Swala la Ulimboka kwa TBC sio habari!?

Waziri Wa Ulinzi akizungumza ndani kipindi Maalumu leo TBC,amesema leo asubuh kituo kdg cha bunju,alienda Raia mwema 1 na kutoa taarifa kuwa wana mtu amepgwa na kujeruhiwa ambae amejitambulisha kwa jina la Dr ulimboka,Na police walipoenda kumhoji akawambia alikuwa Pub fulani karibu na Leaderz ndipo wakaja watu wa 5,wakiwa na Gari na nyeusi isiyo na Preti namba,wakampga kibao wakiwa ktk kuhamaki wakampakia kwenye Gari kuelekea njia ya mwenge.. Na hvyo ndvyo ilivyokuwa.
Source@tbc kipindi maalumu na muda si mrefu wataorudia hbr hii.

Lhrc-wao wanasema....
Kwa taarifa, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani)
na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla
wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na
shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu".

Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi. Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi,
mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...

Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili. Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya
walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'.

Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na Redio Call, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.
 
Muda mfupi uliopita nimemtaza live dr. Ulimboka on clouds tv jinsi alivyopata na mkasa huo, jamani imeendelea kuniumiza.

Maumivu yako hayafanani hata kidogo na maumivu ya wananchi wa tanzania wanaoteseka na unyama wa Dr Ulimboka na wenzake.Ulimboka umepata unachostahiki.
 
Maumivu yako hayafanani hata kidogo na maumivu ya wananchi wa tanzania wanaoteseka na unyama wa Dr Ulimboka na wenzake.Ulimboka umepata unachostahiki.

Ebu fikiria kwa mapana zaidi, yupi kati ya madaktari na serikali wanasabisha haya yote? Acha kuropoka hayo. Na usipende kuwasemea watu wengine nani kakwambia wanaumia?
 
Ulimboka alikua bar moja iko mtaa Tunisia inaitwa Kibona Bar iko mita chache kabla hujafika hospital ya moyo me nlia pale ilikua ni tahaluk kubwa mana 2lijua ni majambaz au ni askar wamemkata mtuhumiwa..gari ya ulimboka ilibaki pale mpaka asubuh me ni mkazi wa hapo kwenye iyo pub
 

--Sasa kama Nchi yetu imefikia hatua hii ya kupoteza watu na kuwapiga (Robert Ouko)

--Sasa tuna fununu na Ugomvi wa kidini huko Zanzibar, Makanisa yanachomwa hakuna anaye na Wasiwasi hata kidogo

--Sasa Mbunge wa Lindi anasimama bungeni na kukashifu Ukabila wa sehemu fulani kuwa ni wezi, wakati hawezi
kukemea Chama chake kwa Wizi wa fedha za serikali

* HAYO YOOTE NYERERE ALIYAPINGA VIBAYA AKATUNYIMA MASTAREHE KIBAO ILI TUWE PAMOJA, TULIMSEMA VIBAYA

HATUKUJUA HIZO STAREHE NDIZO ZITAKAZO TUFANYA TUWE NA MATABAKA MBALIMBALI

KWELI UONGOZI NI HEKIMA, SASA RAIS WETU ANAFANYA SAFARI ZA NJE NYINGI SIO ZA KISERIKALI KWAHIYO HAKUTANI

NA WAANDISHI WA HABARI. NAONA TUANZE KUUFAHAMISHA ULIMWENGU KABLA RWANDA IKATOKEA TANZANIA.
 
Hadithi nzuri sana..ni ushahidi wa kutosha .....lakini ulimboka mwenye hajiwezi..na hajatoa statement yoyote sasa nyie mlijuaje haya? Tena mapema na wanharakati walishafika muhimbili asubuhi mapemaaa hio stori kama ulikuwepo vile hapa juu ya hili kuna njama
njama za kuipaka matope serikali yalitokea kwa ::" yuleeee mesage sent""" hii fitina kubwa lakini ukweli utajulikana
 
Inabidi wananchi tutangaze kwamba hii TV siyo yetu tena bali ni ya ccm na watu wake kwa hiyo isitishe kuchukua kodi zetu bali wanaoitumia waihudumie kwa faida yao wenyewe kwani sisi haina faida kwetu. Bila aibu bila kufikiria wameonyesha udhaifu wa hali ya juu kiasi kwamba inaonyesha kabisa na wao wanaungana na serikali yao kuendeleza unyanysaji na udhalimu wa haki za binadamu. Tusikubali wananchi tuwakatae TBC hata vin'gamuzi vyao tuviwekee mgomo wanunue wao na serikali yao ya ccm kwa faida yao wenyewe
Hivi hawa wagonjwa wanaokufa mbona hamsemi kuna udhalilishaji au haki za binadamu ziko wapi? Mi nawashangaa sana nyie watu, wagonjwa wanakufa lakini hakuna hata anayewatetea, huyu jamaa katekwa, usiku huo huo yule mama wa mtandao kaamuka kuaza kufuatilia, hivi hao wagonjwa mbona hafuatilii kwa kasi hiyo???
 
Kuna taarifa kuwa katibu wa
Medical Association of
Tanganyika (MAT) ameanza
kupigiwa simu na watu
wasioeleweka kama
ilivyomtokea Dr. Ulimboka.
Madaktari wameshapeana
taarifa na wameahidi kumlinda
kwa gharama yoyote. Hii
inamaanisha ni vita dhahiri kati
ya wahudumu wa afya na
serikali.
Tuendelee kuona mwisho wa
sakata hili tete!
 
Hivi hawa wagonjwa wanaokufa mbona hamsemi kuna udhalilishaji au haki za binadamu ziko wapi? Mi nawashangaa sana nyie watu, wagonjwa wanakufa lakini hakuna hata anayewatetea, huyu jamaa katekwa, usiku huo huo yule mama wa mtandao kaamuka kuaza kufuatilia, hivi hao wagonjwa mbona hafuatilii kwa kasi hiyo???

acha kuongea hizi pumba zako, chanzo au kiini ni nini hasa!?
 
Current news kama hii kila media imeripoti kuhusu utekaji huu na unyama aliofanyiwa dr. Ulimboka lakini why Tbc hamjaripoti kulikoni? Kunani nyuma ya pazia?
TBC nao waliionesha kama breaking News, tena wao walienda mbali zaidi kwa kumhoji Ulimboka kabisa, hii ilikuwa taarifa ya saa mbili usiku
 
Back
Top Bottom