chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, leo katika ukumbi wa hoteli ya African Dream mjini Dodoma, amesema ameshangazwa na kitendo cha utawala wa rais Magufuli kutumia nguvu nyingi kukandamiza uhuru wa maoni kwa kuwa yeye ni mtu aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia ambapo maoni tofauti yanakuwepo na yanaruhusiwa kusemwa.
Amesema vitendo hivyo badala ya kuleta amani na utulivu katika jamii ndio vinazidi kuleta hasira na chuki.
Ameongezea kusema kama rais hataki kusemwa basi atangaze rasmi kuwa yeye ni dikteta na atakayemkosoa atakatwa kichwa au kutupwa gerezani.