Sumu aliyolishwa Mwakyembe amesambaza hadi kwa Mkewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumu aliyolishwa Mwakyembe amesambaza hadi kwa Mkewe!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwamakula, Feb 18, 2012.

 1. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Taarifa kutoka kwenye familia zinaonyesha kuwa dalili za sumu hiyo zimeanza kuonekana kwa mkewe!
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,539
  Likes Received: 81,974
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Sitta matatani
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 17 February 2012 21:42
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  Festo Polea
  Mwananchi

  WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameingia matatani baada ya Jeshi la Polisi nchini kutolea tamko ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na kueleza kuwa hautokani na kulishwa sumu, huku likisema limefungua jalada kwa ajili ya uchunguzi wa kauli yake hiyo.

  Tamko hilo la polisi lililotolewa jana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. DCI Manumba aliwataka watu kuupuza madai hayo akieleza kuwa ushahidi uliopatikana kutoka nchini India alikolazwa Dk Mwakyembe hauonyeshi kuwa alilishwa sumu. Manumba alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wake kuhusu hali na mwenendo wa uhalifu nchini katika kipindi cha mwaka jana.

  Akifafanua kuhusu kauli hiyo ya Waziri Sitta, DCI Manumba alisema, "Jeshi la Polisi limekaa kimya muda mrefu likifanyia uchunguzi kauli hiyo kwa kuwa maneno hayo ndani yake yanaonyesha jinai." Aliendelea “Kazi ya Jeshi la Polisi ni kuchunguza makosa na si kufuatilia nani anaumwa ugonjwa gani. Nani anaumwa nini ni jukumu la madaktari. Lakini tumekuwa kimya muda mrefu tukichunguza tuhuma hizo nzito.’’ DCI Manumba aliendelea kufafanua “Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India.

  Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu katika maradhi yanayomsibu Mwakyembe.’’ Manumba aliongeza kuwa kwa kuwa suala hilo ni la kisheria na kiupelelezi, Jeshi la Polisi linaandaa jalada la upelelezi kuhusu kauli hiyo ya Waziri Sitta na likikamilika, litapelekwa kwa DPP kwa ajili ya uamuzi.

  “Hata hivyo, Sitta mwenyewe nilimsikia katika kauli yake akisema kuwa naye ameisikia katika vyombo vya dola, hivyo tunaandaa jalada la upelelezi na likikamilika litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa uamuazi wa kisheria wa nani ashtakiwe au nani ana makosa. Lakini sasa ni hayo kuhusu kauli hiyo Waziri Sitta ninayoweza kusema,’’ alisema Manumba.

  Awali Manumba alisema kabla Dk Mwakyembe hajaanza kuumwa na kukimbizwa India kwa matibabu, Jeshi la Polisi lilipokea maandishi kutoka kwa waziri huyo yaliyodai kuwa alikuwa akitishiwa uhai wake, lakini likiwa katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wake, akaanza kuugua na kukimbizwa India kwa matibabu.

  “Jeshi la Polisi liliwahi kupata maandishi kutoka kwa Mwakyembe kuwa anatishiwa uhai wake, lakini tukiwa katika hatua za mwisho za uchunguzi, Mwakyembe akaanza kuumwa,’’ alisema Manumba. Historia ya ugonjwa wa Mwakyembe Dk Mwakymbe alianza kuumwa Oktoba 9 mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa katika Hospitali ya Apollo kwa matatibu. Alirejea nchini Desemba 11, mwaka jana baada ya kulazwa hospitalini humo kwa takribani miezi miwili.

  Msemaji wa familia ya Dk Mwekyembe na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema mara baada ya mbunge huyo wa Kyela kurudi nchini kuwa, afya yake ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

  Kauli za Waziri Sitta Mara kadhaa Waziri Sitta amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa ugonjwa wa Dk Mwakyembe, umetokana na kulishwa sumu. Akiwa kwenye uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Jijini Dar es Salaam Januari 28 mwaka huu, Sitta alisema:

  “ Nasema Dk Mwakyembe kapewa sumu, kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka,” alisisitiza Waziri Sitta katika hafla hiyo.


  Sitta alihoji “ Ni vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia, lakini baada ya saa moja unarudia tena, kitu hicho si cha kawaida.” Sitta alisema wamejaribu wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote.

