaji nyota kwenye mechi! Kulikuwepo na baadhi ya “wachezaji nyota” na wakajikuta wanaondolewa na mechi inaendelea kupigwa na watu wakashinda vile vile. Jambo hili limewafanya baadhi ya watu wanaojidhania au wanaojifikiria kuwa ni wachezaji nyota kujiangalia mara mbilimbili kweli kweli. Sasa hivi, hakuna kujali sura, tunajali utendaji wa kazi. Niliandika mada moja mwanzoni mwa utawala wa Magufuli na labda watu hawakuelewa uzito wake; nilisema “Tengua Tengua Inayokuja”. Sasa hivi ukipewa kiti cha utawala sheherekea huku unatokwa machozi. Wale wale watakaokuletea maua ya pongezi ndio watakaomletea mwingine maua ya pongezi.

Matokeo ya hili ni kuwa tunaona watendaji wengi – hasa mawaziri – wakiwa wanyenyekezu, wenye kujituma na kila mmoja akijitahidi kujionesha yuko kazini. Hata yule mwana mpendwa baada ya kupigwa mkwara wa juzi, tunamuona naye sasa hivi anakalia kitu kwa kukinyemelea! Wanaofikiria Magufuli anaiheshimu sana sura yake, watakuja kushangaa sana siku si nyingi.

3. Amekuwa Muwazi Mno hadi Kupitiliza
Kwa muda mrefu tulikuwa hatujui mambo yanayoendelea ndani ya serikali yetu. Mambo mengi tulikuwa tunayasikia kwenye majungu tu na vijiwe. Mambo mengine tulikuwa hata hatuyajui kabisa lakini sasa hivi ni kama tumefunguliwa mlango na madirisha tuchungulie kinachoendelea ndani. Rais Magufuli kwa ile tabia yake ya kutokuwa mzuri sana wa maneno, na kukataa kuyapamba maneno yake anaweza kuonekana wakati mwingine kama “fyatu” fulani hivi. Lakini kwa wanaomjua na sisi ambao tumemfuatilia kwa muda mrefu tunajua ni kuwa hana tabia ya kuficha ficha. Hata ile kauli yake maarufu ya “Msema kweli mpenzi wa Mungu” kimsingi inatuambia tu kuwa haoni sababu ya kwanini Watanzania wafichwefichwe. Kile anachoamini ni ukweli atakisema hadharani na wazi kabisa na wakati mwingine kutoificha aibu ndani ya serikali yake mwenyewe. Na watu wakaona – wakamsema na hata kumnyoshea kidole yeye mwenyewe. Rais wetu kwa kiasi kikubwa hana siri sana! Kuna mambo ya siri lakini ukiangalia sana mambo mengi ambayo watu wangependa kuwa ya siri hayana usiri wa maana kivile zaidi ya kufichiana tu siri zisizo na maana.

Uwazi huu umewasaidia wananchi kuona nini kilikuwa kinafanyika na nini kinafanyika sasa hivi. Bahati mbaya inaweza kusemwa ni kuwa uwazi huu ungenoga zaidi kama vyombo vya habari visingekuwa vinajisikia vinabanwa au kuulizwa ulizwa vinapojaribu na vyenyewe kufichua mambo. Hili sitolishangaa litatokea pia kwani “msema kweli ni mpenzi wa Mungu”. Siyo majungu, siyo umbeya, siyo porojo bali ukweli tu. Kwa vile Rais ameamua kuwa muwazi kwa wananchi ni lazima awaache na wananchi wawe wawazi kwa serikali yao; kwa maana halisi ya quid pro quo (nipe nikupe). Hakuna haja ya kufichana.

4. Ameamua Kufanya Ujenzi Mpya wa Taifa
Mojawapo ya mambo ambayo labda ni kubwa zaidi (linaloendana na lile la kwanza) ni uamuzi wake wa kufanya ujenzi mpya wa taifa (national reconstruction). Magufuli ni kama amedakia alipoachia Nyerere. Ukiangalia sasa hivi ni kana kwamba miaka ya Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete haipo. Ni kama Magufuli ameamua kuifuta na kuichukua nchi mwaka 1985. Akiichukua nchi mwaka 1985 anaikuta nchi ambayo imetoka kwenye janga la wahujumu uchumi (ufisadi), viongozi ambao wameshaonja ubepari na sasa kila mtu anataka kula kwa raha zake, na kuwa analikuta taifa ambalo wananchi wake wanatafuta maisha bora. Magufuli anaingia na kuamua kuendeleza mambo yale ya msingi ya kujenga misingi.

1574091954441.png

Ujenzi wa Tanki la Maji huko Singida

Katika hili ameamua kufanya masuala ya ardhi na makazi, miundombinu (infrastructures), elimu, maji, umeme na nishati, kilimo, madini na afya. Katika mambo haya Rais Magufuli anajaribu kupalilia nchi na kupanda mbegu ili wengine waje kuvuna. Na anachofanya – na labda wakati mwingine wengi hawasikii – ni kuwa katika nchi nzima, na kwa wakati ule ule (simultaneously) miradi mbalimbali inatekelezwa.

Anachokifanya ni kuhakikisha kuwa hakuna sehemu kubwa ya nchi ambayo inaweza kujihisi inapitwa. Ukiwasikiliza watu wenye kukosoa kinachofanyika “Chato” unaweza ukadhania Magufuli amegoma kufanya jambo lolote sehemu nyingine ya nchi. Hili linaweza kuwa ni udhaifu wa taasisi zenyewe kujieleza lakini kwa tunaofuatilia tunajua jinsi gani matanki ya maji, njia za umeme, hospitali, vituo vya afya, barabara, vinavyoendelea kujengwa au vilivyokwisha jengwa ndani ya miaka hii minne kulinganisha na miaka mingine yote.

Mwisho
Mambo haya manne Magufuli anayafanya kwa namna ya tofauti sana. Lakini tofauti hiyo naweza kuielezea inatokana na mambo makubwa mawili ambayo hayakuwepo huko nyuma. Moja ni kuwa amekataa kufuata kilichoandikwa vitabuni. Kwamba, namna ya kufanya mambo ni a, b, na c kama watu walivyosoma shuleni. Badala yake anawalazimisha watendaji walio chini yake kufikiria nje ya sanduku na kujaribu vitu tofauti. Matokeo yake baadhi ya mambo ambayo yangekuwa yanachukua muda zaidi au raslimali zaidi yanaweza kufanyika kwa ubora na uharaka kuliko huko nyuma. Chukulia mfano wa mambo mawili tu kati ya mengi – suala la Masoko ya Madini na Vituo vya Mabasi – mambo haya hayakutangaliwa na vikao virefu vya sera na mipango; ni mambo ambayo yaliamriwa na watu wakapewa kazi kwenda kuyatekeleza.

Jambo la pili ni kuwa Rais Magufuli hana hofu ya kukosea au kuonekana amekosea. Kwa wanaomjua Magufuli hili wala si jambo jipya. Toka zamani Magufuli amekuwa ni mtu wa kufikiria kitu na kukitenda labda wakati mwingine kwa gharama kwa serikali au hata hadhi yake; lakini hofu ya matokeo ya kisheria (legal ramification) haijamzuia Magufuli kufanya kitu anachoamini ni sahihi. Hofu ya kuogopa kushtakiwa, au kugombana na wakubwa haikumzuia. Tuliona hili wakati wa suala la Makanikia na jinsi gani baadhi ya watu waliona kama Magufuli amegusa wakubwa na hatokuwa salama tena. Lakini Magufuli alisimamia kile hadi dakika ya mwisho. Hata hili suala la ujenzi wa Bwawa la Nyerere; kwa wengine liliwatia hofu kuwa wakubwa watetezi wa “mazingira” wangemkwamisha; lakini kama huwaombi dola zao watakukwamisha kwa lipi?

Miye nasubiria watakapoanza kutengeneza zile “cable cars” kuruka Ngorongoro na kutengeneza viewing platforms kama zilizoko kwenye vivutio vingi kwenye nchi za wenzetu (nenda pale Grand Canyon utaona). Sitoshangaa kuna watu watapiga kelele kweli. Wakati wenzetu wana barabara za lami zikikatisha Yosemite Parks na Parks nyingine huko majuu sisi kwetu tunaambiwa hata zinatishia wanyama na kuvuka kwa wanya kana kwamba hakuna namna ya kushughulikia hilo. Hili la pili ndio linaweza au limeweza kumtengeneza Magufuli maadui wengi wan je. Hana heshima kwao na kitendo chake cha kutokwenda kwao “kujionesha onesha au kujitambulisha” kunawakwaza wengi kweli kweli. Rais wa Afrika asiyependa kushikana mikono huko New York, Geneza, Paris na London ni mtu wa tofauti sana.

Mambo haya 4 bila ya shaka Magufuli anafanya tofauti sana na wengine watatu waliomtangulia. Inawezekana yapo mengine mengi ambayo anayafanya tofauti na wenzake. Na hapa nazungumzia yale chanya. Mtu mwingine anaweza kubisha. Nani anabisha?

Niandikie:
mwanakijiji@jamiiforums.com

======
Mawazo ya wadau

1. Kuipa magurudumu dhana ya kujitegemea.

Magufuli ni mtu mwenye utovu wa elimu ya kisiasa. Ni Mkemia aliyejikuta kwenye siasa. Hajui akitaka kujitegemea aanzie wapi.

Yupo incoherent.

Mfano mdogo. Aliona kuingilia biashara ya korosho kwa nguvu ya jeshi ndiyo kitu kizuri. Akaonywa hilo si jambo jema na litaangusha mapato, hakusikia, matokeo yake, ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania ya Oktoba 2019 inasema mapato ya exports za mazao ya kilimo kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 yameanguka kwa asilimia 55, ukiyalinganisha na ya mwaka uliopita. Sababu kubwa kabisa ya kuanguka huku ni serikali ilivyoingilia kwa mabavu biashara ya korosho, zao la kwanza kwa kutupatia fedha za kigeni.

Kwa kila shilingi 1000 tuliyopata mwaka wa kabla ya huu uliopita, kwa mwaka uliopita tumepata shilingi 450, hasara ya shilingi 550, zaidi ya nusu nzima!

Mtu aliye incoherent, ambaye anakwenda kwa kuhamanika kwa munkari bila mkakati, hawezi kutupa hoja ya kujitegemea.

2. Magufuli hajakataa kuheshimu sura. Anatengeneza image ya uongo kwamba yeye haheshimu sura. Magufuli angekuwa haheshimu sura kweli, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, angekwishaondolewa siku nyingi sana. Makonda ana scandals nyingi sana. Scandal iliyomvua nguo kabisa Magufuli ni pale Makonda alipotaka kuingiza samani kwa ujanjaujanja, Magufuli akamsema kama anamuogopa vile, wakati kawaida yake anatumbua watu kabla hotuba haijaisha. Hili limetuonesha kwamba Magufuli ni bully tu, anawa bully watu fulani, akifika kwa watu wake kina Makonda anachekacheka, hata wavamie redio na bunduki au waingize vitu bila kulipa kodi. Kabakia kutukana viongozi wenziwe na wake zao tu.

3. Uwazi
Uwazi ni kitu kizuri. Lakini there is such a thing as "too much information". Rais anatakiwa kuwa muwazi, lakini anatakiwa kuwa na kifua cha kuweka maneno.Magufuli hana kifua cha kuweka maneno, anaropoka sana, huu si uwazi. Kuna tofauti ya mtu kuwa muwazi na mtu kuwa mropokaji. Magufuli si muwazi, ni mropokaji. Usichanganye hayo mawili.

