Swala la mipaka ya tanzania

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,526
19,381
Mwaka 1970, Tanzania (Chini ya Nyerere) tuliwahi kupigana vita fupi sana na Malawi (Chini ya Banda) kutokana na mgogoro wa mpaka, halafu mwaka 1979 tena chini ya Nyerere huyo huyo tukapigana vita ya nguvu sana na Uganda (chini ya Amin) kwa jili ya mgogoro wa mpaka. Vita nyingi hapa duniani zimekuwa zinasababishwa na migogoro ya mipaka, hivyo ulinzi wa mipaka ni mojawapo ya majukumu makubwa ya serikali.

Baada ya hapo, sijasikia tena ugomvi wa mipaka ila kila ninapoangalia ramani hizi, naona kama mipaka yetu inachakachuliwa kidogo kidogo. Kwa bahati mbaya, nchi imejikita katika mamabo ya kisisasa zaidi ya maswala ya kitaifa. Leo hii nimesoma mama Tibaijuka azungumzia swala la mgogoro kwenye mpaka baina yetu na Malawi bila kuonyesha uthabiti wa msimamo wa serikali katika swala hilo. Mpaka huo unatakiwa ufuate upite katikati ya mto Songwe na baadaye kuligawa Ziwa Nyasa katikati baina ya Tanzania na Malawi. Kutokana na kutoeleweka kwa mpaka huo na kulegea kwa serikali yetu, mpaka huo umekuwa unasogezwa upande wa Tanzania pole pole na kutokana na ramani zinavyoonyesha, sasa hivi watanzania waktumia Ziwa Nyasa wanaweza kukamatwa kwa kuingia Malawi bila kibali!. Hali inaonekana kuwa vivyo hivyo kwenye mpaka wetu pale Ziwa Tanganyika. Mipaka sahihi ya Tanzania ni kama ionekanavyo hapa chini.

attachment.php


mapofT2.jpg

Leo hii ukitafuta ramani za Tanzania kwenye mtandano, utaona kuwa zaidi ya asilimia tisini sinaonyesha mpaka wa Tanzania ukiwa unapita ukingoni mwa ziwa nyasa badala ya kuligawa Ziwa Nyasa. Na baadhi ya ramani zinaonyesha pia kuwa mipaka ya Tanzania inapitia kwenye ukongo wa Ziwa Tanganyika kama inavyoonekana katika ramani mbili za hapa chini.
attachment.php

map%20of%20Tanzania.jpg


attachment.php

map_map-of-tanzania.jpg

Kutokana na kutokueleweka vizuri mpaka sahihi baina ya Tanzania na Malawi, Google Maps wamonyesha mpaka huo kwa kutumia dotted line badala ya solid line kama invoonekana hapa chini.

attachment.php

mpaka.JPG

Ninaomba kuwe na public awareness ya umuhimu wa kutunza mipaka ya nchi yetu, na viongozi waamshwe kuitetea mipaka hiyo hata kwa nguvu za kijeshi kama alivyokuwa akifanya mwasisi wa taifa hili Mwalimu Nyerere. Ni muhimu kwa viongozi kuweka bayana kwa wachora ramani kuwa ramani zao siyo sahihi kwa vile zinapotosha mipaka ya Tanzania. Kuacha jambo hili liendelee kimya kimya kimya kutafanya mipaka sahihi ya nchi ihame kiasi kuwa vizazi vijavyo vinaweza kudhani kuwa nchi yetu haina haki na maji ya ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom