Sumaye awavaa Polisi mauaji ya Mwangosi, askari walioua kufikishwa kizimbani J'tatu ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye awavaa Polisi mauaji ya Mwangosi, askari walioua kufikishwa kizimbani J'tatu ijayo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Sep 8, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hebu tuipitie hii habari kisha tuichambue. Inahusu Sumaye kuwasemea mbovu polisi walioua na mpango wa kufikishwa mahakamani polisi hao

  Lilian Lucas, Morogoro

  WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuacha kutumia silaha za moto au nguvu ya ziada linapokabiliana na raia, badala yake litumie busara kutatua migogoro.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro, baada ya kufunga mafunzo wa wahariri wa vyombo vya habari yaliyohusu utawala, Sumaye alisema kufa mtu katika mapambano ya polisi na raia siyo kitu kidogo.
  Kauli hiyo ya Sumaye inaonekana kuwalenga polisi ambao wanadaiwa kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Televisheni ya Channel Ten mkoani Iringa, David Mwangosi.

  Mwandishi huyo aliuawa Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Nyololo, Iringa kwa kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa bomu, wakati polisi walipokuwa wakiwazuia viongozi na wanachama wa Chadema kukusanyika wakati wakifungua tawi la chama hicho kijijini hapo.

  Mpaka sasa askari watano wa jeshi hilo, akiwamo anayetuhumiwa kumlipua kwa bomu marehemu Mwangosi, wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa na jeshi hilo mkoani Iringa.

  Sumaye alisema kuwa katika siku za karibuni, polisi wamekuwa wakikimbizana na raia mara kwa mara pamoja na kutumia silaha na nguvu isiyo ya kawaida hata pale pasipostahili. Jambo ambalo alisema siyo sahihi kwa mustakabali wa jeshi hilo.

  “Si lazima sana kwa polisi kutumia silaha hasa za moto kila wakati. Nimekuwa nikitazama kwenye televisheni mara kwa mara na kuona polisi wakitumia silaha, hata sehemu za kuvunja nyumba tu huko vijijini.

  Nawashauri watumie busara,” alisema Sumaye na kuongeza:

  “Tusidhani risasi inaweza kutatua migogoro wakati wote. Risasi inaweza kuharibu kila kitu, zitumike pale inapokuwa ni lazima kwani Watanzania siku zote si watu wa fujo.”

  Alisema kutokana na tukio la hivi karibuni la kuuawa kwa mwandishi wa habari, Serikali, Polisi na vyombo vingine vya usalama, watakuwa wamejifunza kitu katika kutatua migogoro na migongano baina yao na wananchi wanaowaongoza.

  Alisema kwamba Jeshi la Polisi nchini linapaswa kutambua kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi ikiwa ni pamoja na kutumia risasi kutawanya raia, si suluhisho la migogoro baina yake na wananchi, bali kinachohitajika ni busara zaidi, ili kuepusha maafa.

  Akizungumzia suala la polisi kupambana na wanasiasa alisema, mazingira ya siasa kwa sasa yamechangamka zaidi ikilinganishwa na yale ya zamani na kwamba wakati mwingine wanasiasa wamekuwa wakichangia vurugu na hivyo kulilazimisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu ya ziada.

  Watuhumiwa wa mauaji ya Iringa

  Katika hatua nyingine askari watano wanaoshikiliwa Iringa wanaendelea kuhojiwa, huku taarifa zikieleza kuwa wanaweza kufikishwa mahakamani Jumatatu, kutokana na kushindikana jana.

  Jana, taarifa zilisambaa kwamba askari hao walikuwa wafikishwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, lakini hadi jioni, walikuwa hawajafikishwa. Pia hakukuwa na taarifa zozote za nini kilikuwa kinaendelea.

  “Ni kweli walitakiwa wafikishwe leo, lakini hadi sasa hawajafika, wakifika nitawaeleza,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa mahakama hiyo jana.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda hakutaka kueleza lini watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa kile alichosema kwamba kwa sasa yeye siyo msemaji wa jambo hilo.   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Nina mashaka kuwa kama kesi ikifika mahakamani jtatu, basi ndio mwisho wa mchezo wote. Hakuna cha majibu ya tume zilizoundwa wala nini sababu ZITAKUWA ZINAINGILIA UHURU WA MAHAKAMA. serikali inataka kucheza kamchezo hapa kama kwa Ulimboka
   
 3. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huyo kamanda Kamuhanga pia ni mtuhumiwa anatakiwa afikishwe mahakamani pamoja na hao polisi wenzie. Hii serikali inapenda kuwalinda hata watu wasiostahili kulindwa, ndio maana tunaamini ulikuwa mpango uliopangwa.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  I do believe that the outcome will be the same as that of Imran Kombe killings, wale wachimba madini waliouawa sinza, kesi ya Dito, Ulimboka, etc etc, mashaka yako ndio utakuwa ukweli wenyewe, we have been there and that is where we will go again. Na watauawa wengine na hali itakuwa hivyo hivyo, mark my words.
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sumaye bado hajasema lolote kama hakulaani unyama huu. Inashangaza rais amekaa kimya huku akiendelea kuruhusu watendaji wake wazidi kuwaudhi wananchi kwa kusema eti kifo cha Mwangosi kimesababishwa na CDM wakati ukweli ni polisi waliotumwa na CCM. Huu ni woga kwa upande wa Sumaye ingawa amejiridhisha kuwa amejitenda na mauaji. Huwezi kujitenga na mauaji na mateso ya watanzania ukabakia ndani ya CCM. Kama si woga basi ni unafiki na undumila kuwili.
   
 6. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  siasa hizi...ili kumfikisha mtu mahakamani ni lazima kumfungulia shtaka......sasa ndiyo hapo inapokuwa kazi hasa kunapokuwa na mashinikizo ya siasa.....sijui watawafungulia mashtaka gani.......
   
 7. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Katika watuhumiwa watakaofikishwa mahakamani kwa nini RPC IRINGA nae asijumuishwe?
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Sijaona alichosema cha maana zaidi ya kurudia mambo ya kawaida ambayo yapo kwenye mitandao! Aliyosema siwezi kuyafananisha na level yake.
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hapa tuna sahau matukio haraka sana mfano suala la dr ulimboka limeisha kimya kimya na hili la mwandishi pia litaisha hivyo hivyo
   
 10. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Wanataka kuua hili soo. Mahakama ya nini kwa sasa wakati kamati haijatoa majibu? Si wangesubiri? Ili kesho waseme kuwa jambo lipo mahakamani.
  Sumaye hana jipya katika hili, anawapa tu ahuweni polisi. Anaposema mazingira ya siasa yamechangamka anatakiwa awaambie polisi jinsi ya kubadilika na kuendana na wakati wa sasa kisiasa. Huu wakati watu wanadadisi na siyo tu zidumu fikra za mwenyekiti. Unatakiwa uelimishe watu kwa nini wasikutanike na uwe tayari kusikiliza hoja zao. Siyo kuwaambia tuna nguvu, ondokeni tutatumia nguvu. Nguvu ya umma ni kubwa sana, na ndo maana hata kamuhanda anashindwa hata kuliongelea hili.
   
 11. I

  Ichobela JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Hana jipya la kutuambia watz,hapa anatafuta umaarufu wa kisiasa tu! Wakati wa mauaji ya wafuasi wa CUF Zanzibar alikuwa na cheo gani na alichukua uamzi gani? Kwa nn asiyasemee mauaji hayo kwanza ndo atueleze huu upuuzi. Wasifikirie watz wa enzi za uhuru ndio watz wa leo!
   
 12. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Sumaye ameongea kauli LAINI sana..ningetegemea azindue Singo ya RPC KAMHANDA kuwajibishwa.
   
 13. M

  Mndokanyi JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa,aliyeamuru kuuliwa kwa mwandishi ni huyo kamanda,anatakiwa aunganishwe na hao watuhumiwa wengine.
   
 14. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wanasheria hebu tusaidiane hapa haya ambayo yanafanyika ni sawa mbele ya jicho la sheria?Nani anamustaki nani? Wapelelezi ni polisi washatkiwa ni polisi...kamati zilizoundwa na IGP na Waziri matokeo yao yatatumika wapi?bado tunakumbukumbu ya kesi ya kinazombe jinsi walivyoigaragaza serikali....eti ushahidi aukutosha na mpaka leo serikali wameshindwa kumkamata muaji ambaye alikuwa polisi.Wasiwasi wangu muhusika mkuu kwenye hili anaweza asikamatwe tukaishia kama ya kina zombe
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  wewe nawe!!
  utadhani huna kichwa! Unakeraje
   
 16. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Huo ni mwanzo tu.
  Watajichanganya mpaka basi zile picha zimewaweka uchi.
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Sumaye ni mnafiki sana wakati akiwa Waziri Mkuu mbona akusema lolote polisi walipowauwa wapemba, kwenye maandamano
   
 18. m

  mosagane Senior Member

  #18
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini alishawahi kusema kuwa mtu anayetumia kalamu kuingia madarakani,akiingia atatumia risasi nafikiri hiki ndicho alicho maanisha
   
 19. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hajasema lolote. Tunahitaji smart statements which are action oriented and result based.
   
 20. O

  Original JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pamoja na hao askari kukamatwa lakini si hekima kutowakamata wafuatao: Mkuu wa mkoa wa Iringa, Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa, Mkuu wa wilaya husika pamoja na mkuu wa jeshi la polisi wilya husika. Watu hao ndiyo walitoa maelekezo na amri ya nini kifanyike. Waziri wa mambo ya ndani pamoja na IGP sielewi wanangoja nini kujiuzulu.
   
Loading...