Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Akihojiwa leo asubuhi kupitia redio Clouds, Sumaye alisema: 'Mimi ni mwanaCCM damu lakini endapo nikichukua fomu ya kugombea urais halafu nikashindwa na mtu (Lowasa) kwa sababu ya kutumia fedha kuhonga na kugawa rushwa, basi mtanisamehe--nitagombea kupitia chama chochote cha upinzani', alisema.
Wakati huo huo, mwanasiasa mkongwe, babu Kingunge Ngombale Mwilu amewaunga mkono wale walioanza mapema mbio za urais kwa sababu kujitokeza mapema kutawafanya wananchi wawajue, wawajadili na kufanya uamuzi sahihi wakati wa uteuzi/uchaguzi utakapofika.
MY TAKE:
1. Sumaye anatanguliza mbele maslahi binafsi kuliko maslahi ya chama/umma; na hii ndiyo tabia ya wanaCCM wengi--wanajali matumbo yao zaidi ya maslahi na ustawi wa nchi. Ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma miongmi mwa wanaCCM, ni matokeo ya ubinafsi na uchumia tumbo na utovu wa maadili
2. Huu mchuano wa URAIS, ambapo kila mtu huibuka na kusema la kwake, utaipasua CCM hata kabla ya 2015.
Ngoja tusubiri tuone huu mtanange utaishaje.
Kwanza ungetangaza maslahi ambayo umeyficha nyuma ya mada yako. Pili sio Clouds ni Radio Tumaini ya Kanisa Katoliki, ambayo maajabu yaliyotokea hata file la hayo mahojiano limepotea!!!!!
Jambo lingine ni kwamba hakusema atagombea wala atachukua fomu kwa chama kingine bali amesema chama kitagawanyika kama atapitishwa anayegawa fedha za rushwa kwani hata yeye hatompiga kampeni mla rushwa, na akasisitiza akipitishwa mtu msafi hata yeye atakipigia kampeni chama chake. Sasa hayo maslahi unayoyasema yako wapi? ndio maana umechanganya mada na ya Kingunge kumtetea Lowassa. Hujakatazwa kumtetea mtu lakini tujitahidi kutopindisha maneno kwa kulishwa maneno na kuyaweka humu. Kwa taarifa ni kwamba watu wamerekodi live majumbani mwao na audio ipo.
Ni kweli ndani ya CCM hakuna msafi asilimia mia moja hali kadhalika kwa sasa tumeshasikia ndani ya upinzani nako si safi kabisa na sasa wabunge wanajichotea mamilioni (wakiwamo wapinzani) na wanatetea hadi mapovu yanawatoka. Lakini jambo la msingi wanaokemea rushwa tusiwabeze huenda wakatubu na Lowassa asimame akemee rushwa na ufisadi ili tumuone naye ni msafi ama anaelekea kutubu.