Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,806
- 59,286
Hi guys!!!
Natumaini wote mu-wazima.
Kuna habari nimesoma leo ikanisikitisha sana na ndio haswa iliyonisukuma hata kufikiria kuanzisha hii mada.
Kwa ufupi ni kwamba kuna dada wa kiKenya aneishi Sweden anashukiwa kuua watoto wake wawili mmoja wa miaka nane na mwingine minne. Uchunguzi unaendelea hivyo bado haijajulikana kwa uhakika ilikuaje haswa. Neway kutokana na maelezo ya watu waliomfahamu kwa karibu ni kwamba huyu dada alipoteza kazi yake this summer baada ya kuondoka kazini na kwenda nyumban (Kenya)i bila ruhusa kazini hivyo alivyorudi akakuta kazi sio yake tena. Akaomba msaada serikalini ili aweze kujikimu na wanae ila for whatever reason hawakumsaidia. Ikafikia hatua mpaka umeme akakatiwa kwa kushindwa kulipa bili, akajifungia ndani na wanawe na chakula chao kikawa pizza.Watoto wenyewe walikutwa wamezama kwenye ziwa near by.
Hii story nzima imenifanya nifikirie je inawezekana dada wa watu alipata depression kutokana na matatizo yake na kitendo cha kukosa msaada mpaka akafikiria kwamba ni bora wanawe wafe kuliko waishi katika hali waliyokua nayo?Inawezekana jibu likawa ndio au sio...either way mambo kama haya yanawatokea watu wengi tu.
Wengine wanachagua kujiua...kujiweka mbali na watu wengine mpaka wanachanganyikiwa...kuua familia zao (mke/mume/watoto) wakiamini kwamba wanawapunguzia uchungu/hawana namna ya kutatua matatizo yao au kushinda kinachomsumbua hivyo kuchagua kifo badala ya kuishi.
Yote hii inatokana na watu kukosa/kutojua pa kukimbilia.
Unakuta mtu amepoteza kazi ila anashindwa kutegemea ndugu/marafiki zake kwasababu wao wanamtegemea yeye...au kwasababu hawako tayari kumsaidia..au kwasababu haamini kwamba watamsaidia...woga wa kuonekana ameshindwa n.k. Kitu hicho hicho kinaweza kusababishwa na mtu kukutwa na janga ambalo hata kama halihitaji pesa m.f kubakwa/manyanyaso mtu anahitaji kushea matatizo yake na mtu mwingine ili asije akazama peke yake. Mtu anapokosa support akazama kwenye matatizo/mawazo/hofu peke yake ndipo depression inapogonga hodi na kujikaribisha yenyewe. Na inapomtawala mtu ndo unashangaa kusikia fulani kakutwa amejinyonga unabaki kujiuliza ilikuwaje mbona alikuwepo kazini jana .
Ni muhimu kila mtu akawa na mtu anaemwamini kiasi cha kutosha kumweleza pale anapokua matatizoni kwa sababu yoyote ile. Inawezekana mtu huyo asiwe na msaada unaouhitaji kwa wakati ule ila mawazo yake ukichanganya na yako yanweza kukupa solution napia kumweleza mtu anaekujali kinachokusumbua kutakupunguzia mzigo wa mawazo/maumivu kwasababu unakua na mtu mwingine sharing your worries. Yaweza kuwa rafiki au ndugu...mkubwa au mdogo kwako it doesn't matter.
Create your own support system...be someone else's support system.
Ukihisi mtu wako wa karibu ana kitu kinachomsumbua jaribu kuwa karibu nae usije baadae ukabaki kufikiria ''ningejua ningeweza kumsaidia''.
Be blessed and stay blessed.
Dada amekiri kuwaua watoto wake ila bado haijajulikana nini haswa kilimsukuma kufanya vile.