Suzan Kiwanga: Makato ya wabunge wa CHADEMA yako kikatiba na Spika Ndugai ameyabariki na hutukata sh 530,000 kila mwezi pale Bungeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,070
2,000
Akiongea baada ya kuhojiwa na Takukuru mbunge wa Mlimba mh Suzan Kiwanga amesema makato ya wabunge wa Chadema yako wazi kwenye katiba ya chama na yamebarikiwa na Spika Ndugai.

Kiwanga amesema kimsingi wabunge wa kuchaguliwa hukatwa na Spika Tsh 530,000 kila mwezi kutoka kwenye mshahara na posho zao na kuziwakilisha kwa katibu mkuu Chadema.

Suzan amemalizia kwa kusema wabunge wote waliridhia kanuni hiyo ya mapato ndio maana hakuna mbunge aliwahi kulalamika kabla Corona haijaingia.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
9,117
2,000
Bado sielewi INA maana hyo pesa wanayokatwa wabunge inakwenda kwenye akaunti maalumu za chama ama saws na akaunti zingine za chama wanazochangia na wanachama Wa kawaida?
 

Mapatokizazaa

Member
May 24, 2020
39
95
Namaanishi tusiwe wepese kutoa banz ndan ya Jicho la wengine letu tumesahau. Wao walikubali vip kutoa ilihali wanaona kuna wizi kisha waje kulalamika leo, huu n upungufu wa fikra. Ndio maana wanatutungia sheria za hovyo kabsa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom