Sumu na huduma ya kwanza kwa mbwa aliepewa sumu

theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,750
15,636
SUMU NA HUDUMA YA KWANZA KWA MBWA ALIEPEWA SUMU

★ UTANGULIZI

Sumu ni kitu chochote hatarishi katika mwili wa mnyama na binadamu vilevile.

Kwa kawaida mbwa huwa wanatabia ya udadisi na udadisi wao huo huwafanya kukutana na mazingira tofoutitofouti ambapo pia yanaweza kuwa hatarishi kwa maisha yao mfano wa mazingira hayo ni kama vile vichakaa au katika stoo za kuhifadhia malighafi mbalimbali.

Udadisi huo huwafanya kukutana na wadudu na wanyama hatari wenye sumu kama vile nyoka na tandu na pia katika udadisi wao huo wanaweza kukutana na chambo (mtego wa sumu).

★ Vitu vya kuzingatia katika kutoa huduma ya kwanza kwa mbwa aliekula au kulishwa sumu

✓ Kama mbwa wako amekula kitu ambacho kitakutatiza kama ni sumu ama sio sumu ni vyema ukachukua container husika uende sehemu ambayo imeandikwa ingridient ainisha kitu kimoja baada ya kingine na iwapo umeshindwa kuelewa kitu mmoja wapo ni vyema ukampigia simu Veterinary Doctor kwa msaada zaidi ili akueleze ni namna gani ya kuondoa sumu hiyo.

✓ Kama dalili za sumu zinazidi kuonekana ni vyema ukamuwaisha mbwa kwa Veterinary clinic yoyote iliyokaribu na wewe kwa msaada zaidi na ni vyema ukabeba container husika la sumu hii mara nyingi hurahisisha kazi na hupelekea mbwa wako kupewa huduma mapema zaidi.

✓ Huwa inashauriwa kumfanya mbwa atapike ili kupunguza kiwango cha sumu ndani ya tumbo lake kabla ya kumpeleka kwa daktari na mara nyingi daktari hutoa ushauri huo

✓ Kwa mfano mbwa kala sumu masaa mawili yaliyopita na itakuchukua wewe muda wa kama nusu saa kumfikia daktari kwa msaada zaidi ni vyema ukamlazimisha mbwa kutapika (First aid) ili kupunguza kiwango cha sumu ndani ya tumbo lake

★ Usimlazimishe mbwa kutapika iwapo;

✓ Kama mbwa alikwishatapika hapo mwanzo

✓ Anapumua kwa shida, anaonesha dalilli za kuishiwa fahamu na pia kutokuwa na hisia za aina yoyote

✓ Kama mbwa anaonesha dalili zozote za msukosuko na pia kama anataka kuzirai

✓ Kama mbwa kala sumu aina ya acid, alkali, mafuta ya taa au petroli na pia dawa za kufanyia usafi ndani ya nyumba

✓ Kama mbwa kala kitu cha ncha kali ambacho kimekwama kwenye mfumo wa chakula ambapo chaweza leta madhara katika kuta zake

✓ Kama container iliyobeba sumu imeandikwa " Do not induce vomiting "

★ Namna ya kumfanya mbwa wako kutapika kama njia ya huduma ya kwanza

✓ Mpe mbwa wako 3% Hydrogen peroxide katika dose ya 5ml ( kijiko kimoja cha chai ) kwa mbwa mwenye uzito wa 4.5-5kg rudia kila baada ya dakika 15- 20 mara tatu mpaka pale mbwa atakapoanza kutapika.

✓ Unaweza mpa chumvi vijiko vya chai vitatu kupitia mdomo wake pia yaweza kumfanya mbwa kutapika

✓ Unaweza mpa mbwa wako pia syrup ya ipeac ambapo ilikuwa inatumika hapo mwanzo kbla hydrogen peroxide haijaja na ufanyaji kazi wake ni 50% lakni pia yweza kuwa hatari kwa mbwa wako usiitumie kabla hujaruhusiwa na daktari na dose yake ni 0.5-1ml kwa mbwa wa uzito wa 4.5-5kg rudia mara moja tu baada ya dakika 20

✓ Baada ya sumu kuondolewa tumboni mpe activated charcoal ili kukamata kiwango cha sumu kilichobakia tumboni na pia kuzuia unyonyaji zaidi wa sumu katika mfumo wa chakula.
-- Mara nyingi huja kwa mfumo wa kidonge cha 5 grams na dose inayohitajika ni kidonge kimoja kwa mbwa wa 4.5 - 5kg
-- Na pia yaweza kuja kwa mfumo wa powder au maji ambapo husumbua sana kumnyweesha mbwa incase umekosa vitu kama sindano au chupa maalamu ya kumyweeshea mbwa

✓ Kama umekosa activated charcoal ni vyema ukampa mbwa mchanganyo wa maziwa ( 60ml) na ute wa yai ule mweupe ( 60ml) kwa mbwa wa uzito 4.5 -5kg kwa kutumia syringe maalamu yenye gauge kubwa

✓ Then baada ya hapo mpeleke mbwa wako kwa Veterinary Docror kwa msaada na matibabu zaidi maana kuna vitu mbwa wako itabidi apewe ili kuweza kurudia katika hali yake ya kawaida

★ Baadhi ya sumu hatari kwa mbwa wako

✓ Drug poisoning mara nyingi wamiliki wa mbwa huwapa mbwa wao dawa zinazotumiwa na binadamu mbwa wao hii kisheria hairuhusiwi na mara nyingi yaweza kuleta madhara kwa mbwa mfano wa dawa za kupunguza maumivu kama vile Ibuprofen ( advil) na pia acetominophen yaweza kuwa sumu kwa mbwa wako pia dawa kama vitamin, sleeping pills na heart pills

✓ Antifreeze agent kama vile ethylene glycol huwa ni tamu na huwavutia sana mbwa

✓ Dawa za kutegea wanyama waharibifu kama vile strychnine, sodium fluorate, phosphorus, zinc phosphide na metaldehyde hutumika kuua na kuzuia wanyama pori huko vijijini

✓ Dawa za kuzuia wadudu (insecticides) kama vile organophosphate, organochlorde, pyrethrin, pyrethroids na carbamate

✓ Sumu za chakula ( food poisoning) kama vile chocolates, vitunguu, tangawizi, zabibu, macadania nuts na pia xylitol hii hutumiwa sana na watu wenye kisukari

✓ Mimea ya sumu pamoja na bidhaa za mafuta kama vile mafuta ya taa, petrol na tuperntine

✓ Sumu za panya na Contact poisoning

Imeandaliwa na C.E.O
JM Veterinary Centre ( JMVC)

Phone: +255712784472

Motto: We save You and your animal as family

Karibu tukuhudumie
 
Kuna Dr nilimuita kwangu akamchoma shindano 4ml mbwa Wa miezi 3 daaa ya minyoo aina ya kepro
Yule mbwa alikuwa kama kapata kizunguzungu kesho yake akawa Hata kusimama hawezi .nikampigia Dr akasema alikuwa na minyoo sana akaja akamchoma tena dawa limoxn -100 ml4 yule mbwa alizidiwa sana akafa
Mbwa alikuwa mzima kabla ya matibabu .Dr hakurudi na hakupiga simu kuulizia hali na Mimi sijampigia hadi Leo maana nilimpenda sana mbwa Wangu
 
Halafu huyo Dr anasema dawa ya minyoo kepro Hata binadamu unaweza akatumia kwa kuweka kiasi kidogo ni kweli?
 
Kuna Dr nilimuita kwangu akamchoma shindano 4ml mbwa Wa miezi 3 daaa ya minyoo aina ya kepro
Yule mbwa alikuwa kama kapata kizunguzungu kesho yake akawa Hata kusimama hawezi .nikampigia Dr akasema alikuwa na minyoo sana akaja akamchoma tena dawa limoxn -100 ml4 yule mbwa alizidiwa sana akafa
Mbwa alikuwa mzima kabla ya matibabu .Dr hakurudi na hakupiga simu kuulizia hali na Mimi sijampigia hadi Leo maana nilimpenda sana mbwa Wangu
Sorry mkuu mbwa wako alikuwa ana umri gani?.....

Halafu labda nikueleweshe kidogo mkuu sio kila mtu ni daktari...(vets) ni wachache sana hapa nchini....

Kwa maelezo yako naona wazi huyo jamaa anayejiita daktari hakuwa na uhakika ni kitu gani anatibu hivyo alikuwa anafanya blind treatment.... ndio maana ukampoteza mlinzi wako....

Hivyo basi ni vyema ukawa na kawaida ya kuwa consult pure Veterinary doctor na sio hao vishoka wanaochukua majukumu ya vet....
 
Mkuu yote hayo c anakufa kutokana upatikanaji wa huduma
Dawa ni maziwa na mafuta ya nguruwe tuu anapona
Hayo yatapunguza kiwango cha sumu na sio kuimaliza hivyo ukitaka kuondoa sumu mwilini ni vyema akapata huduma stahiki mkuu....
 
Kuna Dr nilimuita kwangu akamchoma shindano 4ml mbwa Wa miezi 3 daaa ya minyoo aina ya kepro
Yule mbwa alikuwa kama kapata kizunguzungu kesho yake akawa Hata kusimama hawezi .nikampigia Dr akasema alikuwa na minyoo sana akaja akamchoma tena dawa limoxn -100 ml4 yule mbwa alizidiwa sana akafa
Mbwa alikuwa mzima kabla ya matibabu .Dr hakurudi na hakupiga simu kuulizia hali na Mimi sijampigia hadi Leo maana nilimpenda sana mbwa Wangu
Pole sana chief
 
MAELEZO MUHIMU KUHUSIANA NA LISHE KWA MBWA NA NAMNA YA KUANDAA CHAKULA CHA MBWA

★ Utangulizi

Lishe/chakula/mlo kamili kwa mbwa ni muhimu sana kwani humpa mbwa afya nzuri na pia huwakinga mbwa na mashambulizi mbalimbali ya magonjwa na hivyo kuwafanya wavutie muda wote

Kwa sasa vyakula vingi vya mbwa hupatikana madukani kutoka viwandani maana vimefanyiwa utafiti na kuzingatia afya ya mlaji ambaye ni mbwa na wanasayansi wameenda mbali zaidi wameweza kutengeneza chakula kutegemea aina ya breed ya mbwa

Lakini hayo yote hayakuzuii wewe mmliki wa mbwa kujitengenezea chakula mwenyewe ambacho kitakuwa kimekidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa mbwa ili kuepuka gharama ya chakula kwa namna moja ama nyingine kama nitakavyoelezea hapa chini

★ Umuhimu wa maji kwa mbwa

✓ Vyakula vyote hata vile ambavyo hukaushwa na hewa maalamu kiwandani huwa na kiwango kidogo cha maji, ingawa mbwa anaweza jipatia maji kwa njia ya kunywa lakni kiwango kingine cha maji kinatokana na chakula

✓ Mbwa anaweza kukaa muda mwingi bila kula chakula ( Hunger tolerance) lakni hawezi kukaa muda mrefu bila kunywa maji kwa maana hiyo mbwa asipokula chakula hutumia mafuta na baadhi ya nyama za mwili kama mbadala wa kupata nishati ya nguvu lakni akipoteza moja ya kumi ya maji yake mwilini mbwa hupoteza maisha

✓ Bila maji ya kutosha mbwa hatoweza kumeng'enya chakula chake na hata kama akifanikiwa kwa hilo chakula hakitoweza kunyonywa vizuri katika mfumo wa chakula hivyo anahitaji maji muda wote na unywaji wa maji hutegemea na mazingira na wingi wa chakula

★ Sifa za mlo kamili wa mbwa

✓ Chakula cha mbwa kinatakiwa kuwa na ladha na harufu ya kuvutia

✓ Chakula kikidhi kiwango cha nguvu (wanga) kinachohitajiwa na mbwa

✓ Chakula kiwe na kiwango cha protini cha kutosha kuwezesha ukuaji wa mbwa na kumkinga na magonjwa

✓ Chakula kiwe na kiwango cha madini na vitamini cha kutosha

Zingatia: Mbwa ni jamii ya wanyama wanaokula nyama (carnivores) lakni tukija katika suala la mchanganyo wa chakula ulio kamili ni lazma uwe na protini, wanga, vitamini na madini na hata mbwa mwitu wanapowinda mbugani mara nyingi wanawinda jamii ya wanyama wanaokula majani na wakifajikisha kumuua hula kitu ukijumuisha matumbo ambayo huwa na majani yaliyomeng'enywa na mifupa yote hivyo kuwawezesha kupata madini na vitamini kwa njia hiyo hivyo basi kwa mbwa wanaofungiwa ndani ni lazma wapate mlo kamili kama nitakavyoelezea hapa chini

★ Vyakula vinavyotakiwa na mbwa na jinsi ya kuandaa vyakula hivyo

a) Nyama

Nyama ndio chanzo kikubwa cha protini kwa mbwa na katika mchanganyo inatakiwa kuwa zaidi ya 50%. Nyama hii yafaa ichemshwe kwanza ingawa mbwa wanapendelea nyama mbichi lakni kwa hili lazma ichemshwe na baada ya hapo ndio inatakiwa kuchanganywa na vyakula vingine

Kama nyama ina mifupa ni vyema mifupa ikaondolewa hasahasa kama nyama ni ya mbuzi/kondoo au kuku maana mifupa yao huwa ni midogo na hivyo inaweza kuleta shida katika mfumo wa chakula wa mbwa baada ya kuondolewa mifupa inatakiwa kuchemshwa pekee hadi pale itakapotoa supu ambayo itatumiwa kuchanganywa na vyakula vingine

b) Maziwa na Mayai

Maziwa na mayai hutumiwa kama mbadala wa nyama pale nyama inapokosekana hapa unatakiwa kuchukua maziwa kiasi cha lita 1.8 yachemshe yaache yapoe kisha changaya na mayai mawili yaliochemshwa vizuri then malizia kwa kuchanganya na vyakula vingine

c) Wali

Wali hutumika kama chanzo cha wanga na mchele unaotakiwa hapa ni ule unpolished (mchele mchafu) maana huwa na virutubisho vingi zaidi tofouti na ule Polished (mchele safi) na unaadaliwa kwa kuchemsha na maji kutengeneza bokoboko ambalo huchanganywa na vyakula vingine

d) Unga wa ngano

Unga wa ngano hutumika kama mbadala wa mchele endapo utakosekana hapa unatakiwa kuuchanganya kutengeneza uji mzito ambao utatumiwa kuukaanga kutengeneza chapati au pancakes ambazo utazikatakata na kuchanganya na vyakula vingine

e) Uji

Uji pia hutumika kama mbadala wa mchele na uji unatakiwa hapa ni ule ambao umetengenezwa na unga wa mahindi ambao haujakobolewa unauacha upoe kisha changanya na vyakula vingine. Mbwa wanaupenda sana uji huu.

f) Mbogamboga

Ingawa mbwa hawapendi mbogamboga lakni ni muhimu kuwemo kwenye mchanganyo maana ndio chanzo cha vitamini na madini mbalimbali mboga kama sukumawiki, chinese ni nzuri lakni ukikosa hizo unaweza chemsha carrot au beetroots na ukachanganya kwenye vyakula vingine na ikumbukwe kuwa kiwango cha mboga kitengeneze 1% ya mchanganyo wote

★ Vitu vya kuzingatia katika ulishaji wa mbwa

✓ Kwa kawaida tumbo la mbwa ni kubwa kulinganisha na viungo vingine vya mfumo wa chakula hivyo anatakiwa kula ambacho kitaweza kukaa mwilini kwa muda mrefu na kwa kawaida mbwa anayakiwa kula mara moja kwa siku ingawa watu wengine huwalisha mara mbili ambapo hutenga chakula kama chakula cha kawaida (light diet) au chakula cha kutosha (heavy diet)

✓ wali kidogo na mbogamboga huandaliwa kivyake baada ya hapo huchanganywa na supu na nyama kidogo na hii tunaita light diet na chakula kamili huwa na nyama,mbogamboga,wali au chapatti na vyote hivi huchanganywa na supu ya mifupa

✓ Na mbwa aina ya chakula kutegemea na majukumu yake yako muda gani ' Kama mbwa analinda usiku basi asubuhi anatakiwa kula heavy diet na jioni masaa machache kabla ya kuingia lindoni anatakiwa kula light diet na kama mbwa anaingia lindoni mchana basi jioni anatakiwa kula heavy diet na asubuhi kabla ya kuingia lindoni ale light diet

✓ Chakula cha mbwa kinatakiwa kuandaliwa muda kidogo kabla ya mbwa kula na kama chakula kikibakizwa na mbwa hatakiwi kulazimishwa kula na chakula hicho kiondolewe ndani ya dakika 10-15

✓ Vyombo vya chakula na maji vinatakiwa kuwa safi na salama muda wote na hakikisha maji hayaishi ndani ya chombo cha maji na kinatakiwa kuwa karibu na bakuli la chakula muda wote

✓ Mbwa wasipewe vyakula vya sukari au chumvi maana vyakula hivyo huwapunguzia umri wa kuishi na pia huwasababishia magonjwa mbalimbali ya ngozi

✓ Muda na mahali pa kulia chakula uwe/pawe sehemu moja hakuna haja ya kubadili ratiba ya chakula kama ni asubuhi ya saa 11 na jioni ya saa2 iwe hivyo muda wote hakuna haja ya kubadili ratiba ya chakula

✓ Kwa siku mbwa anatakiwa kuwa gm 350 za chakula na mara moja unaruhusiwa kumpa mbwa maji yaliyochanganywa na glucose na iwe kila siku

Mr Miller Marire inawahusu hii
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom