Sumaye: Tume ya Uchaguzi imeweka amani rehani

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,885
2,000

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye

Kwa ufupi
Alisema nchi nyingi hupoteza amani na utulivu wao katika hatua hii ya mchakato wa kura na kukataa matokeo.

Arusha.Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema Tume ya Uchaguzi isipotenda haki katika kutangaza matokeo, inaweza ikasababisha uvunjifu wa amani nchini.

Sumaye aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua semina ya uhamasishaji ya vijana wa CCM iliyofanyika mkoani Arusha.

"Wakati wa uchaguzi ni lazima wahusika wote hasa Tume ya Uchaguzi lazima itende na ionekane inatenda haki sawa kwa kila mgombea wa kila chama.

"Upendeleo na uonevu wa aina yoyote iwe baina ya vyama au baina ya wagombea ni sumu kwa amani na utulivu wetu…Tume kutokuwa na uwazi wa kutosha katika shughuli zote zinazohusu uchaguzi hasa wakati wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo.

"Hisia yoyote ya udanganyifu, upendeleo au wizi wa kura ni sumu ya amani na utulivu. Uchaguzi ndipo mahali ambapo raia hutumia haki yake ya kuchagua na kuchaguliwa na hiyo haki yake ya msingi," alisema Sumaye huku akishangiliwa.
Sumaye anayejinasibu kuwania urais, alisema jambo lolote linalotafsiriwa kupokonya haki hii haitavumiliwa na hujibiwa kwa mapambano.

Alisema nchi nyingi hupoteza amani na utulivu wao katika hatua hii ya mchakato wa kura na kukataa matokeo.

"Nchi nyingi zimejikuta katika uvunjivu wa amani na utulivu kunapokuwa na chama au upande moja unaokataa matokeo ya kura zilizopigwa. Mifano ya hali hii ni mingi katika nchi za Afrika na mara kadhaa Serikali zimeangushwa au kuishia katika mgawanyo wa madaraka jambo ambalo linawanyima raia haki ya kutetewa bungeni na upande wa upinzani ambao katika utaratibu huo nao huingia katika serikali ya mseto.

"Ni vyema pale udhalimu haukutumika katika uchaguzi, vyama vyetu vikajua kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani na hakuna utaratibu ambao unawafanya washindani wote kuwa washindi," alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,866
1,500
Nampongeza Sana Sumaye kwa kuliona hili, Inakera kusikia eti kuna maeneo CCM wameweka pingamiza na kuruhusiwa wagombea wao kupita bila kupingwa eti kwa kuwa mahasimu wao CHADEMA waliteleza kwa kutumia muhuri usiotakiwa!!! Ubakaji wa Rasilimali zetu tumefumbia macho huku roho ikizizima kwa machungu, UFISADI tunavumilia kwa uchungu mkubwa ili sharia ichukue mkonndo wake tho majaji wamegeuka genge la walarushwa wakuu... UBAKAJI wa Demokrasia utawatumbukia nyongo Watanzania soon na huenda ikasababisha mauaji ya kutisha kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii... Hope JK anayaona haya yanayotendeka ndani ya nchi yake ....
 
Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,885
2,000
Njia pekee yakuingoa ccm na mapapa wake wa Ufisadi si kutegemea kura ya vikaratasi (Tume Zec) hawa ni tawi moja la ccm na kitakacho fanyika ni udanganyifu tu wa tume.

Hivi sasa Serekali ya ccm imeshindwa na inanuka kwa ufisadi ulokusiri wa mamillionea ya vigogo kuiba pesa ya umma, huku wananchi tukiwa hatuna dawa mahospitalini ,elimu mbovu na kila kitu ununue na kula isio ya uhakika.

Inafika hadi mgonjwa wako anakufia mikononi huna uwezo na mtoto wako kushindwa kuenda chule huna ada, mbali kununua vifaa.

Tukumbuke Watanzania kua kuna sakata la Escrow watu wamekula mabillionea na bado wako maofisini bila serekali ya ccm kuwawajibisha , hii nikuonyesha Serekali ya ccm haiko safi na wanalindana kwa vile sio wasafi.

Hili la Escrow ni moja tu lililokuja juu ,lakini kuna huko nyuma watu wamejilimbikizia mabillion ya wezi wa pesa za Umma, hali hii ikiendelea tujuwe Watanzania nchi itakauchwa na maisha bora tusahau itakua maisha bora ni kwa vigogo na familia zao.

Hii pesa tusizani hatuna haki nayo au haina mwenyewe kama vile watanzania wengi wanavyo hisi mentality hio, hizi ni pesa zetu wananchi na zilitakikana zitumike kwa huduma za umma.

Hukumu ya Mafisadi tusitegemee kutolewa na Mahkama au Bunge ,Nilazima hukumu tuitowe wenyewe wananchi kwa vile Mahakama na Serekali yake ya ccm haziko safi na zimepoteza imani kwa umma wa Tanzania.
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Amwambie JK kabisaaa, kuiba kura na kuweka mapingamizi uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji ni kuminya demokrasi, huo ni uchaguzi ambao hata unaweza kuendeshwa kwa kusimama nyuma ya mgombea maana tunafahamiana na tusiendekeze ndumilakuwili asema hivi anafanya vile
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,939
2,000
Waziri Mkuu mstaafu lakini.kichwani hakuna kitu!

Jana alikuwa anawahamasisha watu wapokee Rushwa!
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,627
2,000
Njia pekee yakuingoa ccm na mapapa wake wa Ufisadi si kutegemea kura ya vikaratasi (Tume Zec) hawa ni tawi moja la ccm na kitakacho fanyika ni udanganyifu tu wa tume.

Hivi sasa Serekali ya ccm imeshindwa na inanuka kwa ufisadi ulokusiri wa mamillionea ya vigogo kuiba pesa ya umma, huku wananchi tukiwa hatuna dawa mahospitalini ,elimu mbovu na kila kitu ununue na kula isio ya uhakika.

Inafika hadi mgonjwa wako anakufia mikononi huna uwezo na mtoto wako kushindwa kuenda chule huna ada, mbali kununua vifaa.

Tukumbuke Watanzania kua kuna sakata la Escrow watu wamekula mabillionea na bado wako maofisini bila serekali ya ccm kuwawajibisha , hii nikuonyesha Serekali ya ccm haiko safi na wanalindana kwa vile sio wasafi.

Hili la Escrow ni moja tu lililokuja juu ,lakini kuna huko nyuma watu wamejilimbikizia mabillion ya wezi wa pesa za Umma, hali hii ikiendelea tujuwe Watanzania nchi itakauchwa na maisha bora tusahau itakua maisha bora ni kwa vigogo na familia zao.

Hii pesa tusizani hatuna haki nayo au haina mwenyewe kama vile watanzania wengi wanavyo hisi mentality hio, hizi ni pesa zetu wananchi na zilitakikana zitumike kwa huduma za umma.

Hukumu ya Mafisadi tusitegemee kutolewa na Mahkama au Bunge ,Nilazima hukumu tuitowe wenyewe wananchi kwa vile Mahakama na Serekali yake ya ccm haziko safi na zimepoteza imani kwa umma wa Tanzania.
Ndio upo kwenye kampeni himu jf or? nenda mtaani.
 
wakimataifa

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
942
0
wewe nenda chama chochote nani anakutaka miaka kumi uwazirikuu umefanya nini ccm hatutaki usizingumzie kupitia mgongo wa ccm kwenda
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom