swalah ya ijumaa

njia ya saada

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2018
Messages
280
Points
250

njia ya saada

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2018
280 250
Sunna ya baada ya Ijumaa inaswaliwa rakaa mbili kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Umar t kuwa alisema: (Alikuwa Mtume wa Mwenyezi ungu ﷺ akiswali rakaa mbili baada ya Ijumaa nyumbani kwake) [Imepokewa na Jamaa.],

au nne, kwa neno la Mtume ﷺ: (Atakayekuwa ni mwenye kuswali miongoni mwenu baada ya ijumaa, aswali rakaa nne) [Imepokewa na Muslim].

na lililo bora ni aziswali nyumbani kwake.

7. Idi na Ijumaa zinapokusanyika, kwa kutoka shakani ni aswali Idi na Ijumaa. Na akiswali Idi ni lazima, kwa uchache, aswali Adhuhuri. Na inaruhusiwa kwa watu wanaokaa mbali, wakiswali Idi, wasirudi kuswali Ijumaa. Amepokewa Iyaas bin Ramlah al- Shaami akisema: (Nilimshuhudia Mu’awia akimuuliza Zaid bin Arqam: “Je uliwahi kushuhudia pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Idi mbili pamoja? Akasema: “Ndio. Aliswali Idi mwanzo wa mchana, kisha akatoa ruhusa kuhusu Ijumaa, akasema: ‘Atakaye kukusanya, basi na akusanye)[Imepokewa na Ahmad.].
https://www.al-feqh.com/sw/swala-ya-ijumaa
 

Forum statistics

Threads 1,389,663
Members 527,997
Posts 34,031,414
Top