BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Ni UHUNI tu unafanyika hapa, leo Ndugai anaruka kimanga kama vile hakuhusika katika kubariki makato husika. Nasikia makato kama haya hata ndani ya ccm yapo lakini wamewekewa MKWARA mzito wasitoe siri hadharani. Bulaya alisema hivyo kwamba alipokuwa ccm Wabunge walikuwa wakikatwa pia ili kusaidia chama.
Akiongea baada ya kuhojiwa na Takukuru mbunge wa Mlimba mh Suzan Kiwanga amesema makato ya wabunge wa Chadema yako wazi kwenye katiba ya chama na yamebarikiwa na Spika Ndugai.
Kiwanga amesema kimsingi wabunge wa kuchaguliwa hukatwa na Spika sh 530,000 kila mwezi kutoka kwenye mshahara na posho zao na kuziwakilisha kwa katibu mkuu Chadema.
Suzan amemalizia kwa kusema wabunge wote waliridhia kanuni hiyo ya mapato ndio maana hakuna mbunge aliwahi kulalamika kabla Corona haijaingia.
Source ITV habari
Maendeleo hayana vyama!