Sumaye na mbeleko ya Lowassa

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
13,344
14,817
Wengi tulijua kwa uwezo wa bwana Fredrick Sumaye kisiasa ni mdogo sana, umaarufu wake kisiasa ulikuja mwaka 95 alipobebwa na mbeleko ya Uwaziri Mkuu baada ya kuteuliwa na Rais Mkapa.

Ni imani kama angesimama yeye kama yeye alikuwa hatoboi, hata huko jimboni kwake Hanang alikuwa akipita kwa mavirigiza tu lakini si kwa uwezo wake kisiasa.

Hata ndani ya CCM alijulikana ndio maana alishindwa mara kadhaa katika kura za ndani ya CCM kama si kukatwa kabisa.

Haikushangaza 2015 ghafla alipojiunga na Chadema, na kujifanya ni mshauri na msindikizaji wa mgombea Urais kupitia bendera ya Ukawa Mzee Lowassa.

Ilijulikana wazi hapo ameamua kujivua nguo mwenyewe na kujionyesha udhaifu wake kisiasa na alijua kusafiria nyota ya Lowassa kama si mbeleko.

Hata Chadema walipompatia huo uwenyekiti kwa ushauri wa Lowassa kama ishara ya shukrani ya kujitolea. Wengi walijua kama kungekuw na uchaguzi wa kweli basi Sumaye asingetoboa.

Mbeleko ya Mzee Lowassa imedhihirika muda mfupi tu baada ya kusimama peke yake, asijitie visingizio kibao vya uwenyekiti wa Mbowe hii imejiweka wazi tu kama kwenye kanda, tena bila mgombea kashindwa.

Je huko taifa angesema maneno gani wakamuelewa?

Sumaye umeamua kujivua nguo kuonyesha uwezo wako mdogo kisiasa na mbeleko ya Mzee Lowassa imechakaa hivyo imekuangusha, lakini pia pongezi kwa wana Chadema kwa kugundua wewe si mwenzao siku zako zinahesabika.

Chukua maamuzi mapema kama wenzio walioona mbali Chadema msingi wake ulijengwa kwa jasho na damu, wewe ulitaka kujitwalia madaraka kirahisi bila kujua wenye Chadema kama wapo hai na wanakuangalia.

Ushauri, jitafakari jitathimini chukua maamuzi mapema mzee siasa ni mchezo mchafu. Ulizoea mbeleko sasa imekubwaga.
 
Hongera kwa kuamua kusema ukweli japo ukiwa umechelewa, na kwa taarifa yako sio hao uliowataja tu hata Magufuli hawezi kushinda kwa uchaguzi wowote wa haki maana hana uwezo wa ushawishi. Fuatilia hata yeye hajawahi kushinda kwa uhalali zaidi ya mara moja, mara zote alikuwa anashinda kwa figisu. Na isitoshe sio Sumaye na Lowassa tu, bali wanaccm karibia wote hawawezi kushinda kwenye uchaguzi halali zaidi ya kutegemea vyombo vya dola.
 
Sumaye kushindwa ndani ya chama chetu sio mwisho haya ni yakawaida Sana katikati ushindani wa haki Achana na ccm manunuzi.
 
unajuwa chadema wa kweli ni yule asiye kuwa na cheo chochote , kama sumaye alikuja chadema kwa nia ya kuleta mabadiliko basi ataendelea kuwa na msimamo wa mabadiliko bila kuwa na cheo. umarufu wake wa kuwa waziri mkuu mstaff unatosha kuendelea kuhubili utawala wa sheria na utawala shilikishi ambao ndio msingi wa chadema.
 
Hongera kwa kuamua kusema ukweli japo ukiwa umechelewa, na kwa taarifa yako sio hao uliowataja tu hata Magufuli hawezi kushinda kwa uchaguzi wowote wa haki maana hana uwezo wa ushawishi. Fuatilia hata yeye hajawahi kushinda kwa uhalali zaidi ya mara moja, mara zote alikuwa anashinda kwa figisu. Na isitoshe sio Sumaye na Lowassa tu, bali wanaccm karibia wote hawawezi kushinda kwenye uchaguzi halali zaidi ya kutegemea vyombo vya dola.
Magufuli atashinda kama alivyoshinda 2015 maana kwa sasa hakuna wa kushindana nae kwa hoja ningemshauri tu safari hii hata kampeni asipige!
 
Hivyo unakiri kuwa amenyongwa sababu ya uwenyekiti!
unajuwa chadema wa kweli ni yule asiye kuwa na cheo chochote , kama sumaye alikuja chadema kwa nia ya kuleta mabadiliko basi ataendelea kuwa na msimamo wa mabadiliko bila kuwa na cheo. umarufu wake wa kuwa waziri mkuu mstaff unatosha kuendelea kuhubili utawala wa sheria na utawala shilikishi ambao ndio msingi wa chadema.
 
Sumaye hakwenda CHADEMA kwa Mbeleko ya Lowasa...yalikuwa NI maamuzi yake Tena magumu,baada ya kutorifhishwa na CCM
Mbeleko ya Lowassa na ukaskazini ndio vilivyompeleka Sumaye CDM.

Sumaye hakuwahi kulalamika wala kukemea ilhali alikua na uwezo wa kufanya hivyo kutokana na nafasi yake juu ya matendo ya CCM baada ya EL kuhama na yeye ndio akachukua uamuzi huo. Hana jipya kwenye siasa
 
Magufuli atashinda kama alivyoshinda 2015 maana kwa sasa hakuna wa kushindana nae kwa hoja ningemshauri tu safari hii hata kampeni asipige!

Sikatai maneno yako maana hiyo ni haki yako. Magufuli anaweza kushinda ila sio kwa ushawishi wa hoja wala ushindi wa kishindo. Namna pekee inayoweza kumfanya ashinde ni mbeleko ya vyombo vya dola. Sasa kama anategemea kushinda kwa kutumia vyombo vya dola, nani atashindwa hilo? Kama angekuwa anakubalika kama mnavyojidanganya basi tungeona watu wengi wakijitokeza kujiandikisha kupiga kura.
 
Mbeleko ya Lowassa na ukaskazini ndio vilivyompeleka Sumaye CDM.

Sumaye hakuwahi kulalamika wala kukemea ilhali alikua na uwezo wa kufanya hivyo kutokana na nafasi yake juu ya matendo ya CCM baada ya EL kuhama na yeye ndio akachukua uamuzi huo. Hana jipya kwenye siasa
Kuelekea uchaguzi 2015 Sumaye alikuwa anaikemea CCM wazi2 kabla hata ya kabla ya Gia ya angani
 
Sumaye umeamua kuonyesha uwezo wako kisiasa lakini pia pongezi kwa wana Chadema kwa kugundua wewe siku zako zinahesabika.

Chukua maamuzi mapema kama wenzio walioona mbali.

Ushauri, jitafakari jitathimini chukua maamuzi mapema mzee siasa ni mchezo mchafu.
Naunga mkono hoja
P
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom