Sumaye: Mimi kwenda upinzani ni faida kwa CCM

Jini Kisiranii

JF-Expert Member
Feb 20, 2018
1,626
1,676
Hebu sikilizeni hii japo ngumu kumeza, wapinzani inabidi mjitafakari sana. mnahangaika na msomi mwenye IQ kubwa sana mara milioni kuliko nyie. Magufuli ana akili kuwazidi mbali sana. Kamwe hamuwezi kupambana naye.

 
sema nini mkuu kuna ukata kama nini

ungeandika iyo kauli na ukaambatanisha na iyo video ingenoga kama nini
 
''baada ya hapa,naomba mh Rais niongee na wewe japo dakika 2''!!!????!!!!!!?!????
 
Siasa ya Tanzania bado haijafikia hatua ya kupevuka yaani "maturity stage". Dalili zote zinaonyesha kuwa tupo kwenye hatua ya kukua yaani "growth stage". Dalili zinazoambatana na ukuaji ni woga na unafiki kwa wanasiasa na tabaka la juu la raia. Idadi iliyobaaki ya raia hata hawajui nini kinachoendelea. Wao wanakuwa watazamaji tu na hawana la kusema.

Kwa bahati nzuri sana, kadri siku zinavyoyoyoma yapo mabadiliko ya msingi yanatokea na matunda yake tutayaona muda si mrefu sana. Kwa mtafiti makini hawezi kushindwa kuona kukua kwa kasi kizazi kinachohoji huku kile kizazi mbumbumbu kikitoweka kwa kasi kubwa sana. Bila ushahidi, ninaona dalili za nguvu za kisiasa zikiamuliwa mijini na kwenye majiji na waamuaji ni watu wenye kiwango fulani cha elimu kama kidato cha nne na diploma.

Kizazi hiki ndio chenye uwezo wa kupiga kura na kulinda maamuzi waliyofanya kwenye sanduku la kura hata ikibidi kwa kumwaga damu. Uhuru unaleta heshima pale ambapo walioupata huo uhuru wapo tayari kuulinda kwa rasilimali zao, damu zao na hata uhai wao.

Tutaelewana tu muda si mrefu.
 
Hebu sikilizeni hii japo ngumu kumeza, wapinzani inabidi mjitafakari sana. mnahangaika na msomi mwenye IQ kubwa sana mara milioni kuliko nyie. Magufuli ana akili kuwazidi mbali sana. Kamwe hamuwezi kupambana naye.



Ungeelewa ni i amekusudi kusem hivyo.
Ccm 2015 ili elemewa na ufisadi na wizi.
Ilikua inanuka kwa kashfa mbali mbali...
Hivyo kulikua na haja ya kuimarisha vyama vingi na kuvipa nguvu ili ccm iamke ijirekebishe iache wizi na ufisadi.
Na ukweli kuwapo kwao upinzani kumewawezesha kupata nguvu na kuweza kushindw kwa kura laki 8 tu.

Hili ilikua funzo kwa ccm watumie muda wao huu kujenga misingi imara ya uchumi , na kuimarisha maisha ya watanzania
Kuondoa ufisadi na kuimarisha utawala wa sheria na haki.

Lakini ccm haikuweza kuchukua kuimarika kwa upinzani kama changamoto bali kama uadui.
Magu anWaonea sana ana wafunga anawakomoa kila Mbunge wa chadema ana kesi.
Amegeuza wapinzani kama maadui wakubwa .
Wapo waliopigwa risasi kina tundu lissu wapo wakosoaji waliopotezwa.
Hivyo ccm hawakumulewa sumaye wamechukua njia inayokiangamiza chama hicho na kujeng uadui na watanzania.
Wangetumia nafasi hio vema basi ndio ingekua kwa faida yao.
Na kama ukawa wangeshinda basi kuwa na watu kama lowassa na sumaye ambao wana uzoefu wa kuongoza serikali pia ni faida kwa ccm kwani nchi inge ongozwa na watu wenye uzoefu
Lakini sikio la kufa
 
Back
Top Bottom