Sura Mbaya, jambazi aliyeitikisa Tanzania kutoka Tabora

Si wanasema serikali haiamin uchawi kumbe ni msemo tyu ila inaamini ...serikali ni raia na bila raia hakuna serikali so usemi wa serikali haiamin uchawi na maneno tyu....raia hawaamin uchawi hahahhaahha
Ukiona umeshatambua mila zawatu basi umetambua uchawi uwe umethibitisha au laaaa..unasikiliza serikali ya TANU +CCm....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
habari za watu Kama hawa hazina afya kwa jamii sababu hazina mafunzo mema Bali huhamasisha uhalifu ntakupa mfano Wa mtu Kama ELCHAPO GUZMAN wao wanamuita mungu Wa madawa ,kilicho muhamasisha kujiingiza katika masuala hayo alikiri kuwa ni pamoja na kutizama picha nyingi za kihalifu na pia kusoma historia za PABLO ESCOBAR ,Nadhani umepata jambo

Kwahiyo ukiangalia sana picha na video za mashoga kuna uwezekano siku moja ukashawikishika kuwa shoga?!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna watu wamefanya matukio ya kutisha lakini historia zao haziandikwi.

Kuna jambazi aliitikisa Tanzania alikuwa akiitwa Sura mbaya, si jina lake halisi bali lilitokana na matendo yake.

Jambazi hili lilikuwa likiishi Tabora miaka ya 1980.

Alikuwa na Uwezo wa kukupokonya chochote hata mkeo na alikuwa hakamatiki.

Najua mpo mnaojua historia ya hili jambazi karibuni mtiririke
Kiroge alitutesa sana watoto wa National na Community na mbwa wake juzi nilikua Tabora nilionana na Dada yake Amina vitumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wamefanya matukio ya kutisha lakini historia zao haziandikwi.

Kuna jambazi aliitikisa Tanzania alikuwa akiitwa Sura mbaya, si jina lake halisi bali lilitokana na matendo yake.

Jambazi hili lilikuwa likiishi Tabora miaka ya 1980.

Alikuwa na Uwezo wa kukupokonya chochote hata mkeo na alikuwa hakamatiki.

Najua mpo mnaojua historia ya hili jambazi karibuni mtiririke
Sura mbaya alikua tishio sana maeneo ya kiloleni, isevya na mwanza road ! Na maeneo ya vijiji jirani, alifika hata Mpanda na Kigoma kwa uhalifu sugu. Alikua jambazi wa kutumia silaha na pia aliweza kupigana sana. Alikua katili sana kiasi kwamba akivunja nyumba kuiba ni lazima aue ama kuacha majeruhi wengi hata kama alichotaka kapewa ! Sikumbuki vizuri aliingiaje kwenye kumi na nane za polisi lakini aliuawa na mwili wake kuletwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete mwaka 1983 kama sikosei watu wakamiminika kumuona mtu huyo hatari aliyesumbua karibu miaka kumi !

Mbali na huyo alikuwepo pia jambazi kwa jina Issa Kandege ! Alikua na mwili mdogo tuu lakini shughuli zake ni balaa ! Aliishi mitaa ya Ng'ambo na mama yake alikua mshirikina sana, ndie aliyekua anampa dawa (hirizi) asikamatwe kirahisi na polisi.

Huyu jamaa alikua anapiga kungfu kama mchina! NADRA sana kuonekana mchana lakini akionekana alikua ni mtu mwenye heshima sana na mnyenyekevu kwa kila mtu. Enzi hizo miaka ya sabini mwishoni na mwanzoni mwa themanini mitaa ya kwihara, maeneo ya chemchem, kanyenye, mlimani gongoni, isevya, kiloleni, mwanza road kote palijaa makundi ya wahalifu na ujambazi kwa hiyo raia waliogopa sana kuwataja wahalifu polisi maana siku hiyo hulali!

Issa kandege, akiitwa pia mama ndege au maza Lee aliwahi kuwatoroka police kwa speed ya ajabu kutoka mizambaraoni hadi ukuta wa uwanja wa sabasaba, kwa sasa ndio uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Akaruka ukuta, polisi wanafika ukutani hapo wanapanda duuu ! Wanamuona anapanda ukuta upande wa pili wa uwanja kama mita 700 wakachoka ya kua kafikaje kule dakika chache vile . Akaishia zake miembeni kwa mwalimu Ahmada Salum kuelekea kwa mawiti maporini.

Mji wa tabora kwa kweli enzi hizo ulikua hatari sana ! Walikuwepo wahalifu wengi sana: Bad Spencer, Mrisho Kachobox, Hamisi mambwa, Shabani Kaburu, Mohamed Lomba (Lomba Lee), Hussein Bebe, Hamad Dogo, Yasini Isinika, Kazoba. Hawa wote ni kundi la Ng'ambo na Mlimani wakijiita Black Scorpion. Chemchem, Isevya, Kiloleni, Mwanza road, Gongoni kote nako walikua na makundi yao. Makundi haya inasadikika pia yalikua yanafanya kazi na baadhi ya maaskari wasio waaminifu, kikodishiwa silaha na kutonywa wakati wa misako! Mwaka 1984 yale majambazi ya kiloleni makina Mzambia yalimuua kinyama ofisa wa JWTZ na kumkatakata vipande na kutundika kwenye miti na sare zake na cheo chake....Ndipo JWTZ ilipotuma platoon toka Milambo barracks kuzingira isevya na kiloleni ! Kilichotokea hapo sidhani kama kuna mtu alikuwepo miaka hiyo atasahau ! Matokeo yalikua miili ya majambazi 13 mortuary kitete hospital!
Hatari Sana usicheze na JWTZ...
 
Back
Top Bottom