Sungusungu Temeke ni udhalilishaji sio ulinzi

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,960
872
Nimesikitika na Jeshi la polisi linavyofanya kazi nchini. Jijini Dar wale panga road wamerudi tena kwa nguvu. Wanakata wananchi mapanga na kuwapora. Kikundi kikubwa chenye watu karibia ishirini hivi kinaendesha wizi usiku wa manane katika mitaa mingi Jijini Dar hususani wilaya ya Temeke maeneo yaliyoathirika zaidi ni Yombo Buza, Vituka, Jet Lumo, tandika, Buza sigara.

Vijana hawa wanapora mali na fedha za wananchi usiku. Sasa baada ya kadhia hii Jeshi la polisi limewataka wananchi kulinda sungusungu. Sungusungu hii kwa sasa ni kama udhalilishaji. Huwezi kumwambia mwanamama ambaye hajawahi kupitia hata mafunzo ya mgambo akalinde sungusungu na silaha ya jadi kama panga na rungu. Kwanza hawezi kukabiliana na vijana hawa waliojitoa maisha yao kwa kazi hiyo. Kwanini Jeshi la polisi lisiweke doria kuwanasa vijana hawa? Limeshindwa kazi? Si tumeambiwa hakuna ulinzi wa polisi jamii? Hii nayo ni polisi jamii ambayo mheshimiwa raisi ameikataa. Jeshi la polisi ndio mlinzi wa watu na mali zao. Leo OCD anakusanya wananchi na kuwaambia kuwa walinde. Hivi anajua madhara ya kumwambia mwanamama ashike panga ili akabiliane na vijana wa panya road?

Hakuna mwanamke atakaye kuwa na ujasiri wa kurusha rungu kwa panya road. Polisi ichukue jukumu hilo na sio kuwaachia wananchi wasio na utaalamu wa ulinzi.

Kimetengenezwa kitega uchumi tena hapo hapo kuwa asiyetaka kulinda achangie elfu 28 kwa mwezi. Hii hela ni ya kuwalipa watakao linda kwa niaba yao. Hii ni hatari sana. Huu ulinzi nani atawakagua kujua huo usiku wanalinda kweli? Kitega uchumi hiki. Kamanda wa polisi wa Temeke kuwa makini. Mahala pengi nchini sungusungu haijawahi kufanikiwa zaidi ya kuleta uonevu na migogoro isiyo na sababu. Yaani watu wamechoka na heka heka za makazini kwao anafika nyumbani saa tatu, halafu hapo hapo saa sita awe kwenye sungusungu kweli ataweza huyu? Hili hapana.
 
wewe acha kuwadharau wanawake juzi tu mwanadada amewanyang'anya majambazi smg... wanaume wa dar sijui mkoje mnashindwa kujilinda mitaani kwenu hawa watoto wadogo sana... huku mikoani tunajilinda wenyewe sasa mkitegemea polisi pekee mtasubiri saana.... polisi wako wachache mno nchi hii.. na polisi jamii aliyoikataa mhe. siyo unayoisemea wewe....

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini msiiombe CHADEMA itangaze mikutano ya USIKU huko??..mtapata ulinzi Wa kutosha!
 
wewe acha kuwadharau wanawake juzi tu mwanadada amewanyang'anya majambazi smg... wanaume wa dar sijui mkoje mnashindwa kujilinda mitaani kwenu hawa watoto wadogo sana... huku mikoani tunajilinda wenyewe sasa mkitegemea polisi pekee mtasubiri saana.... polisi wako wachache mno nchi hii.. na polisi jamii aliyoikataa mhe. siyo unayoisemea wewe....

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
Wachache mno una maanisha nini? Mbona kwenye kulinda mikutano ya kisiasa wapo wengi sana. Unapata wapi ujasiri wa kusema wapo Wachache sana? Una idadi yao kamili? Panya road hawawezi ila kuzuia mikutano ya siasa wanaweza.
 
Back
Top Bottom