Sumaye na Lowassa si wapinzani, Upinzani tafuteni damu mpya

matunge

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
442
426
Sumaye na Lowassa si wapinzani. Na tusipoangalia wataua kabisa dhana ya upinzani.

Inasikitisha kuona wanapewa nafasi za juu kabisa za uongozi (pasi na vyeo) mfano kuwa wageni rasmi katika graduations za wanasiasa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Nasoma kwamba Lowassa alikuwa DSM na Sumaye Dodoma. Jambo la msingi ni kuibuliwa kwa vijana wapya wenye moyo wa dhati wa kuikosoa serikali pia kuonesha dira kinzani yenye hatma ya kushika dola.

Si kuwatumia hawa magalasa waliotemwa kwa kashfa.
 
Serikali inawaandaa vijana damu changa, hawa ambao wanasambazwa kwa nguvu ktk mahafali ya chama ili wawe wapinzani halisi na weny hasira kali.

Usimchezee mnyama aliyejeruhuwa.
 
Sumaye na Lowassa si wapinzani. Na tusipoangalia wataua kabisa dhana ya upinzani.

Inasikitisha kuona wanapewa nafasi za juu kabisa za uongozi (pasi na vyeo) mfano kuwa wageni rasmi katika graduations za wanasiasa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Nasoma kwamba Lowassa alikuwa DSM na Sumaye Dodoma. Jambo la msingi ni kuibuliwa kwa vijana wapya wenye moyo wa dhati wa kuikosoa serikali pia kuonesha dira kinzani yenye hatma ya kushika dola.

Si kuwatumia hawa magalasa waliotemwa kwa kashfa.
andikeni habari nyingine, za lowassa hazikupeni faida........hakuna uchaguzi tena
 
Hayakuhusu, toka lini magamba mkawa washauri wa UKAWA?
Asante. Kwa kumjibu huyu ndugu. Maana nafikiri ndipo uwezo wake wa kufikiri ulipokwamia.

Badala ya kuzungumzia, maendeleo yanayofanywa na uongozi wa chama chake tangu Awamu ya 5 ilipoingia madarakani, wamefanya nini kuondoa umaskini na kuwaletea wananchi maendeleo. Anakuja kuisemea ukawa?
 
Tanzania inahitaji upinzani thabiti ili iweze kuendelea. Wazee hawa wastaafu wanaua upinzani wa kweli.
 
Hebu fikiri kwa mawazo huru; hivi Lowassa awe Rais, Waziri Mkuu Sumaye -----Huu ni uongozi unaotokana na upinzani kweli?
 
kwani lowassa na sumaye walitemwa ndani ya ccm au wao ndo walijiondosha wenyewe ccm, acha porojo andika vitu venye mantiki hivi kwa nguvu alizokuwa nazo Lowassa ndani ya CCM ni nanialikuwa na uwezo wa kukuambia aondoke CCM
 
kwani lowassa na sumaye walitemwa ndani ya ccm au wao ndo walijiondosha wenyewe ccm,acha porojo andika vitu venye mantoki hivi kwa nguvu alizokuwa nazo lowassa ndani ya ccm ni nanialikuwa na uwezo wa kukuambia aondoke ccm
Vyote sawa. Jambo la msingi ni nchi kupata upinzani ulio imara. Kuna vijana wengi wapo vyuoni. Ni rahisi sana kuwafahamu kwani katika kila jambo linalohusu maslahi ya wengi wao huongoza harakati. Tena huwa hawahusiani kabisa na vyama vya siasa.
 
Sumaye na Lowassa si wapinzani. Na tusipoangalia wataua kabisa dhana ya upinzani.

Inasikitisha kuona wanapewa nafasi za juu kabisa za uongozi (pasi na vyeo) mfano kuwa wageni rasmi katika graduations za wanasiasa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Nasoma kwamba Lowassa alikuwa DSM na Sumaye Dodoma. Jambo la msingi ni kuibuliwa kwa vijana wapya wenye moyo wa dhati wa kuikosoa serikali pia kuonesha dira kinzani yenye hatma ya kushika dola.

Si kuwatumia hawa magalasa waliotemwa kwa kashfa.

Acha kukubali kukaririshwa wewe, changanya na za kwako!! Nini maana ya damu changa, watu wanapimwa kwa OUTPUT na sio Damu changa wala iliyokomaa. Dont you know that "Old is Gold"?
 
It is true that old is gold but not for those guys. Hawajawahi kuwa wapinzani; wamelelewa na system na kunufaika nayo. Wanaua upinzani. hakika
 
Unataka kusema ukitoka Simba na kuhamia Yanga huwezi kuifunga Simba?. Na unaposema wanaua upinzani nashindwa kukuelewa, kwani rekodi ya ushindi iliyopo sasa haijawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi, sasa unaposema upinzani unauwawa sijui Research yako ina "base" kwenye facts zipi. Sometimes results zinabase na Hypothesis yako, au chama chako au aliyekutuma kufanya hiyo research.
 
Back
Top Bottom