Sumry T.888 BWK. Abiria tumetelekezwa Makambako

MKUNGA

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
441
71
Wakuu,tumepanda bus la Sumry kuja Dar, limeharibika hapa nje ya Makambako toka saa 3 asubuhi, hawataki kuturudishia nauli,wametuahidi kutuletea bus jingine tokaMbeya wanatudanganya lipo karibu na halifiki.

Hivi hii kampuni inapata wapi kiburi cha kunyanyasa watanzania?

My take: Haya mabasi hayafai coz hata abiria wanasema ni mabovu,so ukiwa na safari ya Mbeya tafuta mabasi mengine.

Hatimae tumeondoka saa 10:10 pm,mtuombee tufike salama,huku kusini usafiri shida ati na naambiwa haya mabasi ya Sumry ndio tegemeo huku.

Update.
Hii sasa too much,tumelikuta Sumry la MZA-DAR limeharibika maeneo ya Ruvu darajani,imebidi abiria wote wajazwe huku kwetu kama magunia vile,kwa kweli inasikitisha jinsi abiria wanavyonyanyasika.
Final update.
Nashukuru Mwenyezimungu ametuwezesha tumefika salama Dar.
 
Mlikuwa mnatokea wapi kama ni yale mapya kwa uzoefu wangu yana shida sana kwenye mfumo wa engine na transmission hii ni kutokana na uendeshaji mbovu wa madereva. hizo gari zina auto control.
 
Poleni ila wakumbushe mkifika late muendako wawape ela ya taxi au ya guest!
 
Mpigie mwakiembe dr no 0782242526 atawasaidia ndio moja ya majukum yake tuliyo amepewa.poleni sana mkuu,au mpigieni kamanda wa kikosi cha barabrni awasaidie mkuu!
 
Poleni ila wakumbushe mkifika late muendako wawape ela ya taxi au ya guest!
Umesahau disturbance Allowance Comrade nayo ni muhimu wakapewa hawa jamaa,nilipata kusikia PM anamkono wake hapo nadhani hicho kiburi kinatoka kwa Pinda, mtoto wa mkulima aliemezwa na Mafisadi
 
Wakuu,tumepanda bus la Sumry kuja Dar, limeharibika hapa nje ya Makambako toka saa 3 asubuhi, hawataki kuturudishia nauli,wametuahidi kutuletea bus jingine tokaMbeya wanatudanganya lipo karibu na halifiki.
.

Mbeya hadi Makambako ni mwendo wa saa kama 3 hivi. Na ku-mobilise basi jingine, dereva nk huenda ikachukua saa nzima. Sijui umesubiri toka saa ngapi, labda unapaswa kuwa na subira. Ila uwezekano wa kulala Morogoro uwe karibu, maana si rahisi mfike Dar kabla ya saa nne usiku!
 
Watu hamna shukrani iyo namba aliitoa ili muwe mnampa kero!
Na kwenye ulimwengu wa masoko feedback ya mteja ni muhimu kwa ajili ya kuimprove huduma!
Ukikaa kimya nani atajua kwamba ulipata tatizo?
 
Poleni sana nafikiri wanasubiri basi la sumbawanga ama songea lifike Mbeya wawapakie sumry sio basi la kupanda.
 
Pole mkuu: vuta subira mtapata usafiri mwingine, kurudishiwa nauli hapohapo sio rahisi sana sana mtaambulia majibu ya hovyo kutoka kwa kondakta na dreva wake kwani pesa huwa zinabaki kwenye ofisi zao wanapokatia tiketi labda ndogondogo za wao kunywa maji na kuonga kwa trafiki ndizo wanatembea nazo.
 
poleni ila mi nawashauri muandamane mapaka kituo cha polisi kilichoko karibu ili kutatua
suala la fedha si unajua wabongo hata bodi ya mikopo lazima wwndamane ili ankara itoke
 
Wakuu,tumepanda bus la Sumry kuja Dar, limeharibika hapa nje ya Makambako toka saa 3 asubuhi, hawataki kuturudishia nauli,wametuahidi kutuletea bus jingine tokaMbeya wanatudanganya lipo karibu na halifiki. Hivi hii kampuni inapata wapi kiburi cha kunyanyasa watanzania? My take: Haya mabasi hayafai coz hata abiria wanasema ni mabovu,so ukiwa na safari ya Mbeya tafuta mabasi mengine.
Fungueni matairi muuze mkagawe pesa za nauli wao si wanajifanya wajanja
 
T.888 BWK mbona gari mpya kabisa hii?


Hapana mkuu. Uzuri wa mkakasi, ndani pande la mti. Sio vyote ving'aavyo ni dhahabu. Magari mazuri kwa makampuni mengi kama sio yote huwa wanayapeleka Arusha na Nairobi. Yakichakaa ndio wanayapeleka Kyela na Tunduma na Mwanza na Bukoba na /.....(Sema tena ni wapi kule?). SABCO alijipatia jina kupitia Kyela, alipolea sifa akanunua mabasi mapya na very comforting, lakini akayapeleka Arusha, Nairobi. hata HEKIMA na SCANDINAVIA walifanya hayohayo.

Suluhisho ni kuwasusia kama alivyosusiwa TAWAQAL na MATEMA BEACH kwa kuleta mabasi chakavu, hawapo tena njia hiyo. ABOUD sijui kwa nini haendi Kyela wakati hata ofisi alifungua. Watu wa Kyela smart sana katika kumponda mtu anayejifanya mjuaji zaidi. Ni jadi yao, kumbuka Kawawa aliambiwaje alipoenda kufunga maduka ya watu binafsi ati maduka ya ushirika peke yake ndio yaendelee, alipotumwa na mkubwa wake Ng'walimu. Kyela, Ujiji na Bagamoyo wote dugu moya kwa misimamo.
 
Sumry wana mabasi mazuri sana kwa nje lakini yasiyo na uhakika sana wa kufika safari,watu wa kusini nashauri tu kuangalia means nyingine za usafiri na sio kutegema hayo mabais kwa mfano songea wanabasi moja linalokwenda Dar liliharibika siku moja maeneo ya lutikira tulianza safari karibia saa 8 mchana.Haaminiki na kupata option nyingine ni suala zito
 
Watu hamna shukrani iyo namba aliitoa ili muwe mnampa kero!
Na kwenye ulimwengu wa masoko feedback ya mteja ni muhimu kwa ajili ya kuimprove huduma!
Ukikaa kimya nani atajua kwamba ulipata tatizo?

Hizi namba hawa magamba huwa wanatoa ili kupata popularity tu kama vile kuuza sura kwani mara nyingi ukiwapigia kwa kutumia hizo namba hawapatikani!!
 
Hizi namba hawa magamba huwa wanatoa ili kupata popularity tu kama vile kuuza sura kwani mara nyingi ukiwapigia kwa kutumia hizo namba hawapatikani!!
Ukitaka kujua kama namba ni yake kweli mtumie M- pesa kiasi fulani then jina litakuja
 
Back
Top Bottom