Swala la waislamu kuchinja ni la kisheria au ni ustaaarabu tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swala la waislamu kuchinja ni la kisheria au ni ustaaarabu tu?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Stevemike, Dec 25, 2011.

 1. Stevemike

  Stevemike Senior Member

  #1
  Dec 25, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika biashara ya nyama ni kawaida waislamu ndio wamepewa jukumu la kuchinja na bila muislamu kuchinja nyama hiyo ni kama hairuhusiwi kuuzwa. Hili limeleta mtafaruku hivi majuzi kati ya muuza nyama na muislamu mmoja baada ya muuza nyama kuchinja mwenyewe na huyo muislamu akataka hiyo nyama itupwe. Sasa nauliza swala la waislamu kuchinja ni la kisheria au ni ustaarabu tu? Kumbuka siko kidini. Msinielewe vibaya.
   
 2. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  acha wachinje maana hata hilo wakinyimwa wataanza kulalama maana wao kulalamika hakuishi acha tu wachinje waridhike
   
 3. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #3
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kuchanja kwa Waislaam ni ibada ! ''Mmeharamishwa (mmekatazwa!) nyamafu (kibudu) na damu (kisusio !) na nyama ya nguruwe, na kinyama kilichochinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kilichokufa kwa kusongeka koo (kunyongwa) na kilichokufa kwa kupigwa na kilichokufa kwa kuanguka, na kilichokufa kwa kupigwa pembe na alichokila mnyama, ila kama mkiwahi kukichinja kabla hakijafa. Na mmeharamishiwa (mmekatazwa) kilichochinjwa panapofanyiwa ibada isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu. Na ni haramu kutaka kutaka kujua siri kwa kuagua kwa mabao (kupiga ramli). Hayo yote ni maasia. Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi . Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema Yangu, na nimekupendeleeni Uislaam uwe dini yenu.
  ''Wanakuuliza wamehalalishiwa nini ? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlichowafunza wanyama kuwinda na ndege wa mawindo. Mnawafunza alivyokufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na muogopeni Mwenyezi Mungu; Hakika Mwenzezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu. Quran: Al Maida: 3-4.
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu hapa inaelezea kitu haramu na kisicho haramu swali je ni sheria kuchinja?
   
 5. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #5
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  unakatazwa kitu kuwa hichi usifanye na fanya hichi! Na ukikiuka wewe ni sawa na asiye amini ! Hapo unaelewaje ? Hili liko katika taratibu za mila na desturi na limekupalika na jamii. Bali ukiwa ni nyama ya biashara na ukaweka ILANI hakuna atakaekusumbua, watakuja wangine. Ni sawa na kuuza nguruwe, watanunua wanaotaka. Katika mji wa Moshi, ili kupunguza usumbufu na wateja wapate urahisi wa kuelewa Bucha za Nguruwe zilikuwa zikiandikwa kwa maandishi makubwa ' Bucha ya Wakristo !
   
 6. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #6
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Suala la waislamu kuchinja ni ustaarabu tu uliojengwa na watanzania, kumbuka serikali yetu haina dini kwa hiyo hakuna ulazima wa mwislamu kuchinja. Labda tu ieleweke kuwa kwa suala la biashara waislamu wachinje ili wenzao wa wawe na amani wanaponunua hiyo nyama
   
 7. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ondoa upupu wako hapa! Kuchinja kwa waislam ipo tangu wakati wa mkoloni, zipo bylaws ambazo ziliwekwa tangu enzi hizo, hukuliona hilo unakurupuka thread ya kibwege tu upate umaarufu! Kaulize machinjioni!
   
 8. dijly4

  dijly4 Member

  #8
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 11, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hasira ya nn bosi wangu. changia mada, huna la kusema usiropoke kwa hasira m2 wangu. au ndo tuseme huna elimu dunia, tumia basi busara ndugu. Hiyo thread ina maana sana kwa sisi wengine.
   
 9. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kuchinja kwa waislamu ni suala la ibada. Na kwa kuwa ni suala la ibada ni suala la waislamu wenyewe, yaani linawabana wao TU. Kwa asiye muislamu habanwi na sheria hiyo ktk maana kwamba asiye muislamu anaweza kujichinjia mnyama wake na kula mwenyewe na familia yake.
  Shida inakuja pale tunapokuwa tumechanganyika kati ya waislamu na wasiowaislamu. Ili kutowakosesha waislamu na sheria ya dini yao kuhusu nyama basiwasio waislamu wanawaachia wao wachinje. Kumbe ni suala zaidi linalohusu mahusiano mema kati ya waislamu na wasio waislamu: kuepuka kumuingiza muislamu ktk kuvunja sheria ya dini. Vinginevo kama mahali hakuna waislamu na kwa hiyo hakuna mtu wa kumlisha nyama 'isiyo halali' basi mtu yeyote anajichinjia kuku,mbuzi wake bila shida.
   
 10. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuna "bylaws" kuhusu waislam kuchinja? Hii mpya kwangu, itabidi nirudie homework!
   
 11. K

  Kolero JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Zilete hizo bylaws tuzione, mazoea yasikufanye uone ni sheria, unafikiri mnayama akichinjwa na Mkristo ama Muislamu atabadilisha kifo cha mnyama huyo ama nyama hiyo? acheni hizo, ishini uasilia wa Mwafrika badala ya kujigenisha katika mazingira yetu ya Kiafrika. Imani za kundi fulani zisiingilie uhuru wa watu, na wala imani ya watu fulani isihalalishe ama kukataza vionjo vya watu, na huyo Mkristo akila kilichochinjwa kwa ibada hizo atakuwa wa dini gani?
   
 12. Stevemike

  Stevemike Senior Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kumbe ktk sheria za jamhuri ya muungano wa tanzania hakuna sheria inayosema lazima muislamu ndiye achinje ndipo nyama iuzwe! Nikichinja na nikaweka ILANI kuwa hii nyama haikuchinjwa na muislamu, hakuna haja ya waislamu kunifanyia fujo buchani?
   
 13. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ilimradi umetahadharisha jamii kuwa kuwa nyama imechinjwa na mkristo wala hakuna tabu.

  Kivumbi kitatimka tu pale utaposahau kujuza umma kuwa haikuchinjwa na mwislamu halafu ukashtukiwa.
   
 14. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mkristo hachinji bali anaua ! Nimekupa aya katika post ya tatu, Mwenyezi Mungu anasema tukichinja tutaje jina lake na tumshukuru ! Kumbuka wanyama ni umma kama sisi ! Kuna nidhamu nyingi ikiwemo kisu kuwa kikali. Wengine wanaua. Tofauti ya Washirikina na Wanaoamini iko wazi !
   
 15. SONGEA

  SONGEA Senior Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuuza pork ni haramu au?
  Anachinja nani??
   
 16. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hapo hakuna tatizo kabisa ! Ndio maana kule Moshi (Kibororoni) kuepuka mtafaruku wenye bucha za Nguruwe waliandika kabisa kuwa 'Bucha za Wakristo' na walieleweka !
   
 17. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Huyo mnyama (Nguruwe) huwa hachinjwi, anauliwa ! Hana shingo ya kuchinjia, ulizia taratibu zake za kumuua.
   
 18. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  thanks
   
 19. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Ni ustaraabu wa wakristu pamoja na madhehebu mengine ila naomba ndugu zangu waislam mpitie vizuri quran na muombe roho wa MUNGU awape uelewa ili mjue kwani ndani yake kuna watu walioanishwa wanaweza kuchinja na je hao watu mi wapi?ikiwa quran inaitambua biblia kwa nini nyie msitambue ukristo?au mpagani ndie anatumia biblia?
   
 20. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Si sheria ya nchi Bali Ni ustaarabu tu uliopo katika jamii yetu mitaani nyama kuchinjwa na muislam ili watu waweze kukaribishana...
   
Loading...