  Waziri Nahodha
  Akijibu moja ya kauli hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nohodha alimtaka Waziri Sitta awasilishe ushahidi wake ili ufanyiwe kazi badala ya kuzungumza nje ya vyombo vya sharia. Hata hivyo, Sitta alisema hatapeleka ushahidi wa madai aliyotoa kuwa Dk Mwakyembe alilishwa sumu kwa kuwa polisi tayari wanao ushahidi.

  Alisema wanachotakiwa kufanya Polisi ni kufanya uchunguzi kuhusu madai hayo ya Dk Mwakyembe kulishwa sumu kwa kuwa ushahidi wanao na wasianze kurushiana mpira.
  “Waziri Nahodha anataka ushahidi gani ikiwa taarifa za madaktari zinazomhusu Dk Mwakyembe kuhusu sumu aliyopewa zilishapelekwa polisi, anataka mimi nitoe ushahidi gani,” alisema Waziri Sitta.

  Kuhusu mwenendo wa uhalifu nchini kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana 2010, Manumba alisema kulikuwa na matishio mbalimbali ya usalama ikiwamo ugaidi, uharamia baharini, wahamiaji haramu na biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Manumba alitaja matishio mengine yaliyojitokeza mwaka huo kuwa ni uingizwaji bidhaa bandia na silaha haramu, dawa za kulevya, migogoro ya kisiasa, kidini, migogoro ya wanafunzi wa taasisi na vyuo vya elimu ya juu na migogoro na migomo ya wafanyakazi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nahisi unatetemeka hadi umeshindwa kuandika vizuri title yako! Pole, ni nduguyo nini!
   
 4. u

  ureni JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mimi nachotaka hapa tuwekewe scanned copy ya taarifa ya uchunguzi wa ugonjwa wa mwakyembe,na hiyo copy iwe imetokea kwa madactari wa india katika hospitali anayotibiwa.Na mtu anayeweza kusaidia ni mwakyembe mwenyewe.

  Nilisikia kwenye vyombo fulani fulani vya habari wanasema inawezekana kapewa polonium yaani sumu ya radiactive,na hiyo sumu ya aina hiyo dalili zake nywele zinanyonyoka na ngozi inababuka,na inaambukiza kwa kuwekewa kwenye chai na majimaji mengine lakini sio kwa kugusana kama kusalimiana n.k,basi kama na mke wake kapata inawezekana ikawa ni hiyo radioactive,ukiwekewa hiyo sumu ni kuwa unahesabiwa muda wa kufa yaani wanasayansi wanaita half life kwa kupitia kiwango alichokuwekea anaweza kucalculate utakufa lini,kama itakua ni hiyo naweza kusema ni terrible.
   
 5. faizah

  faizah Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Wanasutana wenyewe kwa wenyewe tu laana ya walalahoi hiyo na bado
   
 6. V

  Visionmark Senior Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh, kazi kweli kweli! Lkn nachokiamini ni kwawa mh. Sitta hawezi kuzungumza jambo zito kama hilo pasipo kujirizisha na maelezo toka kwa swaiba wake mkubwa Dr. H Mwakyembe & pia mimi naamini kuwa hawa wawili wote ni wa2 makini na isitoshe wanajua fika faida na hasara ya kuzungumza jambo zito kama hilo pasipo uhakika wa kile wakizungumzacho mbele ya hadhara na tukumbuke kuwa wawili hawa wote ni wasomi wa sheria. Kwa kuzingatia tu vingezo hivyo vichache, polisi wa kiTz acheni ubabaishaji & propanganda!
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  khaaa hii sumu itakuwa kali sana ..yaani mume kamuambukiza misumu mikali mkewe..sasa najiuliza hii sumu iko kwenye naniii ndo maana akinaniiihii inaingia kwa mwenzake au..hahaaaa
   
 8. String Theorist

  String Theorist JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  1.Kwa kuwa DCI amesema Mwakyembe hajalishwa sumu,
  2. kwa kuwa kuna taarifa zilisema kuna uwezekano wa mwakyembe ku-reveal secret endapo serikali itaendelea kuficha hiyo siri,
  BASI KUNA KUWEZEKANO WA KUPATA HIYO SCANNED COPY HAPA JF. Ngoja tusubiri wenyewe waziweke hapa.
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  kweli Geshi Ra Porisi Tanzania lina kazi kubwa kupambana na hayo matishio..!
   
 10. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  hapa ni kelele tu,tuwekeeni report ya mwakyembe hapa tujue kusuka ama kunyoa.
  jason bourne kimya.
   
 11. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Nimecha sana japo story ya kuhuzunisha dah ! "Nothing last forever" yana mwisho na tusubiri tu ukweli tutaujua
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  maneno ya viongozi hovyo wa serikali ya kikwete.
  Mgonjwa kasasema yeye kalishwa sumu....yeye ndo anayejua kaambiwa nini na daktari.
  Huyu DCI anatuambia nini huyu!!

  Swala la msingi ni sitta na mwakembe wawaambie umma wa watanzania, ni nani, wapi na kwa nini walilishwa sumu....na ni sumu aina gani.
   
 13. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nchi hii ya kihuni. Jeshi la polisi limeharibu nchi, linashangilia ndugu zetu wamekufa kwa kukosa matibabu!
  Linakumbatia viongozi wasio litakia mema taifa na kusumbua watu wenye nia njema na taifa.

  Hapa nchini hakieleki mpaka tukiingia mtaani kutafuta haki yetu.

  Mwandishi wa Rais Salva Rweyemamu nilimsikia akisema nchi iko salama na inaendelea vizuri! jasho lilinitoka, sikuamini kuwa hawa watu wametusaliti kiasi hiki! Bei ya maharage inakaribia sh 2000 kitu ambacho hakijawahi kutokea huyu mtu mi naona kinyaaa sana na viongozi wote wa nchi.
   
 14. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Anyway, hii nchi haitabadilika mpaka kila raia achangie tuvuruge system iliypo mpaka tu- establish system mpya ya maisha, make system iliyopo, imekuwa ya kishikaji hivyo haitaki mabadiliko na inaonekana ni ya wale walio fanikiwa kuwa wafanyakazi wa serikali na hawataki mtu mpya aingie kwenye nafasi ya serikali kwa kuchuana na kuona kama anaweza bali kwa kujuana na ushikaji. Nitafurahi ikitokea msuguano na hatimaye uasi na mwenye uwezo achukuwe nchi, uhuni wakudanganya kwamba tunachagua kiongozi ni usanii mtupu.

  Nawashangaa chadema kushindwa kufuatilia mambo ya uchaguzi. Bila kuwa na tume huru ya uchaguzi, Tanzania itaendelea kudidimia na viongozi waliko madarakani kuendelea kutengeneza mikataba hewa ya kujinufaisha wao na familia zao, huku wakiacha jamii iliyo kubwa ikiishi kwa maisha ya ki masikini.
   
 15. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kama siyo sumu basi utakuwa ugonjwa wa kuambukiza huo!
   
 16. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ili kumaliza mgogoro huu polisi waende India,waonge na madaktari wa India kwa vipimo vya juu.Mwakyembe akubali kupima Ukimwi na matokeo yatangazwa.Ukimwi na Sumu vinafanya kazi moja.Kama itabainika kuwa kwenye born Marrow kuna sumu isiyokuwa na Ukimwi basi ,sample zipelekwe kwa mkemia,lakini endapo kuna Ukimwi au Ugonjwa wa kuambukiza utakuwa kwa mkewe pia.Hapa ni suala la Muda.Hata hivyo hali ya ngozi ya Mwakyembe na ugonjwa wake umewashangaza wengi na kuwashinda madaktari wetu.Pengine hakuna aliyewahi kuugua.Ni kama jinsi Ukimwi ulivyoingia watu walistuka sana.Hata Ukoma ulivyoingia watu walisituka sana.Nafaham Mgonjwa wa Ukimwi huwa anaharibika sana Ngozi yake na Mbunge wa Kwanza kuanza kunyonyoka ngozi ni Amina Chifupa, kwa tuliomuona kwa macho ktk hatuo zake za mwisho ni afadhali Mwakyembe
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Na yeye kwanini aliisoma nusu ripoti ya Richmond? Aimwage yote.
   
 18. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Dk Mwakyembe anaweza kuwa amelishwa sumu lakini kuna Wabunge wengi ni wagonjwa!Hata Kikwete huwa ana anguka anguka je anau
   
 19. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Je Kikwete anaumwa nini?
   
 20. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180

  Mnyisazu, juzi tu umejisajiri na unaanza kwa *****!
  HIYO RIPOTI YA RICHMOND ndo inayoleteleza hayo yanayomsibu. Unafikiri angeimwaga yote nchi hii ingetawalika toka wakati huo?
  Wanaojua kwamba Mwakyembe anajua mengi ndo hao waliofanya akawa na hali hiyo. Ila nikwambie kitu, kwa mimi mwenye faith naamini kwamba NO SIN EVER GOES UNDISCOVERED!
   
Loading...