Swala la uzazi linaangamiza taifa, Watoto wanafariki sana mahospitalini

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
17,034
7,590
Ninaomba serikali iingilie kati kwa umakini na utulivu mkubwa huku ikihusisha vyombo vyake vya kiuchunguzi kulibani hili, hasa chanzo ni nini na tatizo liko wapi.

Akina mama wanaenda kliniki zao saafi tu ila siku yenyewe wanaambiwa watoto wamefariki, hii imewaacha wana mama wengi wakitoa laana. Vilio vyao japo bado vinaonekana si lolote na si chochote, vimekuwa kama machozi ya samaki. Hii tunamwomba rais aingilie na asaidie kwa taasisi zote za uchunguzi, Taifa letu linaaangamia kwa kasi ya ajabu.
 
Mada yako haiko wazi vizuri, lakini kama unazungumzia suala la ujauzito mpaka uzazi salama kwa mama na mtoto hilo linafahamika na limepungua kwa kiasi kikubwa, ngoja waje watu wa data maana kuna sheria inayohusu utoaji wa data
 
Ninaomba serikali iingilie kati kwa umakini na utulivu mkubwa huku ikihusisha vyombo vyake vya kiuchunguzi kulibani hili, hasa chanzo ni nini na tatizo liko wapi.
Mkuu tulia umalizie unachotaka kukileta, inaonesha una kitu cha maana ila sijui umefurushwa ulipokuwa unaandikia hii post yako?
 
Hivi videmu vinatoa sana mimba hadi vizazi vikiolewa vinaanza kutafuta mimba kwa udi na uvumba hadi kufunuliwa kama mapazia ya guest
 
Ninaomba serikali iingilie kati kwa umakini na utulivu mkubwa huku ikihusisha vyombo vyake vya kiuchunguzi kulibani hili, hasa chanzo ni nini na tatizo liko wapi.
Umeweka kwa kificho sana,lakini swala la uzazi salama unaanzia linaanzia kwenye umasikini na elimu, hakuna huduma za afya za bure ukweli ni kwamba kuna mtu amelipa hio huduma, hivyo ni bora kwanza kuzaa watoto wachache ili uweze kujihudumia kama mwanamke na mwanaume aweze kuhudumia mke wake kilishe na kitabibu, kwani gharama za maisha ni kubwa.
 
Akina mama wanaenda kliniki zao saafi tu ila siku yenyewe wanaambiwa watoto wamefariki, hii imewaacha wana mama wengi wakitoa laana. Vilio vyao japo bado vinaonekana si lolote na si chochote, vimekuwa kama machozi ya samaki. Hii tunamwomba rais aingilie na asaidie kwa taasisi zote za uchunguzi, Taifa letu linahangamia kwa kasi ya ajabu.

Mtu mzima kuwa mmbeya ni vibaya.Taja ni wapi, hospitali ipi ilitokea lini na weka vielelezo vyote usiandike kama umebungia kiroga
 
Mtu mzima kuwa mmbeya ni vibaya.Taja ni wapi, hospitali ipi ilitokea lini na weka vielelezo vyote usiandike kama umebungia kiroga
Ndugu yangu, haina haja ya kuwa mkali kana kwamba nimemchinja mbwa mbele yako. Ukitaka mifano na uharisia mie ninayo mingi sana ambayo nikiitaja hapa siamini kama kuna mkoa ambao utabaki pasi kutajwa ama hospitali zitabaki bila kuguswa. Unatakiwa ulielewe hili katika wigo wake mpana na unyeti wake na ndo utakapotambua kwa undani maaana ya hili. Ningeweza kukutajia maeneo na bado hayataisha, kama unaona nilichokisema hapa ni uongo basi wewe mwenyewe fanya utafiti wako ndani ya wiki moja tu hasa maeneo ya mijini na hasa hapa dar alafu utarudi, na kama hulijui hili vizuri nenda kawaulize wanawake na wanaume watakujibu vizuri sana. Nakuachia mfano mmoja tu ili utomaso wako ukusaidie pa kuanzia. Nenda sinza palestina hospitality, omba idadi ya wanawake waliojifungua tarehe 13/14.4.2016 alafu waombe idadi ya watoto waliopona na waliofariki dunia. Kisha tutaendelea kujadiri, ishu hapa ni kwanini na ni nini kinatakiwa kifanyike kurudisha hari sawa.
 
Duuuh hii sasa kama ni basi ni shida
Yaani sahivi kupata mtoto kwa akina mama linaelekea kuwa kama kucheza kamari na pata potea, kidogo inakuwa na ahueni kwa wale wanaopasuliwa lakini kwa njia ya kawaida ni 50/50%. Sasa ni wangapi watakuwa na uwezo wa kugharamia upasuaji? kweli hii ndo kuwasaidia watanzania wenzetu walalahoi kweli? je, tatizo ni manesi, madaktari, vifaa hamna ama ni nini hasa?
 
Tatizo mi naona ni manesi awa wanaopelekwa kusoma diploma wakitokea kidato cha nne
 
Mtu mzima kuwa mmbeya ni vibaya.Taja ni wapi, hospitali ipi ilitokea lini na weka vielelezo vyote usiandike kama umebungia kiroga
acha siasa kwenye AFYA na UHAI kijana

wiki iliopita kuna member ameweka uzi kwa yaliyomkuta Amana, RC Mulongo akiwa Mwanza aliingilia kati mapacha waliofia tumboni sababu ya uzembe wa wauguzi

+++ Rweye wazazi hivi sasa kliniki uwe chini ya manesi na daktari mzoefu, hawa .com hawa
 
Tatizo mi naona ni manesi awa wanaopelekwa kusoma diploma wakitokea kidato cha nne
Kunaweza kuwa na ukweli mkuu. Kuna haja ya serikali kuangalia upya zoezi zima la mafunzo ya manesi kuanzia viwango vyao vya ufaulu, ubora wa vyuo na mafunzo stahiki wawapo vyuoni. Kuna tatizo mahala fulani
 
Mada yako haiko wazi vizuri, lakini kama unazungumzia suala la ujauzito mpaka uzazi salama kwa mama na mtoto hilo linafahamika na limepungua kwa kiasi kikubwa, ngoja waje watu wa data maana kuna sheria inayohusu utoaji wa data
Mkuu yawezekana walioko huko ndani wanayo ya kutwambia lakini sie huku nje yanabaki ni maswali magumu sana na hii ni kwasababu jambo lenyewe linahusisha kuchukua uhai wa watu. Swali la msingi hapa ni kwamba, wajibu wa mama ni kuhudhuria kliniki. Mama huyu anakwenda kliniki kwa miezi yote tisa, kila akienda anaambiwa kila kitu kiko sawa na mtoto anaendelea vizuri tumboni. Tatizo linakuja ile siku ya uzazi mama anatoka anaambiwa mwanae kashafariki, watoto wengine baadhi wanakaa dakika chache toka wamezaliwa nao wanafariki, tena hospitali zenyewe si zile za kutumia vibatari na tochi. Hivi vifo nani anatakiwa kuwajibika na kila siku vinaongezeka? baadae unajiuliza kuna haja gani basi ya hawa akina mama wanakwenda kliniki miezi yote wakiambiwa watoto wao wako vizuri alafu ghafla siku ya mwisho anaondolewa labour akiwa mikono kichwani? Na ukifanya utafiti kidogo, achia wale mabishoo wanaoona kinyaa kujifungua kawaida na kukimbilia upasuaji. Walio wengi wanaona bora upasuaji ili waweze kuokoa maisha yao na ya watoto wao, sasa unajiuliza imeanzaje hii kwamba kujifungua kwa kawaida linaonekana tishio la uhai kuliko upasuaji, ama kuna kampeni ya kuua makusudi katika njia ya kawaida ili wengi wakimbilie kupasuliwa ili watu wale pesa? Hili nalo linawezekana kwasababu kuna haya mambo ya fursa, siku hizi kila kitu kinaitwa fursa hata kama ni mauaji na kutoa uhai.
 
Back
Top Bottom