Swala la mahali katika jamii nyingi za kiafrika limegeuzwa kama sehemu ya kuchuma mtaji hii imepelekea manyanyaso kwenye ndoa

padlock

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
328
496
Wazazi wengi wamekuwa wakijiskia faraja na furaha pindi kijana wao wa kiume au wa kike anapooa au kuolewa misingi hii imeishi tangu enzi na enzi na imeambatana na mizizi ya kiroho yenye muunganiko wa mafundisho ya kidini.

Uzito wa jambo hili (NDOA) umekuwa na taswira tofauti tofauti pamoja na mapokezi tofauti tofauti ktk jamii na tamaduni mbalimbali za hapa duniani. Kuna baadhi ya jamii na tamaduni huipa uzito mkubwa tukio hili na zingine huona kama ziada
jamii za kizungu zimekuwa haziipi uzito mkubwa sana suala la ndoa kama jamii za kiafrika.

Wamechukulia tendo hili kama kitu cha ziada baada ya ukilele wa mahusiano ya uchumba na maridhiano binafsi ya watu wawili (Akili kubwa zimeelewa) sasa kwa jamii zetu za kiafrika zimefanikiwa kukipa heshima zaidi suala hili la ndoa kwa kufanya uzingativu wa taratibu, sheria natamaduni za kiafrika zinafuatwa katika jambo hili.

Tatizo kubwa huwa katika kipengele hiki kikwamishi kwa vijana wengi "MAHARI". Hili limekuwa janga kubwa sana kwa jamii nyingi za kiafrika kiasi kwamba zama hizi familia nyingi za kiafrika zimegeuza mahari kama sehemu ya kuchuma mtaji haitumiki utu, maridhiano na uwazi katika utoaji wa mahari bali kinachopangwa na kuamuliwa ndicho hiko hiko tatizo hili hupelekea watu wengi kuingia ndoani na visasi, hasira na Manung'uniko ndani ya mioyo yao.

Familia nyingi hazichukulii tendo hili la mahari kama sehemu ya kuanzisha udugu kwa familia yenye kuchumbia na urafiki wenye tija na wa muda mrefu kwa familia zote mbili bali wao huchukulia kama wajibu tu wa kutoza mahari ili wapate wanachokitaka.

Hii imepelekea vipigo viwe vingi katika ndoa, manyanyaso na kukosa uhuru katika ndoa na zaidi huzalisha mentality ya utumwa ndani ya ndoa. Migogoro mingi tunasahau kuwa inaanzishwa tangu siku ya utoaji mahari hadi ndoa kiasi cha kufanya mtoaji kujiamini na kuhisi kuwa na mamlaka juu ya uhai na uwezo wa kufanya lolote juu ya mwanamke (hata kupiga au kudhuru).

Mahari nyingi za kiafrika zimeleta mateso, utumwa na sintofahamu katika ndoa ukubwa wa mahari za kiafrika nazo zimepelekea vijana wengi kutokuoa au kukwama kuzilipa na hii ni kutokana kutokuwa na tija za kiudugu na utu pamoja urafiki ndani yake.

Katika hili nadhani wenzetu waliliona mbali sana kukataa ijapokuwa si dhambi pia ( sina maana ifutwe la hasha) bali isadifu uhalisia wa wapendanao wawili katika hili.

Wazazi wa kiafrika acheni ukale katika suala hili, ndoa nyingi zinakosa ustawi kutokana na baadhi ya mizizi yake kuanzia katika hili, na wale wanaotarajia kuingia ndoani waanze kuwa macho na wazi katika hatua zote za mwanzo wa mchakato huu.
 
Back
Top Bottom