SUPA STAA wa The Mboni Show ni mmoja wa wahanga wa ajali hapa Gairo.

Status
Not open for further replies.

MPANDA Jr

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,295
157
Wadau

Nimejulishwa na watu wangu kwa ufupi kwamba yule mdada mmiliki wa kipindi cha The Mboni Show ni mmoja wa wahanga wa ajali inayohusisha basi na gari nyingine hapa Gairo. Nipo mbioni kuelekea Kituo cha Afya Gairo kupata ukamilifu wa tukio.

Mnisamehe kwa kutoa briefing kabla sijapata full news.

Call it a Head Line

================================
Habari Zaidi
================================

Muongozaji wa Filamu mahiri na aliekuwa mume wa muigizaji maarufu wa filamu Monalisa, George Tyson amefariki dunia usiku huu kutokana na ajali ya gari iliyotokea Kibaigwa akiwa njiani kurudi kwenda Dsm. Mwili wa marehemu George Tyson umefikishwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti mkoa wa Morogoro.

UPDATES
================
Wadau wa JF nimefanikiwa kujionea gari liyopata ajali namna ilivyobondeka, ni aina ya Toyota Custom (kama Noah)....

Lakini kwa Dada Mboni hakuwemo katika Gari hiyo kwani walikuwa ktk msafara wa pamoja wenye gari 3 na hiyo moja ilipasuka gurudumu la mbele na dereva akakamata brek kwa ghafla ndo ikaanguka. Pia tayari kijana mmoja ambaye ni miongon mwa watu wa Karibu wa Mboni amefariki hapahapa Hospitali Gairo.

Kwa ufupi Mboni alikuwa katika gari nyingine aina ya Land Cruiser VX... hivyo amenusurika...

Lakin muda huu Mboni na wenzake wapo hapa Gairo na wameshakabidhi gari iliyopata ajali polisi na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya rufaa Morogoro.

Nimeshindwa kupiga picha kwa sababu ya Giza umeme ulikatika na pia natumia simu kitochi.

Usiku mwema kwa wale wa EA
 
Ndug vip huko hospital umepata taarifa gani na je kuna ukweli wowote kuwa katika ajali hyo yupo na mwanalisa na vip hakuna tuliyempoteza plz tujuze ndg jf
 
Ukipata habari kamili naomba uni_mention

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mpanda jr leta up date goroko mbona hapo gengeni na kituo cha afya si zaidi ya km 2, yote kwa yote Mwenyezi amuepushie mbali!
 
UPDATES
================
Wadau wa JF nimefanikiwa kujionea gari liyopata ajali namna ilivyobondeka, ni aina ya Toyota Custom (kama Noah)....

Lakini kwa Dada Mboni hakuwemo katika Gari hiyo kwani walikuwa ktk msafara wa pamoja wenye gari 3 na hiyo moja ilipasuka gurudumu la mbele na dereva akakamata brek kwa ghafla ndo ikaanguka. Pia tayari kijana mmoja ambaye ni miongon mwa watu wa Karibu wa Mboni amefariki hapahapa Hospitali Gairo.

Kwa ufupi Mboni alikuwa katika gari nyingine aina ya Land Cruiser VX... hivyo amenusurika...

Lakin muda huu Mboni na wenzake wapo hapa Gairo na wameshakabidhi gari iliyopata ajali polisi na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya rufaa Morogoro.

Nimeshindwa kupiga picha kwa sababu ya Giza umeme ulikatika na pia natumia simu kitochi.

Usiku mwema kwa wale wa EA
 
Ahsante sna mkuu mpanda jr, nawewe usiku mwema pia, niombee kwa Mwenyezi kwani siku si nyingi ntakuja kuungana nanyi katika harakati zetu!
 
Uptodates; George Tyson kafariki dunia kwenye hiyo ajali, habari hii ni kwa mujibu walioko hospital ya moro
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom