Sumu aliyolishwa Mwakyembe amesambaza hadi kwa Mkewe!

Hii sio kale kasumu ketu ambako unaweza kujikinga kwa kuvaa plastiki/raba sehemu husika?
 
Sitta matatani
Friday, 17 February 2012 21:42
0diggsdigg

Festo Polea
Mwananchi

WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameingia matatani baada ya Jeshi la Polisi nchini kutolea tamko ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na kueleza kuwa hautokani na kulishwa sumu, huku likisema limefungua jalada kwa ajili ya uchunguzi wa kauli yake hiyo.

Tamko hilo la polisi lililotolewa jana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. DCI Manumba aliwataka watu kuupuza madai hayo akieleza kuwa ushahidi uliopatikana kutoka nchini India alikolazwa Dk Mwakyembe hauonyeshi kuwa alilishwa sumu. Manumba alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wake kuhusu hali na mwenendo wa uhalifu nchini katika kipindi cha mwaka jana.

Akifafanua kuhusu kauli hiyo ya Waziri Sitta, DCI Manumba alisema, "Jeshi la Polisi limekaa kimya muda mrefu likifanyia uchunguzi kauli hiyo kwa kuwa maneno hayo ndani yake yanaonyesha jinai." Aliendelea "Kazi ya Jeshi la Polisi ni kuchunguza makosa na si kufuatilia nani anaumwa ugonjwa gani. Nani anaumwa nini ni jukumu la madaktari. Lakini tumekuwa kimya muda mrefu tukichunguza tuhuma hizo nzito.'' DCI Manumba aliendelea kufafanua "Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India.

Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu katika maradhi yanayomsibu Mwakyembe.'' Manumba aliongeza kuwa kwa kuwa suala hilo ni la kisheria na kiupelelezi, Jeshi la Polisi linaandaa jalada la upelelezi kuhusu kauli hiyo ya Waziri Sitta na likikamilika, litapelekwa kwa DPP kwa ajili ya uamuzi.

"Hata hivyo, Sitta mwenyewe nilimsikia katika kauli yake akisema kuwa naye ameisikia katika vyombo vya dola, hivyo tunaandaa jalada la upelelezi na likikamilika litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa uamuazi wa kisheria wa nani ashtakiwe au nani ana makosa. Lakini sasa ni hayo kuhusu kauli hiyo Waziri Sitta ninayoweza kusema,'' alisema Manumba.

Awali Manumba alisema kabla Dk Mwakyembe hajaanza kuumwa na kukimbizwa India kwa matibabu, Jeshi la Polisi lilipokea maandishi kutoka kwa waziri huyo yaliyodai kuwa alikuwa akitishiwa uhai wake, lakini likiwa katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wake, akaanza kuugua na kukimbizwa India kwa matibabu.

"Jeshi la Polisi liliwahi kupata maandishi kutoka kwa Mwakyembe kuwa anatishiwa uhai wake, lakini tukiwa katika hatua za mwisho za uchunguzi, Mwakyembe akaanza kuumwa,'' alisema Manumba. Historia ya ugonjwa wa Mwakyembe Dk Mwakymbe alianza kuumwa Oktoba 9 mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa katika Hospitali ya Apollo kwa matatibu. Alirejea nchini Desemba 11, mwaka jana baada ya kulazwa hospitalini humo kwa takribani miezi miwili.

Msemaji wa familia ya Dk Mwekyembe na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema mara baada ya mbunge huyo wa Kyela kurudi nchini kuwa, afya yake ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

Kauli za Waziri Sitta Mara kadhaa Waziri Sitta amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa ugonjwa wa Dk Mwakyembe, umetokana na kulishwa sumu. Akiwa kwenye uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Jijini Dar es Salaam Januari 28 mwaka huu, Sitta alisema:

" Nasema Dk Mwakyembe kapewa sumu, kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka," alisisitiza Waziri Sitta katika hafla hiyo.


Sitta alihoji " Ni vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia, lakini baada ya saa moja unarudia tena, kitu hicho si cha kawaida." Sitta alisema wamejaribu wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote.

Waziri Nahodha
Akijibu moja ya kauli hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nohodha alimtaka Waziri Sitta awasilishe ushahidi wake ili ufanyiwe kazi badala ya kuzungumza nje ya vyombo vya sharia. Hata hivyo, Sitta alisema hatapeleka ushahidi wa madai aliyotoa kuwa Dk Mwakyembe alilishwa sumu kwa kuwa polisi tayari wanao ushahidi.

Alisema wanachotakiwa kufanya Polisi ni kufanya uchunguzi kuhusu madai hayo ya Dk Mwakyembe kulishwa sumu kwa kuwa ushahidi wanao na wasianze kurushiana mpira.
"Waziri Nahodha anataka ushahidi gani ikiwa taarifa za madaktari zinazomhusu Dk Mwakyembe kuhusu sumu aliyopewa zilishapelekwa polisi, anataka mimi nitoe ushahidi gani," alisema Waziri Sitta.

Kuhusu mwenendo wa uhalifu nchini kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana 2010, Manumba alisema kulikuwa na matishio mbalimbali ya usalama ikiwamo ugaidi, uharamia baharini, wahamiaji haramu na biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Manumba alitaja matishio mengine yaliyojitokeza mwaka huo kuwa ni uingizwaji bidhaa bandia na silaha haramu, dawa za kulevya, migogoro ya kisiasa, kidini, migogoro ya wanafunzi wa taasisi na vyuo vya elimu ya juu na migogoro na migomo ya wafanyakazi.

Taarifa za ukweli kuhusu ugonjwa wa Mwaki zina kifafa. I'm confused.
:A S-confused1:
 
hivi kuna siku na mahali mwakyembe mwenyewe ametamka kwamba kalishwa sumu?napenda kujua ili nitafakari vema hili suala lenye utata mkubwa
 
Kinachotokea hapa mwakyembe mwenyewe anaogopa kusema kinachomsibu manake anajua kitakachofuata ni kuvurugana ndani ya chama na serikali yake.Naona kaamua afe kimya kimya na gonjwa linalomsumbua.Pole ndo uwanaume huo kuficha kwa sababu ya fadhila ya serikali au manake hatukuelewi taarifa ya polisi huna imani nayo.Basi funguka basi kilichoko moyoni mwake umalize mchezo kama sio tamthilia
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom