Sumry T.888 BWK. Abiria tumetelekezwa Makambako

Sumry wana mabasi mazuri sana kwa nje lakini yasiyo na uhakika sana wa kufika safari,watu wa kusini nashauri tu kuangalia means nyingine za usafiri na sio kutegema hayo mabais kwa mfano songea wanabasi moja linalokwenda Dar liliharibika siku moja maeneo ya lutikira tulianza safari karibia saa 8 mchana.Haaminiki na kupata option nyingine ni suala zito

ni kweli mkuu,hata bus lao la Songea-Dar limeharibika leo,haya mabasi ni mazuri kwa nje tu lakini ni mabovu sana.
 
Ukiona hivyo ujue kuna Kamgomba ameegemea, kamanda vumilia kidogo M4C iko kazini Mambo yatakua Shwari Vimigomba vyote vitakatwa makazi yao mapya ni LUPANGO
 
Ukiona hivyo ujue kuna Kamgomba ameegemea, kamanda vumilia kidogo M4C iko kazini Mambo yatakua Shwari Vimigomba vyote vitakatwa makazi yao mapya ni LUPANGO

Nakubaliana na wewe mkuu kuna kamgomba wanaegemea kwani toka Iringa hamna askari wala trafik yeyote alietusimamisha na kukagua gari au kusalimia abiria japo tutoe dukuduku.
 
hii numba kila siku haipatikani.nadhani zilikuwa mbwembwe tu.
hahaaa nilijua tu nitapata jibu hilo,hawa wapuuzi washatuona sisi wajinga tunaestahili kudanganywa kamawatoto wadogo,dawa ya inachemka watakunywa 2015, kama walivyo pangana kwenda kunywa kikombe kwa babu loliondo.
 
Sumry ni takataka kabisa,mimi nimepanda ile wanayoiita high class namba T 808 BXZ jana kutoka Dar kwenda Mbeya tukafika Makambako brake zikajam baridi ya hapo ikanishinda nikadandia gari ndogo iliyokuwa inaenda Tunduma nikangia Mbeya karibu saa 3 usiku,nasikia waliondoka pale baada ya masaa 3
 
Back
Top Bottom