sumu ya ndoa ni ...

Quiet

Member
Oct 16, 2009
51
0
habari za hapa wanaukumbi , nimepata kijiproject kidogo cha kufanya utafiti wa sumu ya ndoa na nikaona nije hapa jamvini kupata vijisentensi kadhaa.

ningeomba kila post iwe na ujumbe ndani ya sentensi isiozidi mstari mmoja na kianzio kiwe, sumu ya ndoa ni ............

nikifanikiwa kupata mistari 100(i.e equvalent to 100 posts) nitakuwa nimemaliza project na kama ikizidi itakuwa ni vyema zaidi.

naomba tuwe serious na nitaonesha mfano katika post inayofuata ya muundo wa sentensi inavyohitajika kuwa.

kamilisha project hii ili iwe ni elimu kwa jamii inayopoteza mwelekeo katika maadili ya kindoa.

natanguliza shukran zangu kabisa.

ni mimi Mr. quiet
 
sumu ya ndoa ni wanandoa kutokuchunguzana tabia vyema kabla kuowana.
 
Kutoheshimiana mkiwa wenyewe au hata mbele za watu, kutomjali mwenzio, kumsimanga kila kukicha nimekufanyia hili nimekufanyia lile, kumnyima uhuru wa mambo fulani fulani ambayo hayahusiani na kumegwa au kumega nje (kwa mfano Bongo wanaume wengi hawawaruhusu wake zao kuwa na simu za mkono). Kupekuanapekuana kila dakika ili kuhakikisha hamegi au hamegwi kwa mfano kuchunguza simu zote zinazoingia na kutoka au text messages.
 
Sumu ya ndoa ...ubinafsi,mwanandoa akiwa mbinafsi atamega nje.atakuwa anaficha sana mambo yake.
 
sumu ya ndoa ni pale mwanandoa anapotaka kumcontrol mwanandoa mwenzake.
 
Sumu ta ndoa ni wanandoa kuwa na secret bank accounts ambazo wenzi wao hawazijui, hawajui fedha ngapi zimo, zinatika wapi na zinatumikaje
 
kweli hili jamvi la watu wenye akili nyingi, hizi sentensi zilivyotulia tu basi zinathibitisha hivyo. ahsanteni sana wajameni nawashkuruni sana tena sana, waliochangia na watakaochangia .

Mr. quiet
 
Sumu ya ndoa ni kuonesha dharau pamoja na kutomjali mwanandoa mwenzako..
 
Back
Top Bottom