Support System...

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,694
58,766
Hi guys!!!
Natumaini wote mu-wazima.

Kuna habari nimesoma leo ikanisikitisha sana na ndio haswa iliyonisukuma hata kufikiria kuanzisha hii mada.

Kwa ufupi ni kwamba kuna dada wa kiKenya aneishi Sweden anashukiwa kuua watoto wake wawili mmoja wa miaka nane na mwingine minne. Uchunguzi unaendelea hivyo bado haijajulikana kwa uhakika ilikuaje haswa. Neway kutokana na maelezo ya watu waliomfahamu kwa karibu ni kwamba huyu dada alipoteza kazi yake this summer baada ya kuondoka kazini na kwenda nyumban (Kenya)i bila ruhusa kazini hivyo alivyorudi akakuta kazi sio yake tena. Akaomba msaada serikalini ili aweze kujikimu na wanae ila for whatever reason hawakumsaidia. Ikafikia hatua mpaka umeme akakatiwa kwa kushindwa kulipa bili, akajifungia ndani na wanawe na chakula chao kikawa pizza.Watoto wenyewe walikutwa wamezama kwenye ziwa near by.

Hii story nzima imenifanya nifikirie je inawezekana dada wa watu alipata depression kutokana na matatizo yake na kitendo cha kukosa msaada mpaka akafikiria kwamba ni bora wanawe wafe kuliko waishi katika hali waliyokua nayo?Inawezekana jibu likawa ndio au sio...either way mambo kama haya yanawatokea watu wengi tu.
Wengine wanachagua kujiua...kujiweka mbali na watu wengine mpaka wanachanganyikiwa...kuua familia zao (mke/mume/watoto) wakiamini kwamba wanawapunguzia uchungu/hawana namna ya kutatua matatizo yao au kushinda kinachomsumbua hivyo kuchagua kifo badala ya kuishi.

Yote hii inatokana na watu kukosa/kutojua pa kukimbilia.
Unakuta mtu amepoteza kazi ila anashindwa kutegemea ndugu/marafiki zake kwasababu wao wanamtegemea yeye...au kwasababu hawako tayari kumsaidia..au kwasababu haamini kwamba watamsaidia...woga wa kuonekana ameshindwa n.k. Kitu hicho hicho kinaweza kusababishwa na mtu kukutwa na janga ambalo hata kama halihitaji pesa m.f kubakwa/manyanyaso mtu anahitaji kushea matatizo yake na mtu mwingine ili asije akazama peke yake. Mtu anapokosa support akazama kwenye matatizo/mawazo/hofu peke yake ndipo depression inapogonga hodi na kujikaribisha yenyewe. Na inapomtawala mtu ndo unashangaa kusikia fulani kakutwa amejinyonga unabaki kujiuliza ilikuwaje mbona alikuwepo kazini jana .

Ni muhimu kila mtu akawa na mtu anaemwamini kiasi cha kutosha kumweleza pale anapokua matatizoni kwa sababu yoyote ile. Inawezekana mtu huyo asiwe na msaada unaouhitaji kwa wakati ule ila mawazo yake ukichanganya na yako yanweza kukupa solution napia kumweleza mtu anaekujali kinachokusumbua kutakupunguzia mzigo wa mawazo/maumivu kwasababu unakua na mtu mwingine sharing your worries. Yaweza kuwa rafiki au ndugu...mkubwa au mdogo kwako it doesn't matter.

Create your own support system...be someone else's support system.
Ukihisi mtu wako wa karibu ana kitu kinachomsumbua jaribu kuwa karibu nae usije baadae ukabaki kufikiria ''ningejua ningeweza kumsaidia''.

Be blessed and stay blessed.

