Swahiba ampa mimba mtoto wa rafikie ambaye ni denti kidato cha 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swahiba ampa mimba mtoto wa rafikie ambaye ni denti kidato cha 4

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by BornTown, Jul 19, 2010.

 1. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wana JF naombeni msaada wenu ili sheria ifuate mkondo wake:
  Hapa job kwangu nina rafiki yangu amenielezea tatizo lililo mpata kaka yake ni hivi: Kaka anabinti yake ambaye anasoma form IV lakini kwa bahati mbaya amepewa ujauzito na swahiba wake wakufa na kuzikana na pia partner wake katika mambo ya kibiashara huyo swahiba ni mtu mzima hasa maani kijana wake wa mwisho sasa anaumri wa miaka 24 na binti wa rafikie aliempa mbimba anaumri wa miaka 17 sasa huyu kaka ambaye bintie amepewa ujauzito na swahiba wake amechanganyikiwa anashindwa afanyaje na binti ametishia kujiuwa iwapo baba yake atampeleka rafikie mahakamani, mama wa binti amesema polisi laima amfikishe huyo shemeji-mkwe maana amemuharibia maisha binti yake na mke wa mtuhumiwa yuko nje kimasomo.
  Binti shule amesha fukuzwa tayari
  Sasa huyu rafiki yangu hapa job ananiomba ushauri nimeshindwa cha kumshauri naomba nilete shauri hili hapa jamvini ili mnissaidie. Asanteni wana Jamvi
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Hapa iko namna.
  Mimba si ya huyo business partner,
  ni ya konda wa daladala za mbagala tandika
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Hamna swahiba hapo, kuna bazazi tu. Maswahiba hawafanyiani ubazazi huu.
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  NO huyo partner ni mfanyabiashara wa sinza siyo kondakta ni mtu mwenye elimu yake nzuri tu na anajua umuhimu wa elimu
   
 5. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Suala la kukubali mimba hasa na vibinti ni la kuangalia mara mbili mbili. Ili mradi vipimo vya DNA vinapatikana, mjadala usubiri mtoto azaliwe na udhibitisho ufanyike kutambua baba halisi wa mtoto, hata kama huyo jamaa yake kakubali kichwa-kichwa ili yaishe. Kwa sasa mkuu aendelee kulea binti yake mpaka hapo atakapojifungua. Na hili litampa nafasi nzuri ya kutafakari na kuweza kufanya maamuzi sahihi pindi muda ukifika.
   
 6. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu lakini vipi kuhusu haki ya binti kusoma? Huyu bazazi amekubali kuwa mimba ni yake kweli na amekubali kuilea ila anaomba soo liishe lisifikishwe kwenye sheria yuko tayari kutunza mtoto na hicho ndicho kinachompa hasira baba wa binti akiangalia shwahiba wake ni mkubwa sana binti hawezi kuolewa naye, na binti anataka akijifungua muhusuka waishi wote sasa kama akifungwa ataishi na nani ndio hapo anamwambia baba yake iwapo atamshtaki mpenzi wake basi yeye atajiua... kumbuka hiki ndio kizazi chetu cha sikuhizi cha sayansi na teke linalikupiga sio kujia
   
 7. k

  kiuno Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanzania ndio maana hatuendelei, hivi bado kuna yale mambo ya kufukuzana shule kisa eti umepata mimba? mi nilidhani huo ujinga wameshaacha.ukiwa na mimba kwani hauwezi kumsikiliza mwalimu?
   
 8. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  we nawe wa wap??????///amekwambia ya bznes patna then unabsha wasema ya konda wa daladal????
  sa unabisha nini wkt bnt ashasema ivyo?????
  its happen wayaongee yaishe its just mistake,usaliti bin uzembe bt stl YANAZUNGUMZIKA
  jins ya ku handle mambo io
   
 9. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hatuendelei kwa mengi. binti yako ametiwa mimba na bazazi na bado unajiuliza ufanyeje badala ya kumfikisha bezazi huyo mbele ya Sheria? Unajua ameishawafanyia mabinti wangapi huo ubazazi wake? unajua ukimuachia kwa kisingizio eti 'kuzima soo' ( na bila shaka aina fulani ya malipo!) atawafanyia ubazazi mabinti wengine wangapi huko mbele ya safari?
  Hivi kwanza wewe ni mzazi wa aina gani ambaye huna hata hasira kwa mtu anajifanya rafiki yako lakini amekuendea kinyume na kumtia mimba binti yako anayesoma??
  Umeshindwa kumkata panga la huko nanihii kwake, basi hata kumfikisha mbele ya sheria tu unashindwa mpaka utafute ushauri kwa JF???? :mad:
   
 10. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
 11. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu usisahau na ile haki ya mapenzi! Binti ashalikoroga, akae atulie........baada ya kujifungua maisha yataendelea! Asiyefunzwa na mamaye ndio ulimwengu unamfunza hivyo mkuu!
   
 12. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Good! uko sawa mkuu, huyo binti hakubakwa yeye mwenyewe ndio kajipeleka, faida gani itapatikana huyo swahiba kama atafungwa? Acheni kuwadekeza wanawake.
   
