Swabat kwa wanaume na wanawake baada ya kunyoa ili kuzuia mapele

flood

Senior Member
Jul 10, 2017
118
250
Habari wanajukwaa la urembo na utanashati.

Nikianza na wanaume hasa wale ambayo tuna rangi ya mtume kutoka dubai na Beards sehemu za usoni tumekuwa na changamoto hasa tunaponyoa hizi Beards(sharubu) zetu katika swala zima la utanashati.

Baada ya muda vipele vinaanza kuwa kero na kuacha alama nyeusi pale ndevu zinapoota. Sasa basi nikiwa kama mmoja wa mkerekaji nikaamua kwenda kwa mzee mmoja wa kihindi hapa mjini nikamueleza maana kunyoa mara kwa mara kunakomaza ngozi na mm napenda kuwa na ngozi safi isiyona makovu basi akaingia dukani kwake akanipa kipande siwezi sema ni sabuni maana haina povu akaniambia tumia baada ya kushave.

Hiki kipande nimekitumia na ngozi iko super naweza kunyoa vyovyote bila kuwa na wasiwasi wa vipele tena.

Kwa wadada mnaweza kutumia mnaponyoa na kukuacha ukiwa huru.


 

flood

Senior Member
Jul 10, 2017
118
250
Kama kichwa cha habari kilivyo, kwa ujumla ndevu ni nzuri kwa wanaume ila ni karaha pale zinapoota na kurudi tena ndani ya ngozi. Mm nilikuwa mhanga maana pia ukinyoa zinaacha alama, japo Bump Patrol inasaidia ila bado hauwi huru, sasa kuna hiki kipande kimetengenezwa na dawa za asili wanatumia wenzetu wahindi kinaitwa SWABAT kinasaidia sana na nimeona ni vyema kushare.
Matumizi
Kiloweke kwa masaa matatu kwenye maji kidogo ambayo utayatumia baada ya kushave, then ukisha shave chovya kitambaa kisafi na upake, fanya hivyo mara mbili kwa siku kwa siku tatu.

Kinapatikana kwenye maduka ya wahindi wanakouza vitu vya asili
 

Bigbootylover

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
2,844
2,000
Nimeenda kuulizia kwa mhindi mmoja nikamwambia Swabat akadai haijui nikamuonesha picha akasema inaitwa Shabu kibongo bongo, kumbe ni Shabu mkuu, kama ni hiyo basi inapatikana hata masokoni huko. Shabu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom