SWALA MAALUM KWA JK na WANA CCM KWA UJUMLA WAO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SWALA MAALUM KWA JK na WANA CCM KWA UJUMLA WAO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Papa D, Apr 23, 2011.

 1. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu wa CCM,
  Juzi aliyekuwa mpinzani wa Rais Obama kwenye kinyang'anyiro cha Urais [Maccain]nchini Marekani alisafiri kwa niaba ya Taifa lake kwenda kujadili na wapinzani wa Gadaffi namna ya kumuondoa Gaddafi [source aljazeera]. Safari hiyo ilikuwa kwa maslahi ya taifa la Marekani [sote tunajua jinsi Republican na Demacrat walivyo mbalimbali kisiasa].
  Maswali yangu ni kwamba:-
  1. Je, inawezekana kumtuma aliyekuwa mpinzani wako [hapa naongelea JK dhidi ya Dr. W.S] wa karibu kukuwakilisha kwenye maswala muhimu ya maslahi ya taifa nje ya nchi?
  2. Je, unafikiri Maoni ya Lissu kuhusu muswada wa sheria ya mahakama yalistahili kuchukuliwa kichama zaidi badala ya kitaifa?
  3. Je, chama chako chaweza kujifunza kutoka kwa wenzetu jinsi ya kutofautisha siasa na utaifa?
  4. Ni sahihi kuwaona wapinzani maadai wa utaifa wetu hadi kupinga hata mambo ya msingi wanayoishauri serikali ya CCM?

  Wana Jamvi naomba aliye na maoni/majibu kwa niaba ya chama cha mapinduzi atusaidie kujibu hayo maswali!!
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimekupata mkuu! Usa wamekomaa katika demokrasia,sisi tunadandia. Tunadhani demokrasia ya vyama vingi, ingawa watawala hawataki. Bado wana mawazo ya utawala msonge. Haya, nawapisha wana ccm wajibu hoja.
   
 3. A

  Ame JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Haya yanawezekana tu iwapo viongozi wa siasa wapo kisiasa na siyo ki biashara/ajira katika siasa. Siasa za kwetu ni za kunyang'anyana matonge ya ugali maana ugali ni mdogo na midomo inayotaka kula ni mingi. Kungekuwa na maslahi ya kibepari bila kujihusisha na siasa usinge mwona mmoja wa wabunge wanao sema ndiyo bila kufikiria wanachokisema Bungeni. Wengi wa hao ni failures in life na hapo wako ku rescue maisha yao angalau waache kitu kwa watoto wao. Kama ni wazee basi wamestaafu na hapo ni sehemu ya kujipa pension. Mtu mwenye akili zake timamu hawezi kuwa parrot kiasi cha hao wasema ndiyo bila kutumia akili. Jaribu kutafuta CV zao wengi wako kimaslahi zaidi na siyo ki utaifa.
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tofauti ya Tanzania na US ni kwamba wao wanajali utaifa zaidi! Hapa kwetu iwe mbunge au kiongozi wa Chama akifanya jambo utasiki ni sisi ndio tuli ibua akiamanisha chama chake! Ndio mana hata bungeni mijadadala haiendi kwa Maslahi ya Taifa inaenda kwa maslahi ya vyama! Ndio maana utakisikia Kituo cha Haki za Binadamu Kina sema Bunge hili wabunge wa Chadema wamewafunika wabunge wa CCM! Hapa hakuna utaifa ni kujionesha kwa kuvipatia sifa vyama! Ndio maana hata CCM nao huchangia bungeni kwa lengo la kuua umaarufu wa Chama,kama hoja ya kambi rasmi bungeni ili kua ni kuipinga chadema isijinafasi bungeni! Tanzania bado tupo kivyama zaidi badala ya Utaifa!
   
 5. S

  Simon B james Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenye macho haambiwi tazama. Kama ccm wanaogopa kukubaliana na chadema kwenye mambo nyeti ya taifa. Nidhahiri hawa ni wapumbavu. Wana macho lakini hawaoni mpaka waelekezwe. Cha msingi tuunge mkono wanaharakati ili tuwatoe wajinga hawa bungeni 2015. Tusipo watoa upuuz huu wa Ccm utaendelea
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  'Nakipongeza chama chetu sikivu ndo maana kimeondoa mswada mbovu' mnafiki Anne Kilango Malecela
   
 7. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,241
  Trophy Points: 280
  Najibu la kwanza 2, tena kwa swali. Hivi unajua Maccain ana wadhifa upi katika serikali ya Obama. Na unajua ameenda Libya kama nani? Naunga mkono hoja Demokrasia hipo ughaibuni, lakini napenyewe kwenye baadhi ya nchi hasa hasa wanaojiamini ni wasafi kisiasa.
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tatizo hawataki kukubali hadharani ila mioyoni wanajua wanayoambiwa na upinzani una weight kubwa tu! Kwa mfano kashfa nyingi za ufisadi hata Rais mwenyewe aliwabeza waliozitangaza na kuziita uzushi, kwa walioshi mpaka leo nadhani tunashuhudia wanaimba wimbo waliokuwa wakisema hauna jipya ndani yake! Hata hili la muswada wa utawala wa mahakama, wanajua kwamba waliamua kuchukua akili zao na kuzitia mfukoni kwanza, lakini dhamiri zao zinajua kama walichopinga kwa mkumbo kina weight gani katika taasisi hiyo muhimu!
   
 9. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nadhani Chadema ndio wanao ongoza kutaka kuonekana jambo fulani wao ndio wamelianzisha na hili linafanya kuwe na mitizamo ya kivyama bila Utaifa! Utasikia chadema yawasha moto bungeni,chadema ndio ilianzisha suala hili....... Hovyo kabisa
   
 10. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Denoo49!
  nashawishika kutokubaliana na swali lako kwa sababu:
  1. Content za ziara ya Maccain ni kulinda maslahi ya Marekani [kuna thread moja iliwahi kuuliza hivi Tangu mwaka 1987 kuna kiongozi gani amewahi kusema sentensi hii " Kwa kizazi kijacho"] na wala si chama cha Republican au yeye mwenyewe. kwa hivo hiyo haijalishi wadhifa wake bali sera ya mambo ya nje ya taifa lake!!
  2. Maccain na Obama walipingana kwa sera [tena baadhi ya sera] sio mtu binafsi. lakini baada ya uchaguzi maslahi ya Marekani na Wamarekani yakabaki kuwa mbele badala ya chama.
  HIVO BADO NAENDELEA KUULIZA: Maswali yangu matatu. Pia nakuomba unijibu hilo swali la pili ulilolichagua!
   
 11. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  sipendi kuwa mshabiki sana wa chadema ila naomba nipe mfano mmoja wa jambo lililopitishwa bungeni kisha CDM wakatoka kwa maelezo kuwa wao ndio walilianzisha ukiondoa yale ambayo wabunge wa CCM waliyakataa kisha DCM wakayakomalia kwa maelezo kuwa wameyaanzisha na wanataka wananchi wawaunge mkono?
  Kumbukumbu zangu zinaonyesha mambo yoote yanayofanikishwa na serikali ya CCM huenezwa sana kwa slogani ya CCM siyo ile ya Taifa la Tanzania. Angalia Sherehe za uhuru, muungano na dhifa nyinginezo za kitaifa. hakuna hata sehemu moja ya hizo dhifa tuliposikia angalau kwa uchache kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani akipewa nafasi ya kuongea mawili matatu!!! [ this is a weakness!! of Governing party!].
  MIFANO MIWILI YA USTAARABU WA VYAMA VYA UPINZANI:
  1. CUF walikomalia kufutwa kwa kodi ya kichwa - Baadaye Serikali ya CCM ilifuta kwa kujigamba sera zake ni nzuri na zinajali maslahi ya wananchi wa Tanzania.
  2. CDM ilikomalia Katiba mpya na kuiweka ktk sera zake - CCM hawajaanza kujigamba ila nakuhakikishia katika muda muafaka wataibuka na kusema sera yao juu ya katiba ni mzuri na kwa maslahi ya watanzania!!
   