 13. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  BinMgen hebu chukulia binti yako kafanzwa hivyo ukiwa kama mzazi mwenye uchungu na familia ama watoto wako unahangaika usiku na mchana kutafuta pesa ili wasome halafu rakiko wakufa na kuzikana anakuzunguka nyuma anamdo mwanao na ujauzito juu. Je utaendekeza wanawake!!wanapo dai haki itendeke kwa binti yake
   
 14. D

  Dina JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mmh, some 'maswahibas'! kweli beware of swahibas. Mimi nafikiri ajiulize kama aliyempa mimba bintiye asingekuwa 'swahiba' angechukua hatua gani? Manake ninachokiona hapa ni guiltness ya uswahiba tu na si kinginecho. Ajiulize tu kama mkosaji ni konda wa daladala aliyejenga mahusiano na bintiye wakati wa safari za nyumbani-shule-nyumbani, angefanyaje? Akipata jibu, arudi kwa business patna wake!
   
 15. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Asante lakini binti ni under 18yrs na huyo bazazi mzee ni above 55 anakimbilia 60yrs sasa hapa hiyo haki ya mapenzi kwa under 18 ipo kweli hapo?? Ikiwa huyo bazazi anawatoto 4 wa mwisho anamiaka 24 kwa huyo binti amabye ni chini ya miaka 18 hapo pana mapenzi ya kweli??
   
 16. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  asante Dina kwa ushauri wako ndio maana mama wa binti anataka sheria ifuate mkondo baba wa binti yuko njia panda hajui afanyaje
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  binti anatakiwa azae mtoto kisha baba ampe ultimatum..........amsaidie kulea mtoto lakini ende shule (arudie), akikataa na kuamua kuishi kinyumba na huyo patner basi mtoto akalee mwenyewe

  waswahili wanasema HURUMA HAILEI MWANA ...........lazima wazee tuwe wakali kwa watoto
   
 18. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160  Asante kwa ushairi
   
 19. Mathias

  Mathias Senior Member

  #19
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  BornTown
  Mie nadhani hapa hakuna cha uswahiba. Jamaa ameshatenda kosa na-ni kosa kumpa binti wa shule mimba hachilia mbali she is under 18. Hapa ni kumfikisha kwenye vyombo vya sheria tu, ili haki itendeke, leo amefanya kwa uyu na kesho atafanya kwa mwingine, kwa mtu mzima kama uyo anapaswa kufahamu kutembea na mtoto ambaye ana umri sawa na mtoto wake kimaadili yetu haipendezi.
  Kuhusu binti kutishia kujiua, wala hawezi kufanya hivyo, hapa ni mzazi akae chini na mtoto wake amweleze kinaba ubaga swala zima bila kuficha ficha maneno, Mie bado naamini kuwa mtu mzima kama uyo ndo alipaswa kuwa wa kwanza kukataa kuwa na mahusiano na mtoto wa shule. Sasa kama alishindwa kutambua ilo ni dhahiri kwamba hafai katika jamii, na nimchafuvi na ataendelea kuchafua akiachiwa huru.
  Mpaka hapo lilipofikia ilitakiwa ata shule aliyekuwa anasoma uyo binti walitakiwa walifikishe ilo swala Polisi, na Polisi wangemfuatilia mtuhumiwa na kumpata. Swala kama mimba si yake au niyake vipimo vipo, lakini wakati tunasubiria vipo atakuwa ndani akisubiri majibu ya vitendo vyake. Kwa ufupi ni u mwambie rafiki yako aweke uswahiba pembeni aache sheria ichukue mkondo wake.
   
 20. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Matias asante kwa usahuri, mtoto alificha maana alipogundulika shule alipewa barua ya kumwita mzazi then huyo bazazi alikwenda kama mlezi akadanganya kuwa wazazi wa binti wako nje ya nchi kikazi so yaelekea maana sinauhakika huyu bazazi akapitisha mshiko pale shule walimu wakatulia but binti akawa anatoka nyumbani asubui na uniform anajifanya anakenda shule, ss siku yasiku mama wa binti akapita shule kwenda kumchukua bintie jioni wachaasubiri mtoto hatokei si ndio akaingia kwa mwalimu kulizia binti mbona hamwoni naye amefika muda mrefu tu kabla hawajatoka ndio akapewa mkanda mzima hali ilivyokuwa, sasa mama kufika home akachukuwa madaftari ya bbinti kuangalia anamiezi miwili haja andika kitu kumuuliza kulikoni akawa kimya, baba mtu si ndio akaelezwa kachukua bakora kutandika kisawa sawa binti akasema kila kitu tangu walivyo anza na walipokuwa wanzkutania na kuwa akitoka ile asubui anachukua taxi anakwenda kushinda kwenye moja ya nyumba ya mshkaji hadi jioni ndio maana mama amemkuwa mkali anataka hii kesi iende polisi na walimu walioshikishwa nao waazibiwe.
   
Loading...