Sure Boy(Azam):Ulikuwa tuipige Yanga goli 7

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,034
114,448
Wakati Yanga ikijiandaa kupokea kipigo kingine kwa Simba kesho,Mido wa Azam FC ametonesha kidonda kwa kuidharau Yanga.Abubak Sure Boy amenukuliwa na media akisema walikuwa waipige Yanga goli 7 ni basi tu Mungu wao mkubwa.

Yanga wa Kimataifa juzi ilikula kichapo cha mbwa mwizi cha goli 4 bila kutoka kwa Azam katika "bonanza" la Mapinduzi Cup huko Zanzibar.

Aidha mashabiki na uongozi wa Yanga umekuja na visingizio kadhaa kutokana na kupoteza mechi hiyo.Yanga wanasema mataa ya uwanja yalikuwa yanazingua. Lakini pia mashabiki wameshauri kabla ya mechi ya kesho timu ihamishie jambo bara.
 
Mimi Nakiona Kiama Kinawasubiri 4G FC hapo Kesho..... Mnyama Ana Usongo na Hawa Wazee Wa Miamala.....
 
Mimi Nakiona Kiama Kinawasubiri 4G FC hapo Kesho..... Mnyama Ana Usongo na Hawa Wazee Wa Miamala.....
Simba mechi za mabonanza zinawapa farajaaa kama mtani jembe... Yanga timu kubwa (namnukuu Juma Luizio) wachezaji wamesajiliwa kwa ajili ya mashindano yanaayojulikana na CAF period.. Huwezi kumlipa mchezaji milioni 9 kwa ajili ya mabonanza
 
Simba mechi za mabonanza zinawapa farajaaa kama mtani jembe... Yanga timu kubwa (namnukuu Juma Luizio) wachezaji wamesajiliwa kwa ajili ya mashindano yanaayojulikana na CAF period.. Huwezi kumlipa mchezaji milioni 9 kwa ajili ya mabonanza

Hili Ndiyo Tatizo La Kutafuta Visingizio Pale Unapoishiwa Mbinu na Kupoteza Mwelekeo! Hatimae Unaishia Kuumbuka.....
Unaposema Kulipwa Milioni 9, umeshajiuliza Maswali??

Hivi Pesa Anayolipwa Mshindi Wa VPL ya Msimu Mzima unadhani inaweza Kuziendesha Gharama Za Timu Kama Simba, Yanga na Azam Kwa Huo Msimu Mzima (Mwaka mmoja)??

Fahamu Kwamba Hela anayolipwa Mshindi Wa VPL haziwezi Kuendesha Gharama Za Timu Yako Ya Yanga Hata Kwa Mwezi Mmoja tu.....

Sasa Hamuachani Na VPL Mukasema VPL ni Bonanza lisilo na Maslahi na Mukakomaa Katika Mashindano Ya Kimataifa tu (Kama Munavyojiita), Badala Yake Munakomaa Na Munajisifia Kuwa Nyinyi Ni Mabingwa Wa VPL wa Kihistoria??

VPL na, Mtani Jembe na Mapinduzi Cup Yote Haya ni Mabonanza Tu Yasiyoweza Kuendesha Timu, Tofauti Yao ni Kuzidiana Hela tu......

Hebu Acheni Wivu Nyinyi Kwa Mafanikio Ya Wenzenu Wanapobeba Ushindi....

TROPHY ni TROPHY tu Haijalishi imeCost Kiasi Gani bali ni Value kwa anayekuwa Awarded......
 
nimeandaa popcorn za kutosha kushuhudia yanga atakavo tafunwa Leo na mnyama.
 
Back
Top Bottom