Superdoll, s.s bakhresa group, metl, etc | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Superdoll, s.s bakhresa group, metl, etc

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Maundumula, Jul 17, 2012.

 1. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Habari wanabodi,

  Nimefanya ka uchunguzi ka haraka haraka nikagundua kuna hizi kampuni ambazo zimebobea kuajiri wageni kwenye nafasi nyeti especially za uhasibu na general administration mojawapo ni Superdoll, Bakhresa Group, Quality Group, Mohamed Enterpises etc hapa nimetaja chache. Kampuni hizi zinamilikiwa na wazalendo sasa inakuwaje wanaleta nyomi kutoka India kupiga kazi wakati vijana wapo mitaani wanakufa njaa? Bakhresa, Manji, Nassor , Dewji kwani hamna mswahili mzalendo mwenye CPA , ACCA anayeweza kuwa Financial Controller hapo hadi ukakokote wahindi kutoka India? Kama tatizo experience si muweke waswahili chini yao wajifunze halafu wakishajua mnaondoa hao wajamaa.

  Mbona hawa wenzetu wanakosa uzalendo? Kama wahindi wanaweza sana kuongoza si wahamishe na hizi biashara zao ziende huko India?

  Hivi tatizo ni nini wana bodi ni kwamba watanzania hatuwezi hizi kazi? au tuna demand pesa nyingi? au ndio uzoefu? au kasumba tu!?
   
 2. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  idara ya uhamiaji ni dhaifu.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Katika uchunguzi wako umegundua kuna wageni wangapi katika kila hiyo kampuni na kwenye nafasi zipi?
   
 4. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ni kweli, Hawa wahindi hasa Mohamedi DEWJI na bAKHERSA NI SHETANI KABISA NA WANATUMIA FEDHA KUONGA UHAMIAJI KUPATA VIBALI KUAJIRI WAARABU NA WAHINDI.metl hata magari ananunua TATA ya India na kwamba anaonekana kama balozi mzuri kwa kuwa anatoa ajira nyingi kwa wahindi wenzake na kununua mali za india.na Bakhersa yeye nafasi nzuri kuanzia supervisor na meneja ameajiri waarabu au watu wenye asili ya huko na hata mishahara ni tofauti na waafrika weusi. METL amejenga mpaka jengo la ghorofa kama nne hivi maeneo ya Kurasini na kuweka mahausi geli kwa ajili ya kuhudumia wahindi wanaofanya kazi kwenye viwanda vyake vya mafuta na wengi hawana ujuzi kabisa isipokuwa ni rushwa na kujuana kupata vibali. LAANA TUPU NA UJINGA KABISA TANZANIA KUWA SHAMBA LA BIBI.
   
 5. n

  nyandaojiloleli JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii nchi italiwa sana mpaka watu wakaelimike kwisha kazi
   
 6. Ndukidi

  Ndukidi JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 821
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Halafu waswahili wao kazi yao kununua bidhaa zao wakati jamaa wanawanyima kula... inatakiwa kugoma kununua bidhaa zao mpaka na wao wabadirike.Pia nimekutana na Wakenya na Wahindi kibao eti salesmen, hivi kweli Watanzania wamejaa kibao hawana kazo tunaleta Wakenya na wahindi kwa kazi hizo. Dawa ni sisi Watanzania kugoma kununua bidhaa zao hala tuone janja yao. Amkeni jamani , hawa walikimbia Kenya kwa sabau hiyo wanatuona wajinga sisi.
   
 7. N

  Ndikwega JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 4,499
  Likes Received: 1,917
  Trophy Points: 280
  Wadau nadhani mmesahaua kitu kimoja kuwa jamii ya watu hawa wanawacheck black people kama masokwe fulani hivi.Yaani wanadharau na ubaguzi wa rangi umewajaa sana.Binafsi siwakubali hata kidogo, kwani hata wao hawamkubali mtu mweusi, wanamuona kama uchafu fulani hivi.
   
 8. maege

  maege JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 308
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  duuu metl ndani kuna hostel uhamiji wakifika wanachukua chao wanatimka, yaan wahindi wenyewe hakuna cha profeshen wala nini hasa kwenye kiwanda chao cha maji na juice. Yaan hii nchi real inanuka.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Kuna tatizo la uaminifu pia ingawa, uvivu wa baadhi yetu na sio wote, na imani ya waajiri kwamba ni rahisi kuwadhibiti foregners kuliko locals. Wageni hawana misiba mingi ya kuhudhuria kama locals
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Dah kaka Mwanao nina mwaka wa 4 sijawahi kumisi kazini kwa sababu yeyote :happy:

  Sidhani kama ma proffessionals wa kitanzania wana tabia hizo. Umkute mtu mwenye CPA , ACCA, MBA , MSC na miaka kama 10 ya experience kweli awe mvivu mvivu anategea kuja kazini pasi na sababu ya msingi? Mimi nadhani hawa wenzetu wana lao jambo!
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280

  But what else do the employers think? Maana ukiangalia kampuni kubwa za ulaya na marekani, wao issue ni kupata qualified people na sio wala wala wetu.
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ndahani,

  Ila katika ingia ingia zangu kwenye haya maofisi yao nimegundua kitu kimoja ambacho hawa wahindi wa kutoka India na sisi tunatofautiana. Wao when Mr big boss tell them to jump they simply ask "How high" hawanaga maswali maswali wananyenyekea saana, kwao bosi kama semi mungu. I think hawa mabosi wao wana enjoy hii hali maana obedience ya hawa watu imepitiliza. Nadhani ukimpata CPA wa Tanzania yeye anaweza kuwa mkali mkali kwenye maswala kama Tax evasion au reporting of actual income . It might also be a reason , i'm just guessing.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa...ndo hapo tofauti ilipo. Halafu pass zao wamakaa nazo wenyewe au boss anawahifadhia? Ikiwemo kuwawekia sawa jamaa wa uhamiaji...kwanini usifanye kazi kama punda? Sisi hapa kwetu..tunafanya kazi kwa raha zetu bila presha za wakubwa kutaka tuchelewe kutoka na kuwahi kuingia ofisini
   
 14. mtukichwa

  mtukichwa Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mi nadhani tatizo letu wazawa ni kupenda kupiga michongo hasa mahala pa kazi. Inasemekana wadosi ukiwapa Msosi tu ni kazi kwa kwenda mbele, hivyo watu ambao washapigwa sana na jamaa zetu wameamua kuajiri wadosi.
   
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hapo noma aisee

  Bosi kuba ikikwambia "kenge wee" unajibu "kenge mwenyewe" sasa hapo patakalika? Wakati jamaa akimuona bosi anaingia ofisini kwake anasimama kumsalimie wewe huo utaratibu ulishauacha shule msingi.
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu mbona hizo kampuni hata sijawai ona wanatangaza nafasi za kazi!
  Au wanatanzazia magazeti gani??
   
 17. A

  AZIMIO Senior Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siku zote hapa jamvini vikiwekwa vitu vya ukweli,wewe ndio unakuwa wa kwanza kutetea uozo vp leo umekuja na hili?au yamekukuta?
   
 18. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Labda zinatanganzwa kwenye New Delhi Times
   
 19. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sijiongelei mimi mwenyewe naongelea vijana wetu walio wengi ambao wako mitaani tu na miaka inakatika wakati wana academic qualifications nzuri huku kazi zao zinafanywa na wageni.
   
 20. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa yako hao superdoll ndo usiseme kabisa, hawaiamini ngozi nyeusi, sehemu zote nyeti wameweka waarabu wenzao, kama pale store, sehemu za purchasing , na sehemu za kufanyia malipo, halafu wana ubadhilifu sana unaweza ajiriwa leo lakini NSSF/PPF kadi utapewa baada ya mwaka na nusu. Wana ubaguzi wa hali ya juu na pia wameishika sirikali kweli kweli kuna kipindi walikuwa wanatengeneza ma trailer ya kufanyia kampeni ya chama cha mapinduzi. Ni hatari sana hawa. Pia ni wa miliki wa Mtibwa na kagera sugar companies..............
   
Loading...