Swalah ya Kuomba Mvua

njia ya saada

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2018
Messages
280
Points
250

njia ya saada

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2018
280 250
Dalili ya Usheria wa Swalah ya Kuomba Mvua
Swalah ya kuomba mvua ni sunnah iliyotiliwa mkazo kwa kitendo cha Mtume ﷺ, kama ilivyo kwenye hadithi iliyopokelewa na Abdullah bin Zaid t kwamba Mtume ﷺ alitoka kwenda kwenye kiwanja cha kuswali akaomba mvua, akaelekea Kibla, akageuza kishali chake na akaswali rakaa mbili) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Wakati wa Swala ya Kuomba Mvua
Wakati uliowekwa na Sheria wa Swala ya kuomba mvua ni ardhi inapokuwa kavu na mvua kutonyesha, au yanapokuwa machache maji ya chemchemi na visima, au mito ikakauka na mfano wake. Inapendekezwa ifanyike baada ya jua kuchomoza na kufikia kadiri ya mkuki na wakati huo kwa kiasi ni baada ya kuchomoza jua kwa dakika ishirini kama vile Swala ya Idi.
https://www.al-feqh.com/sw/swala-ya-kuomba-mvua
 

Forum statistics

Threads 1,389,660
Members 527,997
Posts 34,031,372
Top