 12. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inawezekana kumtuma mpinzani kama walivyofanya USA ikiwa tu unajiamini katika utendaji wako. Kwa upande wa CCM na wenye magamba wake, suala hili haliwezakani kwa vile hawana ukomavu kisiasa, na chama kinaongozwa kinafiki zaidi. Hivyo ikitokea rais amemtuma Dr. kumwakilisha basi hakutakalika kwenye vikao vya CC na NEC na ataonekana ni msaliti. Kwa CCM hata kama mpinzani ana uwezo wa kidiplomasia kuliko waliopo kwenye CCM, wao wako tayari kumtuma hata mwenyekiti wa kitongoji kuwakilisha na matokeo yake tunaona watu wengi tu wanaotuma wanaenda kulala tu wakati wote wa mazungumzo na wanaporudi huku wanakuwa kifua mbele eti wametatua mgogoro wa nchi fulani. Aibu sana Tz.
   
 13. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  kikwete amshatangaza kuwa CDM wanataka kumpindua, so hawezi kumtuma SLAA sehemu yoyote ile amuwakilishe.

  ANAMUOGOPA............. !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni matazamo tofauti uliuopo katika mataifa haya mawili
  Jk anamuona Slaa kama mpizani not wa chama tu bali hata yeye mwenyewe na kwa hali ya kawaida hawezi kumtuma demokrasia yetu ni sawa na ya Ivory coast
   
 15. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo watanzania tuaangalia na kuweka mbele maslahi ya vyama vyetu kwanza na ya Tanzania baadae, kinyume kabisa!
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  John McCain ni member wa Armed services committee wa US congress anayefanya kazi kwa masilahi ya Taifa lake, Tanzania vijisafari ni deal na ulaji yaani unataka CCM wampatie mtu wanayemchukia kukilo wote Tanzania kwa sasa ulaji?
   
 17. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Je, Kwa mienendo ya Wapinzani inawezekana wakafanya uwakilishi kwa maslahi ya nchi na si kukihalibia chama tawala?
  Je, ni kweli kama CDM, CUF au NCCR ingekuwa madarakani ingeweza kufanya hayo ya USA?
  think about it!!
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tofauti ya Tanzania na US ni kwamba wao wanajali utaifa zaidi! Hapa kwetu iwe mbunge au kiongozi wa Chama akifanya jambo utasiki ni sisi ndio tuli ibua akiamanisha chama chake! Ndio mana hata bungeni mijadadala haiendi kwa Maslahi ya Taifa inaenda kwa maslahi ya vyama! Ndio maana utakisikia Kituo cha Haki za Binadamu Kina sema Bunge hili wabunge wa Chadema wamewafunika wabunge wa CCM! Hapa hakuna utaifa ni kujionesha kwa kuvipatia sifa vyama! Ndio maana hata CCM nao huchangia bungeni kwa lengo la kuua umaarufu wa Chama,kama hoja ya kambi rasmi bungeni ili kua ni kuipinga chadema isijinafasi bungeni! Tanzania bado tupo kivyama zaidi badala ya Utaifa!
   
 19. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  KATIKA MUENDELEZO WA HOJA YANGU YA VYAMA VYA SIASA KUAMINIANA!
  Suala la Nyamongo lingeweza kupata ufumbuzi wa kudumu kama Serikali ingewatuma CHADEMA kwenda kutatua huo mgogozo kama Obama alivyomtuma MAccain kule Libya. Hapa mantinki ni rahisi sana kwamba:-
  Government is one thing and Political party is another case. Na kwamba tunaangalia nani aweza kusikilizwana jamii husika!!
  Kifupi ni kwamba Taifa letu inabidi litenganishe Serikali na Chama cha siasa kama tulivyofanikiwa kutenganisha siasa na dini.
   
Loading...