Dada amekiri kuwaua watoto wake ila bado haijajulikana nini haswa kilimsukuma kufanya vile.
 
kwa tunaoishi africa lifestyle yetu ni support system kubwa

ofisini mnaongea yote,kijiweni the same....wadada wakienda saloon ndo usiseme

kwenye daladala wakati wa foleni.watu wanabwabwaja tu mambo yao.....

uswahilini,wapangaji wenzio na kadhalika......ndugu,mjomba,shangazi....

sometimes ukiishi kizungu kwa hapa africa unapata hizo risk za depression....

ingawa siwalaumu wanaoishi hivyo but nimeona saana
 
Lizzy umeongea kweli kabisa na kama alivyosema Boss, maisha ya kiafrica yanapunguza stress na namna hii kutokana na tamaduni za kuingiliana. Ukiwa unawaza chumbani kwako mara amekuja jirani umemsimulia, inasaidia. Ila Ulaya bana style ya maisha inasababisha sana stress. Ni hivi majuzi tu nikiwa kwenye nchi fulani, ilikuwa nusura dada mmoja ajiue kwa stress ndogo sana, ambayo binafsi nilijua katoka nayo Tanzania, lakini alipofika ughaibuni, siku baada ya siku ikawa inazidi kujikusanya ndani yake, na ilipokuja kulipuka ilikuwa ni balaa, shukrani kwa majirani tuliokuwa karibu, kwani hadi sasa kalazwa...
 
Hata kwa watu wanaoishi Afrika sio wote wako huru kuongelea matatizo yao. Bado ule uhuru wa kuongelea mambo ambayo ni mazito haujatutawala kisawasa kwahiyo iwe ulaya au Afrika kwa baadhi ya watu bado hatari ya kukumbwa na depression iko pale pale.
 
Lizzy umeongea kweli kabisa na kama alivyosema Boss, maisha ya kiafrica yanapunguza stress na namna hii kutokana na tamaduni za kuingiliana. Ukiwa unawaza chumbani kwako mara amekuja jirani umemsimulia, inasaidia. Ila Ulaya bana style ya maisha inasababisha sana stress. Ni hivi majuzi tu nikiwa kwenye nchi fulani, ilikuwa nusura dada mmoja ajiue kwa stress ndogo sana, ambayo binafsi nilijua katoka nayo Tanzania, lakini alipofika ughaibuni, siku baada ya siku ikawa inazidi kujikusanya ndani yake, na ilipokuja kulipuka ilikuwa ni balaa, shukrani kwa majirani tuliokuwa karibu, kwani hadi sasa kalazwa...

Tatizo sio mahali bali ni watu wanaokuzunguka.
Unaweza ukawa ulaya na ukajihisi huru zaidi katika kushea mambo yako kuliko mtu aliyeko Afrika. Ndio maana haa huyo dada pamoja na kwamba yupo ulaya mwisho wa siku amepata msaada aliohitaji.
 
Dah! nilitaka kuongea kitu kuhusu hii post lakini acha niuchune tu. eniwei mheshimiwa Tuko yupo very right.
 
Lizzy...umeongea vyema.
Hii story inaumiza sana...those poor kids didnt deserve to die...
 
Lizzy...umeongea vyema.
Hii story inaumiza sana...those poor kids didnt deserve to die...

Yeahh inasikitisha sana!!
Ngoja tusubirie kujua sababu zake...

Binafsi namuonea hata mama huruma maana kama akidhani anawasaidia hisia za hatia zitamfuata mpaka anakufa!
 
Asante kwa kutochakachua thread ...
Vipi wewe unadhani kama huyo dada aliwaua wanawe kutokana na kuchanganyikiwa nani alaumiwe?
Kwa system za maisha ya ulaya sidhani kama angeshindwa kuwakabidhi hao watoto kwa social security! Mimi nadhani ana personal issues ambazo zimempatia depression tu na akaamua kuuwa watoto kwa msukumo wa depression.
Au pia inawezekana amekosana na watu wa kwenye system na akajijua yeye yupo right hivyo ameamua kufanya hivyo ili system iwajibishwe. All in all mama yupo very wrong.
 
Nakumbuka tulipokuwa wadogo tulikuwa na majirani ambao kidogo walikuwa hawana uwezo; you can't imagine baba alikuwa akinunua gunia la sukari basi jua hata kilo kumi zinaenda kwa jirani. Yani kuomba chumvi ilikuwa si shida. But these days we are more westernized; sijawahi kuona mtu anaomba chochote kwangu wala mimi kuomba kwa mtu.

kwa tunaoishi africa lifestyle yetu ni support system kubwa

ofisini mnaongea yote,kijiweni the same....wadada wakienda saloon ndo usiseme

kwenye daladala wakati wa foleni.watu wanabwabwaja tu mambo yao.....

uswahilini,wapangaji wenzio na kadhalika......ndugu,mjomba,shangazi....

sometimes ukiishi kizungu kwa hapa africa unapata hizo risk za depression....

ingawa siwalaumu wanaoishi hivyo but nimeona saana
 
Nakumbuka tulipokuwa wadogo tulikuwa na majirani ambao kidogo walikuwa hawana uwezo; you can't imagine baba alikuwa akinunua gunia la sukari basi jua hata kilo kumi zinaenda kwa jirani. Yani kuomba chumvi ilikuwa si shida. But these days we are more westernized; sijawahi kuona mtu anaomba chochote kwangu wala mimi kuomba kwa mtu.

umeona ehh?
tena wataalamu wanasema unapowasaidia watu
kisaikolojia unajisaidia wewe mwenyewe saana,ila hatujui...
 
Kwa system za maisha ya ulaya sidhani kama angeshindwa kuwakabidhi hao watoto kwa social security! Mimi nadhani ana personal issues ambazo zimempatia depression tu na akaamua kuuwa watoto kwa msukumo wa depression.
Au pia inawezekana amekosana na watu wa kwenye system na akajijua yeye yupo right hivyo ameamua kufanya hivyo ili system iwajibishwe. All in all mama yupo very wrong.

Aliwaomba msaada wakamnyima...bila kutoa sababu.
 
Nakumbuka tulipokuwa wadogo tulikuwa na majirani ambao kidogo walikuwa hawana uwezo; you can't imagine baba alikuwa akinunua gunia la sukari basi jua hata kilo kumi zinaenda kwa jirani. Yani kuomba chumvi ilikuwa si shida. But these days we are more westernized; sijawahi kuona mtu anaomba chochote kwangu wala mimi kuomba kwa mtu.

Ugumu wa maisha nao unachangia.
Mtu ana familia yakena tayari anahangaikasana kuwawekea kitu mezani alafu na wewe uende kwake kuomba msaada ?Inakua ngumu kwa kweli.
 
Aliwaomba msaada wakamnyima...bila kutoa sababu.
Je yeye alikuwa entitled kupata huo msaada?, manaake samtaimu sisi waafrica tunafuja wenyewe kwenye haya masuala halaf tunaanza kuforce. Inaelekea huyu mama alipoteza kazi yake bila sababu zinazokubalika kisheria na halaf akalejea social kuclaim benefit. But still alikuwa na option ya kuwakabidhi hao watoto kwa social security kama yeye hakuwa na income yoyote (though sijui system ya sweden ikoje, lakini i guess system za ulaya zinafanana)
 
Ila kuna story kama hii nadhani imetokea this year pia. Kuna Mkenya huko US amemuua mkewe na watoto wawili kati ya watatu. Na majirani walikuja kugundua baada ya days na alikuwa anakaa na maiti ndani akiwa na mtoto wake huyo mmoja alobaki. Mmoja kati ya watoto alikuwa ni mwanafunzi kama nakumbuka baba yake alitoa taharifa kuwa mtoto ni mgonjwa shuleni kumbe kamuua. Na huyo baba alikuwa violent nadhani kwani social workers walikuwa wana pay visit kwenye hiyo nyumba now and then. Sasa hii ni coincidence au wenzetu wana depression sana.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom