Swala ya Witr

njia ya saada

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2018
Messages
285
Points
250

njia ya saada

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2018
285 250
Hukumu ya Swala ya Witri na Fadhla zake
Witri ni sunna iliyotiliwa mkazo. Mtume ﷺ anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Anapenda Swala ya Witri basi Swalini Witri enyi watu wa Qur’ani ) [Imepokewa na Abu Daud.].

Na alikuwa Mtume ﷺ akidumu nayo akiwa mjini na akiwa safarini

Namna ya kuswali Witri
1. Uchache wa Swala ya Witri ni rakaa moja na wingi wake ni rakaa kumi na moja au kumi na tatu, anaziswali mbilimbili kisha anaswali moja ya kufanyia witri.

2. Na uchache wa ukamilifu ni rakaa tatu, ataswali rakaa mbili kisha atowe Salamu, kisha ataswali rakaa moja na atowe Salamu. Pia inafaa kwa mtu kuziswali hizo rakaa tatu kwa kikao cha Atahiyatu kimoja. Na inapendekezwa asome katika rakaa ya kwanza baada ya Fatiha sura ya Al-A’laa na katika rakaa ya pili sura ya Al-Kaafiruun, na katika rakaa ya tatu sura ya Al-Ikhlas, kwa hadithi iliyothubutu kutoka kwa ubayy bin Ka’b t kuwa alisema: (Alikuwa Mtume ﷺ akisoma katika rakaa ya kwanza ya witri ‘Sabbihisma Rabbikal A’laa’, na katika ya pili ‘Qul yaa ayyuhal kaafiruun’, na katika ya tatu ‘Qul Huwallaahu Ahad’) [Imepokewa na Nasaai.].

Wakati wa Witri:
upate taarifa zaidi tembelea website hii
https://www.al-feqh.com/sw/swala-ya-sunna
 

Forum statistics

Threads 1,392,181
Members 528,565
Posts 34,100,876
Top