Supu na michemsho kwenye mabaa ya Dar es salaam hazina kiwango ukilinganisha na tunazokula mikoani.

Siku moja kulikua mechi ya Simba na Yanga, tiketi zilikua zinauzwa pale buguruni sheli.
Mimi naishi mbezi mwisho, nikaona ninunue tiketi pale, niende uwanjani nikiwa na uhakika.

Baada ya kupata tiketi, na kwakua bado asbuhi ya saa tatu, nikaona nitembetembee kidogo buguruni, sababu mara nyingi napita barabarani tu.
Nilitoka nyumbani bila kupata chai, nikaingia sehemu nipate chochote, ni bar, nikaagiza Supu, aise ile Supu walisema ya ng'ombe, ila haikua na ladha ninayoijua kabisa, yaani pale nilikula mbwa Live, kiasi kikubwa cha nyama nilimtupia paka.

Na kuna siku nilimwagizia jamaa ya anunue mishikaki, kuja kula ile mishikaki, ukitafuna ina sikIka grii grii ila mitamu sana na laini, nikatema nikaachana nayo, yaani yule alikua paka Live.
 
Kweli wewe ni ''mtu wa mikoani''. Karne hii bado unasifia supu zenye mafuta mengi na harufu! Dunia ya kistaarabu walishapita huko. Vyakula la kijanja ni vile visivyo na mafuta mengi na vinatengenezwa kiutaalam kwa kuwekwa viungo kiasi ambacho harufu na ladha inakuwa nzuri sana! On serious note: Sisi huku Afrika tunapenda michemsho yenye mafuta na nyama isiive kupitiliza.
Hujitambui na hujui supu za ukweli. Unajua supu za ukweli zilivyo? Au umezoe hayo maji ya moto unayokula siku?
 
Siku moja kulikua mechi ya Simba na Yanga, tiketi zilikua zinauzwa pale buguruni sheli.
Mimi naishi mbezi mwisho, nikaona ninunue tiketi pale, niende uwanjani nikiwa na uhakika.

Baada ya kupata tiketi, na kwakua bado asbuhi ya saa tatu, nikaona nitembetembee kidogo buguruni, sababu mara nyingi napita barabarani tu.
Nilitoka nyumbani bila kupata chai, nikaingia sehemu nipate chochote, ni bar, nikaagiza Supu, aise ile Supu walisema ya ng'ombe, ila haikua na ladha ninayoijua kabisa, yaani pale nilikula mbwa Live, kiasi kikubwa cha nyama nilimtupia paka.

Na kuna siku nilimwagizia jamaa ya anunue mishikaki, kuja kula ile mishikaki, ukitafuna ina sikIka grii grii ila mitamu sana na laini, nikatema nikaachana nayo, yaani yule alikua paka Live.
Ulienda kupata supu kimboka bar mkuu?
 
Nakumbka zamani kiria bar kinondoni supu saa moja tu asubuhi iko tayari watu tupo Hapo unapiga supu na unashushia safari zako 2 mapema tu

Pr Camp walikuwa na supu nzuri pia

Hugo mwembe jini pale mchemsho wao
Ulikuwa safi

Opposite na makaburi ya kinondoni sahv breakpoint kuna jamaa alikuwa na supu safi sehemu Ilikuwa ndg Ila watu walikuwa wanajaaa

Tmk kisuma walikuwa vzr nao

Siku hizi ulipuaji tu hakuna kitu
Supu inajazwa mimaji tuuuuu

Ova
Ladha ya Mifugo ni chakula mjuba, Dar mbuzi wanakula samaki na ndizi rosti unategemea ladha gani ukutane nayo.lakini Dar akili kumkichwa michemsho mingi unawekewa ladha na kile kiungo chenye rangi nyeusi
 
Huwa nashangaa sana nikiwa kwenye ziara zangu huko jijini Dar es salaam. Utakuta supu ya ng'ombe au kuku inauzwa buku nne mpaka sika. Tena kwenye baa za kiwango kikubwa lakini ukionja unakuta hazina kiwango kabisa. Huzikii harufu ya ya supu ya kuku au ng'ombe. Supu yenyewe majimaji tu yaani haina kiwango kabisa.

Lakini mikoani huku unakuta supu ya ukweli na inavutia kabisa na ladha ya asili lakini bei nzuri kabisa na ukiwa na Hangover unainjoi vizuri kabisa

Sijui tatizo nini juu ya supu za Das laam?
Ndaza
Vibudu
Nyama mbovu
Nyama ya wanyama waliogonjeka nk
 
Huwa nashangaa sana nikiwa kwenye ziara zangu huko jijini Dar es salaam. Utakuta supu ya ng'ombe au kuku inauzwa buku nne mpaka sika. Tena kwenye baa za kiwango kikubwa lakini ukionja unakuta hazina kiwango kabisa. Huzikii harufu ya ya supu ya kuku au ng'ombe. Supu yenyewe majimaji tu yaani haina kiwango kabisa.

Lakini mikoani huku unakuta supu ya ukweli na inavutia kabisa na ladha ya asili lakini bei nzuri kabisa na ukiwa na Hangover unainjoi vizuri kabisa

Sijui tatizo nini juu ya supu za Das laam?
Umeandika kama bado una hangover!!! Ebu ongeza kwanza supu akili ikae sawa.
 
Kuna chimbo nilikuaga nagonga supu pande za buguruni supu ni mia tatu tu ila haina nyama hata moja ikabid nimuulize mana muuza nyama unamuuziga nan kila siku tunaish na supu bila kuona mfugo ?
Akaniambia yeye huwa hanunui nyamaa anaendaga buchani kuchukua gogo la kukatia nyama ndio analichemsha usiku kucha asabuh wahuni tunapata supu, tulilia kama watoto siku ile sijawah kuona wahuni wanalia namna ile
 
Kuna chimbo moja uyole pale vibar vya pale chini zinapopaki costa za hakuna kulala buku tano kuku wa kienyeji unawekewa na firigisi kuna maza bonge hivi anatumia na ndizi tatu safi kabisa, ukishindwa kuna wasomali hapo hapo uyole buku mbili jero unaweza kushinda unajamba tu
Panaitwa makasini Apo zinapopaki akuna kulala na kwa wasomali Apo ni kwa Bex stand ya yukuyu....karibu uyole
 
Back
Top Bottom