Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Frederick Sumaye ni mtu mwenye bahati sana maishani mwake. Ni waziri mkuu pekee katika historia ya Tanzania, ambaye amewahi kushikilia cheo hicho kwa muda wa miaka 10. Haijawahi kutokea, siku zote kazi ya uwaziri mkuu inachukuliwa kama vile ina mkosi. Imejaa lawama, imejaa mitihani mingi sana. Lakini katika miaka hiyo 10 ya Sumaye akiwa kama mtendaji mkuu wa serikali ya awamu ya tatu iliyokuwa chini ya Mzee Benjamin Mkapa, aliwahi kusikika akisema kwamba hajui ni kwanini nchi hii ni masikini.
Alikuwa akilipwa mshahara mkubwa, akitunzwa vizuri, akihakikishwa kila aina ya msaada kikazi, lakini hakuwa akifahamu ni kwanini Tanzania ni masikini( Hata JMK na yeye aliwahi kuongea maneno ya fedheha kiasi hicho). Ni mpaka miaka 10 yake ya uwaziri mkuu ilipomalizika, wakati alipokwenda kuongeza elimu huko Marekani, ndipo eti akaja kufahamu matatizo ya Tanzania ni yapi!.
Namtazama waziri mkuu wa awamu ya tano Kassim Majaliwa Majaliwa jinsi anavyochapa kazi. Jinsi anavyowahoji watendaji wa serikali akiongea kwa mamlaka makubwa huku akiwa anazo taarifa zote za uzembe wa yule anayehojiwa, kwa kweli anautendea sana haki wadhifa wa uwaziri mkuu. Sidhani kama KMM akihojiwa leo hii anaweza bila aibu kusema kwamba hajui ni kwanini nchi hii ni masikini.
Frederick Sumaye ana bahati sana maishani, ushahidi wa bahati ya kuzaliwa unapatikana ikiwa mtu anaamua kwa makusudi kulinganisha uwezo wake kikazi ndani ya miaka 10 na uwezo wa Kassim Majaliwa ndani ya kipindi kisichozidi miezi minne. Natumaini Tanzania ya kesho na keshokutwa itakuwa na kina Sumaye wachache sana, pia ni matumaini kwamba itakuwa na kina Majaliwa wengi sana.