Sumu yamtesa Magufuli

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
NA DUNSTAN SHEKIDELI, MOROGORO

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli wiki iliyopita akiwa mjini hapa alitoa kali ya mwaka baada ya kukataa kukalia kiti alichoandaliwa mkutanoni, hali iliyozusha minong’ono kutoka kwa watumishi wa serikali kuwa sumu inamtesa.
Katika tukio hilo lililowaacha midomo wazi

wafanyakazi wa wizara yake wa mkoani hapa na mwandishi wetu kujionea, Dk. Magufuli baada ya kugoma kukalia kiti alichoandaliwa na wenyeji wake, alichukua kiti alichoandaliwa mwenyeji wake, Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Injinia Mdee na kukikalia.
Ajabu kubwa ni kwamba kiti hicho cha

Magufuli baada ya kukikataa, hakuna kiongozi mwingine aliyekubali kukikalia na badala yake kikashushwa chini ya jukwaa na kubaki wazi hadi mwisho wa mkutano.

Mbali na kugoma kukalia kiti hicho mbele ya wafanyakazi wa idara zote za Wizara ya Ujenzi mkoani hapa waliofika katika Ukumbi wa Chuo Cha Ujenzi mjini hapa kumsikiliza, Dk. Magufuli pia hakunywa maji ya chupa yaliyokuwa meza kuu.
Kama vile hiyo haitoshi, waziri huyo pia aliandaliwa chakula

cha mchana ambapo kwa mshangao wa wengi, alikataa kula bila wafanyakazi kuelezwa sababu ya kiongozi wao kukataa mlo huo.
Minong’ono iliyoenea katika ukumbi huo ni kwamba kitendo hicho cha Magufuli kususa vitu hivyo hadharani ni hofu ya sumu hasa ikitiliwa maanani kwamba

Naibu wake, Dk. Harrison Mwakyembe amekuwa akiteseka kwa ugonjwa kipindi kirefu hadi akapelekwa India Oktoba 9 mwaka jana kwa matibabu kutokana na kile kilichodaiwa kuwa alilishwa sumu katika moja ya mikutano yake ya kikazi.
Mwandishi wetu alimfuta Waziri Magufuli kwa lengo la

kupata ufafanuzi wa kukataa kiti, maji na chakula alichoandaliwa ambapo alipotakiwa kujibu maswali hayo, aligoma kufafanua na kujibu kwa mkato:
“Samahani kijana nimechelewa sana, nina mkutano sehemu nyingine, hivyo sitakuwa na muda wa kuzungumza na wewe. Nisamehe kwa hilo.”
Katika

mkutano huo, Dk. Magufuli pamoja na mambo mengine, aliwataka watumishi hasa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuacha kula rushwa na akasema atatumia maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa nchini (Takukuru) na jeshi la polisi kuwakamata wale wote

wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro, Injinia Doroth Mtenga alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo la bosi wake kugoma kukalia kiti na kula chakula walichomuandalia naye alionekana kukwepa kuzungumzia hilo akasema:“Mimi sijui ni kwa nini amekataa na

kwamba siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na hilo.”
Afisa mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya mkutano huo aliyeomba hifandhi ya jina lake kwakuwa siyo msemaji wa Tanroads, alisema anadhani waziri amefanya hivyo kwa sababu ya mambo ya kiusalama.“Wakati tunambadilishia kiti

alisema eti ni kirefu lakini kiukweli ni kwa sababu za kiusalama … kuna kitu amehofia ndiyo maana hata chakula amekataa kula, hili ni tukio la mwaka.”
Baadaye mwandishi wetu alibaini kuwa Waziri Magufuli alikwenda hoteli aliyofikia iitwayo Nashera, ile ambayo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ‘alilizwa’ mamilioni ya shilingi na vitu kadhaa vya thamani hivi karibuni.
SUMU YAMTESA MAGUFULI - Global Publishers

 
kweli huu ni udaku.ngoja na mimi niongezee kidogo;
inasemekana baada ya magufuli kuagiza bomoabomoa huko upareni alijikuta akipatwa na ugonjwa wa figo katika mazingira ya kutatanisha.hii imemfanya awe muoga sana na mambo ya ulozi!nadhani hata huko morogoro amesita kukalia kiti kwa maelekezo ya sangoma...kazi ipo Tanzania.
 
voodoo mbele kwa mbele, mnadhani uongozi ni kuongoza bila kujikinga na kujilinda?
 
Hofu yangu mimi ni hiyo SOURCE ya habari yenyewe.
Kwahiyo ina maana kuwa huamini kwamba

a)alikuwepo kwenye mkutano,

ama una amini kuwa

b)alikalia kiti, kula chakula na kunywa maji kwenye mkutano?

Ama ni kipi kinachokufanya uulizie source hapo?Wewe unaamini mkutano haukuwepo?
 
Kwahiyo ina maana kuwa huamini kwamba

a)alikuwepo kwenye mkutano,

ama una amini kuwa

b)alikalia kiti, kula chakula na kunywa maji kwenye mkutano?

Ama ni kipi kinachokufanya uulizie source hapo?Wewe unaamini mkutano haukuwepo?

mkuu,source kuwa gazeti la UDAKU inatia shaka!
 
Vizuri kuwa makini na afya yako. Hili suala sio geni kwa magufuli. Alipokuwa wizara fulani alikuwa anagawa kwa makatibu mahsusi wake vifaa vya chai, juice au vinywaji anavyopewa ofisini kwa ajili ya sikukuu. Kwa ufupi alikuwa hali ingawa kuna wakati alikuwa anaenda kula kwenye kantini za wafanyakazi
 
Hofu yangu mimi ni hiyo SOURCE ya habari yenyewe.

nna ndugu yangu tanroads aliwahi kuniambia magufuli hatumii kinywaji au chakula chochote kilichoandaliwa na ofisi. Kuna secretary wake aliyehama naye ofisi ndio anayemwamini.
 
Huyu MuIran Rostam anasumbua sana watu..hata mzee malecela na mh ferdrick sumaye hawanywi wala kula kwenye shughuli hata za kindugu na kijamaa..watakuja na maji yao/vinywaji vyao na watatafuta kila njia ya kutotia mkono kwenye chakula kilichoandaliwa rasmi kwa ajili yao..
 
Back
Top Bottom