Sumaye: Hatutaki watu wanaochochea fujo ndani ya nchi kwasababu tu wanatafuta madaraka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,406
2,000
WAZIRI Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Frederick Sumaye, ameibuka na kuitaka serikali na vyama vya siasa kuchukua hatua dhidi ya wagombea ambao wanatoa kauli zinazohatarisha kuvunjika kwa amani.

Pia amesema ushindani wa vyama na wagombea upo japo si mkali sana kulinganisha na uchaguzi uliopita.

Sumaye ambaye alikuwa akizungumza jana katika mahojiano maalum na gazeti hili, alisema amani ya Tanzania lazima idumishwe kwa kiwango chochote kile, hivyo haitakiwi mgombea au viongozi wa chama kutoa kauli ambazo zinahatarisha amani.

"Wanaotaka kuleta vurugu, kwanza vyama vyao viwashughulikie lakini kama haviwezi kuwashughulikia serikali ipo iwashughulikie," alisema Sumaye licha ya kwamba hakutaja wagombea ambao wanatoa kauli za kuhatarisha amani.

Sumaye ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu aliporejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema wananchi kwa upande wao wawaadhibu wagombea wanaoleta vurugu kwa kutokuwapa kura.

"Hatutaki watu wanaotaka kuleta fujo kwenye nchi kwa sababu tu wanatafuta madaraka. Mgombea wa namna hiyo hafai kuwa kiongozi," alisema Sumaye.

Aliongeza kuwa amani ya Tanzania ni lazima ilindwe kwa kila mtu na si kitu cha kuchezea kwa kuwa nchi yoyote ikishapoteza amani huwa hairudi tena.

Kwa mujibu wa Sumaye, katika kipindi cha kampeni wagombea wanatakiwa kujikita zaidi katika kunadi sera za vyama vyao ili wananchi wazichuje na kuwachagua wale ambao sera zao ni nzuri.

Sumaye alisema Tanzania ndiyo nchi pekee katika Afrika ambayo wananchi wake wamekuwa wakifurahia amani kwa hiyo haitarajiwi mtu yeyote afanye mambo ambayo yanahatarisha amani ya nchi.

Alisema kiongozi yeyote anatakiwa awaonyeshe wananchi kwa kuwaletea maendeleo na si kuleta mapigano.

"Kama kuna chama ambacho kinasema sera yake ni kuleta fujo itabidi kishughulikiwe tofauti, japo najua hakuna chama ambacho kitaandikishwa kama chama cha siasa kikiwa na sera ya kuleta vurugu,"alisema.

Uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na rais umepangwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu, ambapo kwa hivi sasa vyama vinaendelea na kampeni.


IppMedia
 

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,963
2,000
Amani ya kweli ipo huku, malipo ya buku saba saba
JamiiForums2012431779.jpg
 

Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,387
2,000
Chadema wanajibidiisha sana kuchafua amani ya nchi ili wapate madaraka kiulaini.
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,607
2,000
Amani ya kweli ipo huku, malipo ya buku saba saba View attachment 1567025
KWani watu wa CCM hawapswi kuwa na pesa? Sisi CCM hatufanyi kazi za kujitolea kwa sasa, tulifanya hivyo wakati wa kutaka uhuru.
Sisi pesa tunazo kama chama na pesa zote zitaenda mpaka kwa wanachama wa chini, tofauti na nyie viongozi Pelee ndio wala pesa za chama wengine wajitolee.
 

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,059
2,000
Haya maisha yanastaajabisha, mtu anatumia miongo mingi kujijengea heshima halafu anatumia dakika moja tu kuharibu heshima yake yote.
 

parts

JF-Expert Member
Mar 31, 2018
1,732
2,000
opportunist tu huyu, kuna viashiria vingi vya uvunjifu wa amani ktk awamu hii, yeye amekuwa na msimamo gani?, amewahi hata kukemea?.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom