Sumu Ndani ya Vyakula - Food Poisoning

Mr.Toyo

JF-Expert Member
Feb 9, 2007
433
117
Ni matumaini yangu kuwa mu buheri wa afya.

Nitazungumzia kuhusu sumu inayopatikana ndani ya vyakula au kwa kimombo food poisoning, Karibuni.
**********************
Neno food poisoning ni ugonjwa unaosababishwa na ulaji na unywaji wa chakula kilichochafuliwa au kuguswa na aidha sumu za bacteria au vimelea vya maradhi na kumsababishia mtu maumivu ya tumbo (tumbo kukata) kuhara, kutapika n.k. NInaposema unywaji ninamanisha vinywaji kama vile maji, maji ya matunda, maziwa n.k. Kesi nyingi za kuchafuliwa huko kwa chakula zinatokana na ulaji wa vyakula
vilivyochafuliwa na bacteria wengi wanaosababisha madhara, hata hivyo food poisoning inaweza pia kusababishwa na virusi, kemikali, mimea na samaki wenye sumu. Ni wazi kuwa, tumezungukwa na bacteria kila upande, kwa hiyo kutokea kwa baadhi ya kesi za uchafuzi wa chakula ni jambo la kawaida. Vimelea hao wanaotuzunguka wanapatikana pia kwenye chakula na wakati mwingine wanaweza kuwa wa manufaa kwetu .

images
images
images
Hata hivyo bacteria wale ambao wako katika vitu vilivyooza na mabaki ya vyakula, si wazuri kwetu. Mtu aliye kula chakula kilichochafuliwa au kugusana na vijidudu maradhi hao, huwa na dalili kuu zifuatazo: kutapika, kuhara na maumivu ya tumbo(kitaalamu hujulikana kama stomach flu). Aidha dalili hizo mara nyingi huambatana na maumivu ya misuli, homa, kutetemeka mwili na kuihisi kuchoka. Hatua ya kuhara na kutapika mtu, husaidia mwili kuondoa mada zenye sumu au athari katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula (digestive tract) na hivyo kuzizuia sumu au vijidudu maradhi hivyo kuingia katika mfumo wa damu. Vyakula vinavyotokana na wanyama, vyakula vibichi na vile vya jamii ya mboga ambavyo havioshwi, vyote vinaweza kuwa na vidudu maradhi au Germs na kuchafua chakula au kusababisha food poisoning. Vyakula hivyo ni kama vile nyama, kuku, mayai maziwa na samaki aina ya kama wadogo. Bacteria kama vile Salmonela na Listeria ni miongoni mwa vimelea vinavyopatikana katika vyakula vilivyoharibika au kuoza.

Wakati mwingine inakuwa vigumu kueleza iwapo umekumbwa na hali hiyo baada ya kula chakula kilichoharibika. Sasa iwapo mtu atakuwa na mojawapo ya dalili hizo zilizotajwa, kama vile tumbo kukatakata, ni vyema awaulize watu wengine wa familia iwapo kuna wengine walio na dalili kama hiyo na kama wamekula chakula kama hicho alichokula yeye. Na iwapo kutakuwa hakuna yeyote mwenye dalili kama yake, basi kwa kiasi kikubwa huwenda akawa amepatwa na maradhi hayo. Wakatimwingine mtu huanza kujisikia mgonjwa katika muda wa masaa machache baada ya kula chakula kilichochafuliwa na sumu za bacteria au na vimelea vya maradhi. Dalili huanza kujitokeza kuanzia muda wa saa moja hadi matatu baada ya kula chakula kisichofaa. Na wakati mwingine mtu hawezi kujisikia mgonjwa, hadi kupita siku kadhaa baadaye. Na iwapo mtu atakuwa amekula chakula chenye kiasi kidogo cha sumu au toxin, muda wake wa kuuugua utakuwa mfupi na mara moja ataanza kujisikia vizuri. Katika hali kama hiyo mtu anapoona ana dalili hizo nilizozitaja, ni vyema amuone daktari mapema kwa ajili ya matibabu. Iwapo utakwenda kwa tabibu au daktari, atakuuliza masuali mengi kama vile unajisikiaje, umeanza kuumwa lini, ulikula nini hapo kabla na je kuna mtu yoyote wa karibu yako au unaemfahamu aliye na dalili kama zako? Nk. Aidha daktari anaweza kukuandikia vipimo vya haja kubwa na ndogo ili kuona kama vijidudu hivyo maradhi ndivyo vimesababisha hali hiyo iliyokusibu. Na iwapo utaona damu ndani ya kinyesi, unashauriwa kumuona daktari mara moja pasina na kuchelewa.

Mambo mengi yanaweza kufanywa ili kuzuia vijidudi maradhi na sumu kuchafua chakula chetu. Mosi, safisha mikono yao kwa utaratibu, kabla na kila mara unapotayarishah chakula, funika kwa sashi au bandage sehemu yoyote ya yenye mchubuko au uliojikata katika mkono wako kabla ya kuanza kuandaa chakula,safisha sehemu zote utakazotumia wakati wa maandalizi ya chakula, madokidoki na sponji za kuoshea vyombo kwa kiasi kikubwa huwa nan uwezekano wa kubeba bacteria.. Kwa hivyo ni lazima zioeshwe mara kwa mara baada ya kutumia. Vyakula aina ya nyama na mayaii vinapaswa kupikwa barabara na vipoti kupashwa moto vizuri kabla yakuliwa. Hakiisha jokofu au friji lako lina nyuzi joto 40 na freeza ikiwa nyuzi 0 au chini ya hapo, kiporo cha chakula kisikae ndani ya jokofu kwa zaidi ya siku nne, usiache ovyo nyama bila ya kuihifadhi, na vyema uichemshe kwa zaidi ya nyuzi joto 140, kuwa mwangalifu wakati wa kuhifadhi vyakula kama vile samaki, nyama mbichi na mayai, hivyo vyote vinaweza kuchafuliwa na bacteria wa maradhi. Usivue samaki kutoka kwenye maji yaliyochafuka, safisha mboga mbichi na matunda kabla ya kula au kupika, unanunua vyakula vinavyouzwa ndani ya makopo, mikebe n.k unapaswa kwanza kuangalia muda wa matumizi yake unakwisha lini, usile uyoga wa mwituni, ambao haujaidhinishwa na mtaalamu kuwa ni salama kwa mwanadamu na mwisho hakikisha kuwa bidhaa zote zinazotokana na maziwa ambazo nyingi huuzwa madukani ni lazima ziwe zimeondolewa vijidudu hasa bacteria kwa njia ya kitaalamu ijulikanayo kama pasteurization. Maziwa ya ng'ombe ambayo hayajapitia katika njia hiyo ya pasteurization, yanapaswa kuchemshwa vizuri kabla ya kutumia.. Itakumbukwa kuwa watoto, wazee na wale wote wenye magonjwa ya muda mrefu au wenye kinga ya dhaifu ya mwili huwa na hali mbaya wakati wakila chakula kilichoharibika au kuchafuliwa na vimelea vya maradhi. Kwa hiyo ili kukabiliana na tatizo hili, watu wazima wanapaswa kubeba jukumu kuu la kuepukana na suala hilo na vile vile kuwaelekeza watoto pia nini cha kufanya.
*********************
 
Back
Top Bottom