4. Ameamua kufanya ujenzi mpya wa taifa

Kuna habari moja, sijui kama ni ya kweli au kutungwa, lakini ina funzo zuri, hivyo kwa msingi huo, naiona inafaa kurudiwa, hata kama ni ya kutungwa, kwa sababu ina mafunzo mema.

Wanasema kulikuwa na Waziri mmoja wa Fedha wa Nigeria. Alienda Uswizi kwenye mabenki makubwa ya dunia. Akaaulizia, hapa benki kubwa kabisa inayoficha hela za vigogo wa Nigeria iko wapi? Akatajiwa. Akaenda ile benki, akasema mimi waziri wa fedha wa Nigeria, naomba kuongea na mkurugenzi wenu.

Akapewa appointment na Mkurugenzi, akaenda kuongea naye.

Akamwambia Mkurugenzi, nimekuja hapa nina shida, Africa tunaibiwa sana fedha. Nataka unipe list ya wateja wako wa kutoka Nigeria, na hela walizoweka katika benki yako, tuwahakiki na biashara zao kama hela hizi ni halali, wanalipa kodi etc.

Yule Mkurugenizi Swiss banker akamwambia wewe jamaa una kichaa ama nini? Sisi tuna sheria za kulinda wateja wetu hapa. Waziri akamwambia mimi sijajja kufanya mchezo hapa, nina barua kutoka serikali ya Nigeria. Mswizi akamwambia hata ingekuwa serikali ya Uswizi au Marekani, hatujali, tuna sheria zinatulinda. Waziri akasema sawa, tutafuta deals zote za serikali ya Nigeria na benki yako, mtakosa hela nyingi sana. Yule Mkurugenzi akasema wala sijali. Waziri akatoa bastola, akamuwekea Mkurugenzi kichwani, akasema nipe majina haya, usiponipa nakufyatulia risasi ufe. Banker Mkurugenzi Mswizi akasema Waziri wewe niue tu, majina sikupi.

Waziri akasema, vizuri sana. Nimeitafuta benki yenye usiri kama hii kwa muda mrefu sana sijaipata. Haya hapa mamilioni yangu nataka mniwekee, maana kwa usiri huu umehatarisha mpaka maisha yako, nikiweka hela zangu hapa, hakuna atakayejua.

What is the point of this story? Mara nyingine watu wanaojifanya wakali sana kupinga rushwa, kujenga taifa etc, wanaweka show tu. Wao hao hao ndio wapigaji wakubwa na wala rushwa wakubwa.

Magufuli hawezi kuwa ameamua kujenga taifa, kwa sababu analigawa taifa kisiasa, ameharibu umoja wa kitaifa kuliko rais yeyote aliyempita, anasema wazi kwamba atapendelea watu wa CCM. Sasa hapo anajenga taifa au anajenga watu wa chama chake?
 
Jibu kwa hoja siyo hasira. Wewe uko upande Wa pili kwa hiyo siyo ajabu kuwa na majibu ya hasira hivi
Hakuna hoja kama mtu kaandika ujinga! Can he tell ua the story of Lisu, Azory, Ben and many many many others? Unadhani Idd Amin hakufanya yote hayo? makaburu walifanya 1,000,000 times ya hayo lakini walipigwa vita! Unafiki kwa vile ni msukuma, walimsakama Jk sana hawa watu, namkumbuka sana MMK.... leo atrocities za JPM hazioni kama the so called Maaskofu/some masheikh...
 
Baniani mbaya bali kiatu chake dawa, kama kwa mambo makubwa ya maendeleo ya vitu Mheshimiwa anafanya makubwa. Na ni imani yangu kuwa mpaka ifikapo mwaka 2025 watu wengi wataridhika na jitihada zake. Mimi kwa upande wangu naamini atakuja na ilani ya CCM ya 2020 ikiwa imebeba vitu vichache, ili hivi alivyovianzisha akapate kuvikamilisha.
 
Asante MMJ

Naona comment zinazokuchallange unazifuta
Retired

Lakini kitu ulichoandika ni professional Rubbish hii ni sababu ya kulinda mkate
Sasahvi cheo ni kuunga juhudi na juhudi yenyewe ni kulinda mkate wa ubalozi wa kupewa

1. Kama nchi ameipa gurudumu la kujitegemea mbona deni la taifa linapanda kila mwaka?

2. Ujenzi wa taifa wakati anatugawa watanzania?? Unajengaje taifa wakati democracy kwenye nchi ni zero? Unajenga taifa ambalo viongozi.hawana UTU?

3. Rais amekuwa muwazi ????kwa kusema uwongo,MMJ rudisha akili.yako iliyopotea na andika vitu vyenye uhalisia

4. amekataa kuheshimu.sura? Kama amekataa kuheshimu sura mbona viongozi wake wanaonekana wahuni mbele ya jamii na anawaacha mfano bashite na wengine?

Mwisho MMJ acha kutumika haikusadii

Nguvu unayotumia kusafisha hewa chafu ndio unatia uvundo. Heshimu akili yako uliyopewa na mwenyezi Mungu
 
Baniani mbaya bali kiatu chake dawa, kama kwa mambo makubwa ya maendeleo ya vitu Mheshimiwa anafanya makubwa. Na ni imani yangu kuwa mpaka ifikapo mwaka 2025 watu wengi wataridhika na jitihada zake. Mimi kwa upande wangu naamini atakuja na ilani ya CCM ya 2020 ikiwa imebeba vitu vichache, ili hivi alivyovianzisha akapate kuvikamilisha.
Endeleza maisha ya watu kisha maendeleo ya vitu yatakuja taratibu.
 
1. Kuipa magurudumu dhana ya kujitegemea.

Magufuli ni mtu mwenye utovu wa elimu ya kisiasa. Ni Mkemia aliyejikuta kwenye siasa. Hajui akitaka kujitegemea aanzie wapi.

Yupo incoherent.

Mfano mdogo. Aliona kuingilia biashara ya korosho kwa nguvu ya jeshi ndiyo kitu kizuri. Akaonywa hilo si jambo jema na litaangusha mapato, hakusikia, matokeo yake, ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania ya Oktoba 2019 inasema mapato ya exports za mazao ya kilimo kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 yameanguka kwa asilimia 55, ukiyalinganisha na ya mwaka uliopita. Sababu kubwa kabisa ya kuanguka huku ni serikali ilivyoingilia kwa mabavu biashara ya korosho, zao la kwanza kwa kutupatia fedha za kigeni.

Kwa kila shilingi 1000 tuliyopata mwaka wa kabla ya huu uliopita, kwa mwaka uliopita tumepata shilingi 450, hasara ya shilingi 550, zaidi ya nusu nzima!

Mtu aliye incoherent, ambaye anakwenda kwa kuhamanika kwa munkari bila mkakati, hawezi kutupa hoja ya kujitegemea.

2. Magufuli hajakataa kuheshimu sura. Anatengeneza image ya uongo kwamba yeye haheshimu sura. Magufuli angekuwa haheshimu sura kweli, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, angekwishaondolewa siku nyingi sana. Makonda ana scandals nyingi sana. Scandal iliyomvua nguo kabisa Magufuli ni pale Makonda alipotaka kuingiza samani kwa ujanjaujanja, Magufuli akamsema kama anamuogopa vile, wakati kawaida yake anatumbua watu kabla hotuba haijaisha. Hili limetuonesha kwamba Magufuli ni bully tu, anawa bully watu fulani, akifika kwa watu wake kina Makonda anachekacheka, hata wavamie redio na bunduki au waingize vitu bila kulipa kodi. Kabakia kutukana viongozi wenziwe na wake zao tu.

3. Uwazi
Uwazi ni kitu kizuri. Lakini there is such a thing as "too much information". Rais anatakiwa kuwa muwazi, lakini anatakiwa kuwa na kifua cha kuweka maneno.Magufuli hana kifua cha kuweka maneno, anaropoka sana, huu si uwazi. Kuna tofauti ya mtu kuwa muwazi na mtu kuwa mropokaji. Magufuli si muwazi, ni mropokaji. Usichanganye hayo mawili.

4. Ameamua kufanya ujenzi mpya wa taifa

Kuna habari moja, sijui kama ni ya kweli au kutungwa, lakini ina funzo zuri, hivyo kwa msingi huo, naiona inafaa kurudiwa, hata kama ni ya kutungwa, kwa sababu ina mafunzo mema.

Wanasema kulikuwa na Waziri mmoja wa Fedha wa Nigeria. Alienda Uswizi kwenye mabenki makubwa ya dunia. Akaaulizia, hapa benki kubwa kabisa inayoficha hela za vigogo wa Nigeria iko wapi? Akatajiwa. Akaenda ile benki, akasema mimi waziri wa fedha wa Nigeria, naomba kuongea na mkurugenzi wenu.

Akapewa appointment na Mkurugenzi, akaenda kuongea naye.

Akamwambia Mkurugenzi, nimekuja hapa nina shida, Africa tunaibiwa sana fedha. Nataka unipe list ya wateja wako wa kutoka Nigeria, na hela walizoweka katika benki yako, tuwahakiki na biashara zao kama hela hizi ni halali, wanalipa kodi etc.

Yule Mkurugenizi Swiss banker akamwambia wewe jamaa una kichaa ama nini? Sisi tuna sheria za kulinda wateja wetu hapa. Waziri akamwambia mimi sijajja kufanya mchezo hapa, nina barua kutoka serikali ya Nigeria. Mswizi akamwambia hata ingekuwa serikali ya Uswizi au Marekani, hatujali, tuna sheria zinatulinda. Waziri akasema sawa, tutafuta deals zote za serikali ya Nigeria na benki yako, mtakosa hela nyingi sana. Yule Mkurugenzi akasema wala sijali. Waziri akatoa bastola, akamuwekea Mkurugenzi kichwani, akasema nipe majina haya, usiponipa nakufyatulia risasi ufe. Banker Mkurugenzi Mswizi akasema Waziri wewe niue tu, majina sikupi.

Waziri akasema, vizuri sana. Nimeitafuta benki yenye usiri kama hii kwa muda mrefu sana sijaipata. Haya hapa mamilioni yangu nataka mniwekee, maana kwa usiri huu umehatarisha mpaka maisha yako, nikiweka hela zangu hapa, hakuna atakayejua.

What is the point of this story? Mara nyingine watu wanaojifanya wakali sana kupinga rushwa, kujenga taifa etc, wanaweka show tu. Wao hao hao ndio wapigaji wakubwa na wala rushwa wakubwa.

Magufuli hawezi kuwa ameamua kujenga taifa, kwa sababu analigawa taifa kisiasa, ameharibu umoja wa kitaifa kuliko rais yeyote aliyempita, anasema wazi kwamba atapendelea watu wa CCM. Sasa hapo anajenga taifa au anajenga watu wa chama chake?
 
Hapa ulichofanya mleta mada ni kutoa sifa za twiga kiasi kwamba hizo sifa zikawa zina ukweli kiasi fulani lakini zikapoteza ukweli. Yaani unasema twiga ni mrefu kuliko kitu chochote duniani, wakati ukweli ni kuwa twiga ni mrefu, lakini sio mrefu kuliko kitu chochote duniani.
 
Mimi nina maswali mawili kwako MMK
Mosi: dhumuni la mada yako ni kutaka kumsifia? Ndio.mana umesema ule upande unaomkosoa hutaki kuugusia?

Pili: hivi haya aliyoyafanya ambayo ww umeyasifia je? Hayakuwa na njia.nzuri ya kufanya na yalete tija ile ile au ni.mpaka kwa mabavu, kashfa na ukali hivi?
 
Back
Top Bottom