Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye kesho Jumamosi anatarajiwa kuunguruma akitokea Dodoma.
Ni katika mahafali ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali wa mkoa mkoa wa Dodoma ambao ni wanachama wa CHADEMA chini ya Umoja wao ujulikanao kama CHASO.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CHADEMA atakuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo na anatarajiwa kutoa hotuba mbele ya halaiki hiyo.
Sumaye mwenye mvuto mkubwa katika Taifa hili na mwenye mvuto mkubwa katika jamii amekuwa akipamba na kuteka vyombo vyote vya habari pale anafungua mdomo wake kutamka jambo lolote.
Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanabashiri hotuba ya Sumaye itajikita katika mambo kadhaa ikiwamo vurugu zinazoendelea ndani ya bunge la Tanzania kwa kufukuza hovyo wabunge wa upinzani.Pia anatarajiwa kuzungumzia upigaji marufuku wa shughuli zozote za kisiasa kwa vyama vya upinzani na pia yanayoendelea kutokea Zanzibar.
Maandalizi yote yameshakamilika na shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa African Dream (Area D) kuanzia saa 4 asubuhi.
Waziri mkuu huyo mstaafu atafuatana na wabunge wote wa UKAWA walioko Dodoma na viongozi mbalimbali wa chama mkoani Dodoma na Taifa.
Kutokana idadi kubwa sana ya waandishi wa habari waliothibitisha kushiriki wanaombwa ifikapo saa 2 asubuhi wawe wameshakaa kwenye nafasi zao.